June 9
Mithali 29:18
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa ili kufikia malengo yetu ya kufurahia utukufu wa Mungu
lazima tuishi tukiwa na malengo au mwelekeo ulio sahihi; tukumbuke kuwa mtu
bila malengo ni sawa na mtu kukosa mwelekeo wa kesho. Na Mtu bila kuwa na
malengo daima atarudia maisha yake ya Jana. Tukumbuke kuwa maono au uwezo
wa kuona nini kiko mbele yetu ni daraja
muhimu sana kati ya sasa na baadae. Bila uwezo huo tujue kuwa lazima
tutaangamia, tukumbuke kuwa maono
yanatoa nafasi nzuri sana kwa maumivu yetu kupata sababu ya kufany jambo. Wale wote ambao hawana maono ya maisha yao
wanatumia muda wao mwingi kuongelea njia ambayo inawaletea ugumu wanapojaribu
kujiondoa katika maumivu ya maisha. Wengi
wetu tunapitia maisha yetu bila kuelewa majaribu yaliyo mbele yetu. Tunatumia muda
mwingi kutembea katika barabara ya manunguniko tukiamini kuwa kila jaribu
ambalo liko mbele yetu ni tatizo na lazima tulikimbie.
Tafakari yetu leo hebu tuliangalie hili neno maona kwa maana pana zaidi;
kwa tafsiri rahisi ni nini tunaona, na kwa namna gani au kwa njia ipi tunaona;
maono ni kama darubini ambayo inatusaidia sisi kuelezea matukio ndani ya maisha
yetu, namna ambayo tunawaona wenzetu na hata tunavyo weza mwelezea Mungu. Tatizo
nki kuwa kama tuna mikwaruzo katika miwani yetu ni wazi kuwa tutamwona kila mtu
kati yetu kuwa anamikwaruzo pia; lakini katika mazingira ya namna hii tatizo
litakuwa kwetu kwa sababu maono yetu yatakuwa sio sahihi. Tuelewe kuwa
kinachojitokeza ni kuwa akili yetu
inapokea picha kutoka kwenye macho yetu, mioyo yetu inatafsiri picha hizo. Kama
mioyo yetu inapata uchungu, au inakuwa na wivu, au inaumia au inaadhirika kwa
namna moja au nyingine maono ya moyo ndio yanaharibika. Tukisoma Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo
kweli itawaweka huru. Na kweli
inatokana na kuwa na maono sahihi na sio maono ya kujifanyizia.
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa maono sahihi lazima yatoke kwa mungu, kama kitabu cha mithali 15: 22-24
kinavyotukumbusha Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa
washauri huthibithika. Mtu
hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema
kama nini! Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke
katika kuzimu chini. Kama nilivyosema
hapo juu maono lazima yatoke kwa Mungu, wajibu wetu sisi kama binadamu ni
katika kusaidia kukamilisha na kutimiliza ndoto ya maono hayo ili iweze timia. Ukamilifu
wetu sisi binadamu lazima uwe katika kulielewa neno la Mungu kwa kusoma na kwa
mafundisho yake. Kama Mithali 16:9 inavyosema Moyo wa mtu huifikiri njia
yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake. Au
ukisoma Zaburi ya 37:23-24 Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye
aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na
kumtegemeza
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa ili tuweze kuifikia
safari hii ya utukufu wa Mungu lazima maono na malengo yrtu juu ya Mungu
yatimie. Tumepewa uwezo wa maono lakini tatizo letu hatujui jinsi ya kutumia
maono haya katika kufanikisha na kufikia ushindi wa kweli. Akili yetu
imeendelea kufungwa Mioyo yetu imeendela kujaa kutu na kiburi na kushindwa
kuona maono yanayotufaa katika maisha yetu na kuishi kuwa na maono finyu ya
kibinadamu nay a kidunia ambayo hayatusaidii kwani upeo wake ni mdogo na wa kidunia
tu. Yatupasa kuamka sasa na kuwa na maono stahiki kwa utukufu wa Mungu na
maisha yetu. Kwani pale ambapo hakuna maono watu wangu wanaangamia.
Hii ndio tafakari yetu ya leo- Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment