June 20
Yohana 17: 1-5
Tafakari yetu ya leo
inatukumbusha ombi ambalo Yesu, aliwaombea mitume wake wawe na umoja kama wao
walivyo katika ufalme wa mbinguni. Yesu aliwakumbusha mitume wake bila kujali
khali zao, wametoka wapi; wana nini wanapaswa kuwa wamoja. Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa watu wa mungu wametoka kutoka makabila yote; lugha
zote;mataifa yote;katika khali tofauti za uchumi. Ndio maana Yesu aliwaombea
wafuasi wake wawe na Umoja kama wao walivyo. Tunatoka katika mazingira tofauti
lakini wote ni zao lake yeye; tunajitenga na kuchukiana kwa sababu za tofauti
zetu na mazingira ambayo tunajijengea miongoni mwetu; mungu anataka sisi
kushirikiana pamoja kwa upendo wote;
Tafakri yetu leo
inatumumbusha kuwa tunatakiwa kufikiria katika akili zetu kuwa mimi ndio natakiwa kuwa sababu ya umoja wetu;
natakiwa nititoe kwako, niwe nawe na nishiriki nawe katika yale yote ambayo
yameelezwa katika amri ile kuu ya
upendo; kuwa Mkristo wa kweli na sio wa kuhudhuria katika makanisa ni kuishi
amri hii ya upendo kwa vitendo; na tukiishi kwa vitendo ndipo tutatekeleza
maana ya kuwa Mfuasi wa kristo; tukumbuke kuwa zawadi zote ambazo Mungu ametupa
sisi, zawadi za Muda, zawadi ya Nguvu, afya njema Mungu ametujalia sisi lakini
anataka zawadi hizi tuzitumie kwa manufaa ya wengine pia; heshima ambayo sisi
tunatamani kuwa nayo ndio iwe hsehima hiyo hiyo ambayo tunapaswa tuionyeshe na
kwa wengine; tunapaswa kushauriana; inatupasa kutiana moyo; yatupasa
kushirikiana kwa Yesu alivyotenda kwetu; Yesu daima anataka sisi tuwe chumvi
ambayo inaleta radha nzuri katika chakula. Wafilipi 2:2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, nia moja.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Jamii yetu leo kuwa ukweli sio kitu
ambacho kinapewa thamani ya kweli; Mungu katika mafundisho yake ukweli mmeweka
kuwa msingi wa kila kitu; tukiangalia zaburi ya 51:6 Tazama,
wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, au Zaburi ya 86:11 Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda
katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako; Wafilipi Ufunuo 21: 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote
kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa
katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Yesu alituombea tuwe na umoja akijua kuwa palipo na umoja ukweli hutawala
na amani itadumu, na palipo na ukweli na umoja unyenyekevu utatawala uwazi wa
mambo ya msingi yahusuyo amani yatafanyika, na mashauriano mema yatafanyika kwa
upendo mkubwa; ndio maana yesu alitaka tuwe wamoja tukiwa wamoja tutashirikiana
kwa ukaribu zaidi. Tutapendana na hata pale ambapo hatutakubaliana tutamaliza
tofauti zetu kwa upendo na hekima ya kweli. Yesu anatufundisha kuwa Maisha ya
Mkristo ni mchanganyiko wa vitu viwili yaani machungu na furaha; katika
machungu maisha yanakuwa yamegubikwa na mambo mengi ambayo yamejaa masikitiko,
taabu na mateso kwa baadhi ya yetu na wengine wakifurahi maisha yalijaa furaha
na starehe. Tukisoma Warumi 8:28 inatukumbusha kuwa Nasi twajua ya
kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika
kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Hivyo sisi sote pamoja na taabu zetu
na furaha zetu Mungu ametuita tuwe pamoja naye, Ndio maana yesu alituombea tuwe
wa moja katika umoja wetu tutaweza kusaidiana katika kyakabili maisha katika
khali yeyote ile;
Tafakari
yetu inatukumbusha kuwa katika umoja wetu hakuna magumu. Bali neema ya Mungu ndio
silaha ya kweli katika kupambana na majaribu yeyote yale. 2 Wakorinto 12:9-10 inatukumbusha kuwa Naye
akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.
Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu
yangu. Kwa hiyo napendezwa
na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo.
Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Pasipo
na umoja ni karibisho la udhaifu; bali tukiishia katiaka umoja tunajenga nguvu
ya ushindi. Ombi la Yesu aliloomba juu
wa wafuasi wake lilikuwa la maana na msingi mkubwa akitambua kuwa mitume wake
walikuwa ni watu wenye uwakilishi tofauti, utu tofuti na walikuwa wamekulia
katika mazingira Tofauti, walikuwa wengine ni wapole, waaminifu, wengine ambao
walikuwa tayari kwa shari; hivyo ombi lake juu yetu likuwa ni msingi mkubwa;
Yohana 17;
20-26 inavyotukumbusha Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe
katika kweli. Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakao niamini
kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami
ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba
wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja
kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika
katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama
ulivyonipenda mimi. Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo,
wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya
kuwekwa msingi ulimwengu. Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi
nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili
pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao. Umoja ni
silaha muhimu sana katika imani yetu.
Hii ndio tafakari yetu ya
leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment