June 28
Yohana 16:24
Tafakri ya leo
tujukumbushe umuhimu wa kufanya maombi ipasavyo ili tuweze kupata kile ambacho
kweli tunakihitaji kwa wakati muafaka; Tunatakiwa kukubali kuwa Mungu anajibu maombi yetu lakini pengine jibu
lake linakuwa hapana wakati sisi tulikuwa tumetegemea ndio; Tukumbuke kuwa hata
jibu likiwa hapana ni kwa ajili ya faida yetu sisi kama binadamu ambao hatuna
upeo wa kuweza kuona yale ambayo yako mbele yetu; Jukumu letu la msingi wakati
tukiwa tunafanya maombi tunatakiwa tuwe
watu tuliojaa uaminivu na ukweli na tujue kuwa ambaye anatawala maombi
yetu ni mmoja tu ndiye yeye ambaye ni Alpha na Omega; yeye ndio anayetufanya
tuyaelewe maisha yetu; tuyakubali na mwisho ndiye anayeleta uzima. Je tunapoomba
maombi yetu tunaomba katika njia sahihi na lengo sahihi; Yakobo 4:3
anatukumbusha Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa
tamaa zenu. Tukumbuke kuwa lengo kubwa sala kwanza ni kumshukuru na
kumwabudu Mungu kwa wema na utukufu wake. Je tunapomwomba Mungu tunakuwa tayari
tumekiri makosa yetu na kuomba msamaha?
Tafakari yetu inaendelea
kutufundisha kuwa mkono wa Mungu sio mfupi katika kutuokoa au sikio lake ni
bofu kusikia, tatizo ni dhambi zetu ambazo zinakuwa zinatutenganisha sisi
nayeye hata asisikie shida na maombi yetu kwa wakati kwani anatusubiri sisi
kwanza tujitambue kuwa tuna dhambi nasi tuweze kukiri dhambi zetu na kasha kuomba
msamaha kabala ya kuomba ili tupate msadda wa shida zetu. Isaya 59: 1-2 lakini maovu
yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole
vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu
zimenong'ona ubaya. Ezekiel 14:3 Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na
kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni
laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?
Katika Tafakari yetu leo tukumbuke kuwa ni jambo la muhimu
sana kudumisha uhusiano wetu mzuri wakati wote; kwa kufanya hivyo tutaweza
kushinda majaribu ya Shetani ambaye anasababisha maombi yetu yasipokelewe; Laki
kama tutadumisha na kujielekeza kwa
Mungu tutaweza kushinda kama Injili ya Yohana 15:7 Ninyi mkikaa
ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi
mtatendewa. Tatizo maisha yetu
bado tunayaishi katika ulimwengu wa dhambi na kiburi huku tukitegemea Mungu
asikilize shida zetu na kutubariki. Je Mungu anaweza kumbariki Mwenye dhambi
ambaye hajitambui na hayuko tayari kujuta dhambi zake? 1 Yohana 3:21-22 Wapenzi,
mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika
amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. Tukumbke kuwa hatuwezi kumzihaki Mungu
Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote
apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
Zaburi ya 66:17-20 inatukumbusha kuwa Nalimwita kwa
kinywa changu, Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu. Kama ningaliwaza maovu moyoni
mwangu, Bwana asingesikia. Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu. Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala
kuniondolea fadhili zake. Mara nyingi sana Maombi yetu hayapati kibali
mbele ya macho ya Mungu kwa sababu tunadhambi ambazo zinatakiwa tuziungame na
tuache kuishi katika dhambi ili sala na maombi yetu yapate kibali cha Mungu.
Tukitimiza hayo Mungu anaweza jibu maombi yetu kwa kadiri na namna ambayo sisi
tumemwomba; lakini jibu lake llinaweza lisije kaulingana na kalenda ya
mwombaji, anaweza hata tumia njia ya kuchelewesha kidogo ili kutufundisha sisi subira,unyenyekevu
na upole. Kusubiri ni fadhila moja kubwa sana katika maombi yetu.
Tafakari yetu vile vile inatukumbusha kuwa
tunaye mpatanishi ambaye anatuombea kwa Baba na hivyo ni wajibu wetu kuomba
kupitia yeye Mathayo 7:7-8 inavyotukimbusha Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni,
nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa
maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Ili tufanikiwe katika hili tusijenge tabia ya kumaliza ombi letu kwa kutaja tu
jina Yesu mwisho wa maombi yetu; bali tunatakiwa kuishi maisha ya utakatifu ili
sala zetu zipate kibali; lazima tuishi katika mapenzi ya Mungu. Jambo nyingine
lakuzingatia ili maombi yetu yapate kibali cha Mungu ni kuhakikisha kuwa kwa
wale wote wako kwenye ndoa wajue kuwa mahusuiano yao mazuri na utii miongoni
mwao ni kibali kikubwa katika usikivu wa maombi yetu; 1 Petro 3:7 Kadhalika
ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo
kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu
kusizuiliwe.
Tumalizie
tafakari yetu kwa kukumbuka tujijengee tabia ya ushindi kwa kuzingatia matendo
yetu mema, maisha bora yanyompendeza Mungu; Kutimiza wajibu wetu ipasavyo
katika jamii tukiendelea kuamini kuwa Mungu ndiye mwenye mamlaka na ndiye
mwenye mamlaka na pekee ndiye jibu la shida zetu kama Mtume Paulo 2 Wakorinto
12:8-10 aliposema Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba
kinitoke. Naye akaniambia,
Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi
nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu
yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na
adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
Mungu anatupenda sana na daima anajibu kwa wakati wake ambao ndio wakati
muafaka ambao unapita uelewa wa akili zetu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment