June 27
Mathayo 6: 5-7
Tafakari ya leo inatukumbusha kuhusu utekelezaji wa majukumu
yahusuyo imani ambayo yanampendeza Mungu. Je Mungu anapenda sadaka tunayoitolea
kwake iwe ya aina gani? Je sisi tunapomwomba au kumtolea sadaka tunakuwa katika
msingi wa namna gani ni ule unaopendeza Mungu au tunakuwa wanafiki mbele ya
macho ya mataifa? Tukisoma bibilia tunaona kuwa Mungu anataka Moyo wa kweli,
moyo thabiti ambao unajitoa kweli kwa Mungu. Mungu hataki mtu mwenye sura mbili
ambazo zinatofautiana na ukweli wa Moyo wake; Mungu hajali kuhusu mwonekano
wetu wa nje bali anataka mwonekano wetu wa ndani ambao unatakiwa kuwa umejaa
ukweli na imani: Mungu anatazama unyenyekevu wa mioyo yetu; Mungu anatak kuona
utakatifu wa mioyo yetu; na sio unafiki wa mioyo yetu. Mungu aliuona unafiki
huu toka kuumbwa kwa dunia; tukifungua bibilia tunaona tatizo la unafiki liko
toka katika kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana. Kwa msingi hii Hata
Mwokozi wetu Yesu alionyesha kwa vitendo unafiki ambao ulukuwako katika Nyumba
za ibada; Unafiki ambao ulikuwako miongoni mwa wanasheria; hata kati ya mitume
wale 12 kulikuwako na unafiki pia.
Tafakari yetu leo inatukumbusha
kuwa tukimsoma nabiia Amos katika sura
ya 5: 21-23 Mimi nazichukia
sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za
kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka
zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana
sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu. Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama
maji makuu. Katika maneno mengine
Mungu anatufundisha kuwa katika vitu vyote ambavyo nimewapa; katika vitu vyote
anbavyo vimevumbuliwa; katika vitu vyote ambavyo nimeamsrisha sisi tumeshindwa
kuvitekeleza ipasavyo na badala yake tumevigeuza na kuvudharau na kufanya mambo
tujuavyo sisi; hata kuomba tuonavyo sisi inafaa; hivyo hata tunavyoomba
tunaishia zaidi kujipamba kwa nje na sio kwa ndani; huu ndio unafiki ambao Yesu
aliukataa.
Tunavyoendela na tafakari yetu hebu
tuangalie Ole ambazo Mathayo alizitoa katika sura ya 23:13-24 Ole wenu waandishi na Mafarisayo,
wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe
hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie. [Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo
mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.] Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa
mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili
zaidi kuliko ninyi wenyewe. Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu
atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu,
amejifunga. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya
sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale
mengine msiyaache. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na
kutokuwa na kiasi. Ewe
Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa
safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa
mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na
watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, Enyi nyoka, wana wa
majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa mnafiki hujifanya
kuwa ni mwenye haki kwa mwonekano wa nje; lakini kwa mwonekano wa ndani sinyo
alivyo; maisha yake yamejaa uwongo na mara nyingi ikiwa mwongo mwonekano wako wan
je unakuwa na tofauti na mwonekano wa ndani; hivyo mtu wa namna hiyo anakuwa
sio mwaminifu; sio mkweli; mpenda kujisifu hata kwa vitu ambavyo hawezi
kutimiza; anataka kupata kibali kutoka kwa watu wanaomzunguka na kupendwa. Je
wewe unatabia hiyo? Bwana wetu yesu Kristo alitutaanzarisha kuwa tukisoma
Mathayo 6: 1-4 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi
mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu
aliye mbinguni. Basi wewe
utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika
masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin,
nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono
wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini
atakujazi. Hii ni taathari ambayo Bwana wetu Yesu aliitoa kwetu ili kuwa
wakamilifu wa kweli;
Tafakri ya leo
inatukumbusha kuwa lazima tujitambue kuwa sisi ni wenye dhambi na tumemkosea
Mungu Ukisoma warumi 3:23 Ukisoma Mithali 20:9. Tunatakiwa kuelewa kuwa Yesu
alikufa kwa ajili ya dhambi zetu Warumi 5:8 na lazima tuwe tayari kupokea
matokeo ya dhambi zetu Warumi 6:23 na Yatupasa kuomba msamaha wa dhambi zetu
Matendo ya Mitume 20:21/ 3:19. Tusipokuwa wanafiki ni rahisi kujenga imani yetu
ya kweli juu ya Mungu. Huu ni wajibu wetu wa msingi na tunapaswa kuutekeleza
bila shuruti;
Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment