June 11
2 wakorinto 12: 7-10
Tafakari ya leo tunaangalia jinsi maumivu katika maisha yetu kama
yanakuwa na fundisho lolote au yanaishia tu kuwa maumivu ambayo yanafanya
maisha yetu kuwa magumu na ya kusikitisha. Tunajifunza kutoka kwa Mtume Paulo
jinsi ambavyo alivyokuwa akikumbana na maumivu wakati alipokuwa akihubiri neno
la Mungu kwa mataifa tukisoma waraka wa 2 Wakorinto 11:25-27 Paulo anatukumbusha
kuwa Taabu na maumivu hatuwezi kuyakwepa katika kutafuta uzima wa milele na
maisha bora ya baadae; Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa
mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za
wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za
mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika
njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. Hivi vyote hatuwezi kuvikwepa;
Tafakari yetu leo inatukumbusha hata ndani ya familia zetu
tabu na maumivu tunakabiliana nazo; lakini tunatakiwa hizo changamoto tuweze
kuzikabili vizuri na kuzishinda kwa ufanisi kwa kuzingatia neno la Mungu;
katika familia zetu tunakabiliwa na maumivu yatokanayo na magonjwa; maumivu
yatokanayo na maisha kama maisha ya ndoa; khali ngumu ya maisha kutokana na umasikini;
kama Mtume Paulo alivyomwomba Mungu amwondolee maumivu na Taabu ili aweze
kufanya kazi ya uchungaji zaidi lakini Mungu alimjibu kwa namna tofauti kwani
kutokana na taabu na maumivu watu wengi waliokolewa na kumrudia Mungu. Yesu
alipata Tabu na maaumivu aliposulubiwa msalabani.
Tafakari yetu ya leo kama ilivyokuwa kwa Mtume Paulo tulio
wengi hatuoni dhumuni la taabu na muumivu mwanzoni; tunatakiwa tuombe neema ya
kutambua taabu na maumivu yetu kupitia jicho la mungu toka mwanzo ili tuweze
kusherekea utukufu wa Mungu kwa dhumuni ambalo ameliweka katika shida zetu; Tunatakiwa
kuimarisha imani yetu kwani Imani inamchango mkubwa sana katika taabu na
maumivu; tunatakiwa kumwomba Mungu atuonyeshe dhumuni la taabu na maumivu, na
kutuimarisha ili kutuwezesha kuzikabili hizo changamoto zote;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Maumivu na taabu yana
nguvu sana kama Paulo alivyosema neema yangu inatosha katika madhaifu na mapungufu
yetu. Hivyo tunatakiwa keweka neema ya Mungu mbele na ili tuone dhumuni la maaumivu
na taabu ili tupate nafuu; Mauumivu na Taabu ni kama taa za taadhari ambazo
zinaashiria kuwa kuna jambo linaweza kutokea kama hatutakuwa makini katika maisha
yetu; hatutakiwi kudharau taa hizo hivyo haitupasi kudharau maumivu na shida
zetu bali tutafute neema ya Mungu katika kujua sababu ya Maumivu na tabu zetu
kwa utukufu wa Mungu;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wakati mwingine maumivu na
taabu huwa ni chachu za mabadiliko ambayo Mungu hutaka sisi tuyapitie;
tukumbuke kuwa Mungu ni Yule Yule; Mungu hataki watu tupate taabu na maumivu
lakini wakti mwingine anafanya katika kutujengea nidhamu; kutufundisha na
kutuongoza sisi tupite katika njia ambayo ni sahihi; sio kuwa Mungu ana hasira
au hatupendi bali anatupenda sana na kutujali; Tatizo letu sisi hatuko tayari
kubadilika hata katika Maumivu na Taabu zetu.
Tafakari yetu inatunyoshea kidole kuwa sasa ni wakati wa
kubadilika na kusisma imara ili kujiepusha na maumivu na taabu;
Hii ndio tafakari yetu ya Leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment