January 14
Tafakari ya leo inahusu nguvu na
uwezo ambao Mwenyezi Mungu ametujalia sisi kama tunavyosoma kutoka kitabu cha
mwenjili Luka 10:19 “Tazama, nimewapa Amri ya kukanyaga Nyoka na Nge, na nguvu
zote za yule Adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru ” Somo hili linatumbusha
kuwa sisi wanadamu tumepewa uwezo wa kumshinda Shetani
na Nguvu; kupitia hii Mamlaka tuliyopewa na mungu kupitia Bwana wetu Yesu
Kristo, tuna uwezo wa kuzikanyaga na kuzisambaratisha Nguvu za Yule Adui
Shetani.
Leo tunapotafakari
tukumbuke kuwa ni ukweli usiopingika kwamba tumepewa uwezo wa kuharibu nguvu za
aina yoyote za adui. Lakini ni ukweli usiojificha tulio wengi tumekosa imani
thabiti ya kutumia nguvu hii kubwa hivyo ni wakristo wachache sana
wanaojitambua kwamba wana uwezo huu ndani yao na kuweza kutumia nguvu hizo;
Mara nyingi Yesu aliona udhaifu huu hata kwa wafuasi na Mitume wake ndipo
tukisoma Yohana 14:12 alituasa hivi; Amin,
amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye
atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Leo tujipime
na kujitambua kuwa kila mtu ana nguvu na uwezo wa kuziharibu nguvu za giza. Lakini
lazima tukubali kuwa mwanadamu yeyote
asiye jitambua hawezi kufaulu katika jambo lolote. Usipojitambua kwamba waweza
kufanya kitu Fulani, basi huwezi kusonga mbele, maana tayari umeshaona huwezi.
Mtu yeyote aliyefanikiwa kimwili na kiroho huanza kwanza kujitambua ndani yake.
Na utambuzi anakuja na Imani ambayo
inakujengea uwezo mkubwa wa kutekeleza jukumu lolote lile ambalo liko mbele
yako;
Tafakari
ya leo inatakiwa itukaribishe karibu kabisa na utekelezaji wa jukumu hili ambalo
linaanzia kwenye maombi na kumshukuru Mungu. Ni kazi ambayo inakuwa na vikwazo
vingi lakini inahitaji Nguvu imara ya Imani ili mkono wa Mungu uwe juu yako/yangu katika
kuifanya kazi hii ilojaa vikwazo kila mahala adui anapoona anakanyagwa naye hujitutumua kukushinda hivyo
shetani ndivyo alivyo;
Hii ni
tafakari kubwa kuwa nguvu ya ushindi i katika kukiri na kuamini kwetu, tumepewa
mamlaka ya kumiliki kila tunapokanyaga iwe ofisini, shuleni kwenye biashara
zetu sehemu yoyote ile tumepewa mamlaka ya kutawala kila kitu na kila mahali
kama Mungu alivyomwabia Adamu. Luka 10.19-20 anasema tazama nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na
nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachonidhuru.
Tukumbuke Jinsi wale wafuasi wa yesu
walivyorudi kwa furaha baada ya kupewa mamlaka ya kutenda kazi: Wafuasi wale sabini walipewa na Yesu amri ya
kukanyaga nyoka na nge na wasiwadhuru na kisha pepo wakawatii, hii inawezekana
tu kwa mamlaka kutoka kwa mfufuka, Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha,
wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, ..…Tazama,
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala
hakuna kitu kitakachowadhuru
Hii ni
tafakari yetu ya leo tutumie mamlaka ambayo Yesu ametupatia kwa siafa na
utukufu wake na kwa ili nasi turudi na ushuhuda wa furaha kama wafuasi wa Yesu-
Amina
No comments:
Post a Comment