Tafakari ya leo tunaangalia kwa nini mafundisho ya yesu yaliweza kuvuta
watu wengi na amekuwa na wafuasi wengi hata baada ya kupaa kwake na kurudi kwa
baba Mbinguni; tunaangalia kuwa injili yote ambayo inaendelea kufundishwa leo
ni mafundisho ya Yesu kwa wafuasi na waamini wake; alifahamika kwa wengi kuwa
yey alikuwa ni Rabi yaani mwalimu. Tunajua kuwa Yesu alikuwa akifundisha kwa
maalaka ambayo hata pale alipokuwa akisisitiza jambo daima alikwenda mbali zaidi
ili wafuasi wake waweze kuelewa na kuishi kulingana na mafundisho yake; Injili
inaonyesha maisha ya yesu alivyoishi hapa dunia huku akiwa akitimiza kazi
ambayo alitumwa kuja kuimamilisha ya wakovu wetu sisiwanadamu.
Tukiangalia
mafundisho ya Bibilia tunaona kuwa kulikuwa na kila aina ya watu ambao walikuwa
wakimsikiliza kila wakati alipokuwa akihubiri. Kulikuwa na wataalamu wa sheria,
walimu wa masinagogi, na watu wa kawaida. Na tukifuatilia sana mafundisho yake
Yesu alikuwa akifundisha katika mtazamo tofauti alipokuwa akiongea na watu wa
kawaida na pale alipokuwa akiongea na wataalamu wa sheria vile vile mafundisho
yake yalikuwa yakibadilika.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa sio tu alikuwa mwalimu bora lakini
alikuwa pia akiwaandaa wale mitume kumi na wawili ili pindi yeye atakaporudi
kwa baba waweze kufanya kazi hii ya ukombozi kwa nguvu ile ile. Mafundisho yake
yalikuwa yamejaa zaidi mifano ambayo ilikuwa inawasaidia sana wafuasi wake
kulelewa nini alikuwa akifundisha na kuwawezesha kufuata kwa urahisi zaidi; na
alikuwa akitumia mifano ambayo ilikuwa rahisi sana kueleweka kwa mtu yeyote
Yule; alikuwa akitumia mifano ya kawaida ambayo iko katika maisha ya watu ya
kila siku; mifano ya vitu kama mwanga; mlango; zabibu; mchungaji; ni mifano ya
kawaida ambayo ilikuwa ikipatikana katika maisha ya jamii husika na ilikuwa
ikieleweka kwao kwa haraka na kwa urahisi zaidi;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa ili tuweze kutimiza wajibu wetu vizuri
katika maisha yetu ya kila siku lazima Yesu kupitia mafundisho yake anatukumbusha
kuwa tunatakiwa kuwa watu wa furaha daima tukionyesha tabasamu wakati wote wa
utumishi wetu na kuongea katika lugha na
misemo ambayo ni rahisi kueleweka kwa kila mtu kulingana na mizingira ambayo
wapo; tukisoma Injili ya Mathayo 10:16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya
mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua. Yesu aliwapa maelekezo mitume wake ya kufanya
kazi ngumu lakini wawe na busara ya khali ya Juu na kuwaelimisha kwa mifano ya
vitu vitokanavyo na mazingira yao;
Tafakari yetu inaendelea kutoa mafundisho ya
Yesu tukisoma Injili ya Marko 4:34 wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi
wake mwenyewe mambo yote kwa faragha. Mafundisho yake kwa mifano daima yaliweza
kuwaunganisha wafuasi wake kwa haraka zaidi na katika uelewa mpana. Mfano
hadithi ya Mototo mpotevu fundisho ambalo liko kwetu sote kupitia hadithi hii
ni kuwa jinsi mungu anavyotupenda hata kama tutakuwa tumemkosea vipi kama tu
kwa dhati kabisa tutakiri udhaifu na makosa yetu yeye atatupokea na kutufanyia
karamu kubwa. Huu ulikuwa ni mfano wa kawaida katika maisha ya kila siku.
Tafakari yetu leo inatukumbusha pia kuwa Yesu pia alikuwa akifundisha
huku akitoa kauli za kutisha ili kuwaleta karibu wafuasi wake wawe na woga wa
kuogopa na kutenda mema; tukisoma Mathayo 5: 29-30 Jicho lako la
kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako
kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako
wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako
kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Au tukisoma pia Mathayo 7:3-5 Basi,
mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo
ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au
utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna
boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe,
itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema
kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. Hizi ni baadhi tu ya mifano
ambayo ilikuwa inawagusa watu na wanaogopa na kuupokea ujumbe vile ambavyo yesu
alitamani uwafikie kwa haraka na kwa ubora wake ili kila mtu aweze kuishi
maisha yaliyo bora; hivyo kama nasi tunatamani kuhubiri mafundisho yetu kama
Yesu alivyo fanya lazima tuwatishe watu ili washituke na kuamaka;
Tafakari yetu inatuhimiza kuwa Yesu alikuwa akifundisha kwa semi fupi
fupi ambazo zilikuwa ni rahisi kwa wafuasi wake kukumbuka na kuweza kuzifuata
kama vile alivyokuwa akifundisha tukisoma Injili ya Luka 6: 36-38 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na
huruma. Msihukumu,
nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi
mtaachiliwa. Wapeni watu
vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata
kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho ndicho mtakachopimiwa. Na mfano mwingine ambao ni Mzuri ambao Yesu
aliutumia alipokuwa akihubiri ilikuwa sheria ya dhahabu Luka 6:29-31 Akupigaye
shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na
kanzu. Mpe kila
akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Na kama
mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. Alikuwa daima
akifundisha kwa ufupi lakini maneno yake yalijaa hekima na busara na ni rahisi
kuyashika na kuafuata.
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa Yesu alikuwa akitumia mbini nyingi
ili kuhakikisha kuwa wafuasi wake wanaelewa mafundisho yake na kutekeleza kile
ambacho alikuwa anatamani wao wafuate ili waweze kupata wokovu; alifundisha kwa
kuuliza maswali kila alipokuwa akifundisha; Mathayo 16:26 Kwani
atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au
mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Mathayo 22: 20-21 Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii,
na anwani hii? Wakamwambia, Ni
ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu
yaliyo ya Mungu. Alikuwa anatumia vile mtindo kurudia rudia akijua kuwa kuna
wakati mwingine wafuasi wake wasikie jambo hilo mara kwa mara; ama kuhusu kifo
chake na ufufuo wake;
Marko 8:31 Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa
Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani,
na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. Marko 9:31 Kwa sababu
alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa
katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu
atafufuka. Marko 10: 33-34 akisema,
Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa
wakuu wa makuhani na waandishi, nao watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa
Mataifa, nao
watamdhihaki, na kumtemea mate, na kumpiga mijeledi, na kumwua; na baada ya
siku tatu atafufuka.
Hii ndio tafakari ya leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment