June 7
Mathayo 5:39
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuelewa
kwa nini Yesu aliwaambia wafuasi wake sentesi hii; pengine ni vyema kujua
mazingira na umati ambao Yesu alikuwa akiuhubiria tukisoma Mathayo 5:38 alianza
kwa kusema kuwa Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa
jino; Lakini mimi
nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume,
mgeuzie na la pili. Yesu alikuwa
ameziangalia sheria zilizokuwa zikitumika wakati huu kama tukisoma Kutoka 21:24
ilikuwa ikisisitiza kuwa jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa
mkono, mguu kwa mguu; adhabu hizi zilikuwa zikitolewa katika wakati huo
ili kutenda haki katika mazingira yako kama kitabu cha Kumbukumbu la Torati 19:
20-21 Na watakaosalia watasikia na
kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa
jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa katika kipindi hicho sheria ambazo zilikuwa zikitumika
zilikuwa zimetawaliwa na ulipizaji kisasi; kila mwenzako anachokufanyia na wewe
mfanyie hivyo hivyo; lakini mafundisho ya Yesu Mlimani yalikuwa yakilenga
kuondoa dhana hii ya kupipiza kisasa na kuanza kujenga dhana ya msamaha dhana
ya upendo; dhana ya kuanza kuuliza maswali kwa nini ? je nikusaidie vipi; Yesu
alianza kuleta dhana ya mazungumzo katikati ya tukio; yesu alikuwa
anatufundisha kuwa tunatakiwa kuwa na subira tukisoma Warumi 12:17 Msimlipe mtu
ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Au tukisoma
Mithali 24:29 Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa
na tendo lake.
Tafakari
yetu leo inatukumbusha kuwa sisi kama wakristo tusijihami wakati wowote wa
fujo, hujuma au vitisho; yesu hakusema kuwa hatuna sababu ya kujilinda lakini
kama wakristo tunatakiwa kuonyesha upendo wetu tunavyokabiliana na matukio ya
namna hii katika maisha yetu na tusisababishe sisi wenyewe kufanya vitu ambavyo
vitaashiria hasira, chuki na fujo; yesu anasisitiza sisi kufanya retreat katika
wakati wote ili kuepuka mapigano, fujo na kuchukua hatua ya kujilinda wenyewe
na kuomba msaada wa nguvu za sheria kama Polisi. Mathayo 26:51-53 Na tazama, mmoja wao waliokuwa
pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa
Kuhani Mkuu, akamkata sikio. Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali
pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba
yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
Hivyo kazi ya malipizi tumwachie Mungu yeye anajua lini na wapi anaweza fanya
malipizi.
Tafakari yetu leo inasimama katika
kuepuka kulipiza kisasi; kugeuza shavu la kulia ni dalili ya unyenyekevu; ni
dalili ya kukomaa kimaadili kama mkristo; hata kama unatukanwa huna haja ya
kujibu matusi unatakiwa kuonyesha upendo wa ajabu ili hata Yule ambaye
anakutukana au anataka kukufanyia fujo atabadilika na kuacha fujo; Yesu
anatuonyesha kuwa fujo nyingi ni sababu ya kuvunjiana heshima, dhuluma.
Ukiangalia magovi mengi husababishwa na majibishano, kutuvumiliana, dharau,
hivi unyenyekevu huweza punguza matatizo haya yote; Hivyo kugeuza shavu la
kulia ni kuonyesha unyenyekezu na kufufua dhana ya mazungumzo.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa utu
wetu unakuja kwa sababu tumeumbwa na Mungu; umuhimu wetu unakuja kwa sababu
tumeitwa na Yesu ili tuibadilishe hii dunia; na Nguvu yetu inatokana na roho
Mtakatifu ambaye ametujaza sisi nguvu ya kupokea matusi kutoka kwa wengine na
kuyajibu kwa busara na upendo kama Yesu alivyokuwa akiwajibu wale wote
waliokuwa wakimtukana.
Tafakari yetu inatuhimiza kuwa kugeuza
shavu la kulia maana halisi tusiwajibu wale wanaotutukana kwa matusi bali kwa
unyenyekevu na upole; wale wanaotuchukia kwa chuki bali tuwajibu kwa upendo.
Tuige mfano wa Yesu yeye alikuwa kweli hazina ya Uvumilivu,unyenyekevu, upendo
na msamaha.
Hii ndio Tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment