June 13
Yakobo 1:19
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuchukua taadhari kabla hatujechukua hatua yeyote muhimu ambayo
inayahusisha maisha yetu kwa ujumla; kwani kama hatutachukua taadhari tutaishia
kupata maumivu na sio faraja ambayo kama tunaitegemea katika maisha yetu; Taadhari hii tukiifuata inavyopasa itatusaidia
katika katika maisha yetu ya kila siku
na maandalizi yetu na mungu. Mfano wa kawaida tu ni kuwa kama tunachukua
taadhari na kupata nafasi ya kusikiliza
nini watu wengine wanatuambia na tukawapa nafasi ya kutosha
watatusimulia mambo mengi kuhusuwao wenyewe; lakini kama tutakwa wavumilivu, na
wasikivu zaidi watakusimulia mambo ya ndani zaidi ambayo hata hukutarajia
kuyasikia. Na hivyo pengine ukapata nafasi ya kumsaidia mtu zaidi, kwa sababu
tu umechukua taadhari, hujekurupuka kumkatisha katika maelezo ya shida yake,
hivyo umemwelewa sana na unakuwa umepata nafasi nzuri ya kumsaidia.
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuwa tusipokuwa makini kila kitu tukifanyacho au tunachokifikiria
kinaweza kuwa na mwisho mbaya; hata vitu ambavyo tayari vimetayarishwa kwa
ajili ya matumizi au kutusaidia sisi wenyewe; Kama vitu au mawazo yetu
hatutaytumia kwa namna inayofaa. Mwamba mdogo tu katikati ya bahari unaweza
kusababisha madhara makubwa kama Nahodha akuwa makini wakati alipokuwa
akiangali na kuendesha chombo chake; hivyo yatupasa kuwa makini tukikumbuka
kuwa kila kitu hata kama ni kidogo bado vina umuhimu mkubwa sana. Kwa hiyo
yatupasa kuchukua taadhari katika kufanya maamuzi yetu kwani kila kitu ni
muhimu. Hivyo yatupasa kuwa makini kama 1Petro 5:8 anavyo tufundisha Mwe na kiasi na
kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa lazima tutumie busara na hekima katika maamuzi yetu kama
kitabu cha mithali14:15 kinavyofundisha Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara
huangalia sana aendavyo. Kwa kutafakari
na kuchukua taadhari kabla ya kufanya maamuzi ni jambo la hekima kubwa; hekima
hiyo ndio tunayoihitaji sana katika masia yetu ya kila siku; Busara na hekima
yetu itatufanya sisi kuwa na msimamo na kufanya maamuzi sahihi kama Paulo
alivyosema katika waraka wake kwa Waefeso 4:14 ili tusiwe tena watoto
wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa
hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Tafakari inatuonya kuacha kuwa wazembe na wazivu katika
kuchambua. Kufuatilia, kuangalia na kusikiliza ili mawazo na matendo yetu
yaweze kulingana na faida ambayo tunaisubiria kwa hamu kubwa , na sio kukurupuka
na kujikuta tukiishia kwenye korongo kwa kushindwa kuangalia na kupima hitaji
linalohitajika kabla ya kufanya maamuzi. Tumejaliwa elimu na maarifa katika
kutekeleza majukumu yetu; bibili ni chanzo kizuri sana cha maarifa na kina
dhana zote nzuri za kutusaidia kuweza kuruka bila kupata athari yeyote ile; au
kusikiliza bila kupata hasiri; lakini mwenyezi Mungu bado ametuachia maamuzi ya
kufanya mambo yetu kwa busara na hekima bado yako juu yetu; ni wakati sasa
umefika wa kubadilika na kutumia busara na taatdari katika maamuzi yetu yote;
Hii ndio tafakari yetu ya Leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment