January 26
Tafakari
ya leo tuangalie tatizo la kuvunjwa Moyo katika maisha yetu; Tabia hii hutendwa
sana pale ambapo unaonekana kuwa unafanya kitu sahihi lakini unapata matokeo
hafifu. Wakati mwingine unajiona kuwa unafanya kazi kwa bidii lakini mafanikio
hayaonekani na wale wanaokusaidia wanafurahia kushindwa kwako; upinzani uko
hasa kwa wale wanaofanya vizuri.
Na ukiangalia
sana hali hii ya kuvunjwa moyo inaumiza sana nafsi na moyo wa muhusika, wakati mwingine
unaweza kufikiria hata kuacha kile ambacho umepanga kukifanya hata kama
unafanya kwa maendeleo ya jamii yenye huhitaji; hata Yeramia alipatwa na khali
kama hii;
Lakini
tukumbuke kuwa pamoja na majaribu mbele yetu bado tunatakiwa kuwa watiifu na
kutathimini wito wa wajibu wetu kwa Mungu na Jamii; Tunatakiwa tu kujiuliza je ulifanyalo na unajikuta katia wakati mgumu
wa upinzani umeitwa na Mungu ulifanye?
Kama ndio
hata kama utavunjwa moyo kiasi gani hutakiwi kuacha kutenda kwani wakati
ukifika Mwenyezi Mungu atakuinua tu kama alivyo mwinua Yeramia alipokuwa
akipambana na matendo dhalimu ya Pashhur. Fundisho kutoka kwa Yeraamia ni kuwa
aliitwa na Mungu kwa kazi yake, pamoja kuwa hata yeremia alimkasirikia Mungu
lakini hakuweza kudharau wito na kazi ambayo mungu alimpa kuifanya na
aliifanya.
Tunatakiwa kuwa makini na
waangalifu na kutambua kuwa Mungu yuko nasi na tuendelee kujiombea na
kuombeana; Yeramia 20:11
anavyotukumbusha kuwa Bwana yu Pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa
hiyo hao wanaonionea watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili
watona aibu ya milele ambayo haitasauliwa kamwe. Hivyo tafakari ya leo
inatulumbush kuwa bwana akiwa upande wako hakuna yeyote wa kukushinda au
wakushindana nawe; mungu atawashughulikia iipasavyo wakati ukifika. Hivyo hatutakiwa
kuwa na wasiwasi.
Najua
kama binadamu wakati kama huu ambapo tunapovunjwa moyo tunajiangalia na
kujiuliza maswali mengi kwa nini iwe hivi, mimi ninatatizo gani? Na kwanini
naandamwa hivi kulikoni? Tunaishia kupata mfadhaiko ambao unaturudisha nyuma
katika jambo njema ambalo ulikuwa unatakiwa kulifanya. Yeramia anatukumbusha
kuwa tukiwa katika khali kama hii tunatakiwa tumwangalie zaidi Mungu na kujua
kuwa kamwe Mungu hawezi kutuacha katika wakati kama huu yeye anasimama kama
jemedari mkuu wakati wote wa majaribu. Jukumu ketu kubwa ni moja tu kumwomba
yeye na kumtumaini yeye kwa imani thabiti.
Leo tunapotafakati
kukumbuke kitu kimoja katika kila hali tutambuwe kuwa Mungu yu pamoja nasi
anatembea sambamba nasi, anatuongoza na kutuepusha na kila hatari ambayo
inakuja mbele yetu yeye hutukingia kifua cha ushindi.
Lakini hayo yote yatawezekana kama tutakuwa watu wa kusali, kumshukuru
Mungu, kama Yeramiha alivyomsifu Mungu baada ya ushindi; Yer.20.13 mwimbieni
Bwana msifuni Bwana kwa maana ameiponya
roho ya mhitaji katika mikono ya watu watendao maovu.
Tukumbuke kuwa tunapomsifu Mungu tunadhihirisha kuwa yeye ni
kiongozi na anaweza kufanya chochote
anachotaka kufanya, lakini tukumbuke
kuwa mungu hutenda kila kitu kwa haki na upendo mkuu sana.
Tunapomsifu mungu
tukumbuke kuwa tunatekeleza mambo Haya makuu;
Kwanza tunamtambua kuwa
yeye ni kiongozi wetu na hakuna mtu wa kutuvunja moyo kwani ametuita kufanya
jambo njema ndani yetu na kwa jamii inayotuzunguka; hivyo kama yesu alivyo
waambia makutano wasipomshangilia hata mawe anaweza akayafanya yamshangilie;
Pili tunatambua kuwa
yeye ndiye mwenye mipango yote tukisoma Yer; 29:11 maana nayajua mawazo
ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni
mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
Tatizo ambalo linatusumbua tunatamani kuona kuwa tunaweza kufanikiwa bila nguvu
ya Mungu. Lakini mungu anatupa nafasi ya kuchagua kkuhusu au kushindana na
mwito wa Mungu au kukubali mwito wa Mungu na kamwe hata vunjika moyo.
Tatu tutambue kuwa
tunamsifu Mungu sio kwa kufikiria nini anatufanyia au nini kitatokea mbele ya maisha yetu bali
tunatakiwa tumsifu Mungu kwa vile alivyo kwani yeye ni mwanzo na mwisho. Kama zaburi
ya 22:3 inavyosema na wewe ni mtakatifu uketiye juu ya Israeli. Tukumbuke kuwa
sala zinafungua milango ya matumaini zaidi ya kweli ndani ya maisha yetu. Kwa hiyo
nguvu ya Mungu iko karibu yetu tukiwa tunamwabudu. tujifunze kuwa kama watoto wadogo wao wanafuraha daima na hata wanapovunjwa moyo husamehe na kusimama tena imara katika kucheza.
Hii ni tafakari yetu ya
leo Mwenyezi Mungu apewe sifa ya utukufu uliotukuka Amina
No comments:
Post a Comment