January 22
Tafakari ya leo
inatukumbusha wazo nzima la kuombeana:
tukumbuke kuwa kwa kuwaombea wengine tunaonyesha upendo mkubwa miongoni mwetu. Tukisoma
Yohana 1:34 anasema amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi,
ninyi mpendane vivyo hivyo. Tukumbuke kitabu cha Torati inasisitiza kuwa umpende
jirani yako.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tunatakiwa kutafuta na kufuata mambo ya amani na mambo
yafaayo kwa kujengana na sio kutengana. Tunatakiwa kuendelea kufarajiane na
kujengana kila mtu na mwenzake na njia pekee ya kujengana ni kwa kuombeana:
Tusihukumiana tukihukuminana
hatutakiani Baraka.Kitabu cha waefeso 4:32 kinatukumbusha kuwa, tena iwe
wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika
Kristo alivyowasamehe ninyi.
Tukumbuke kuwa tunaposali tunasali
katika namna tatu aina ya kwanza ni ile
ya ya kuelekeza juu kwa Mungu sala
ambazo tunaelekeza zaidi kwa Mungu wetu kwa kumwabudu, kumsifu, kumshukuru na
kuomba msamaha.
Aina ya pili ni sala ya
ndani yetu ambazo zinatuhusu sana sisi wenyewe tukikazia zaidi kuomba msamaha,
kuomba nguvu na ulinzi wa mungu na mwongozo wa maisha bora kulingana na
maelekezo ya Mungu.
Na Aina ya mwisho ni kwa
ajili ya wengine zinalenga nje sala
ambazo zinalenga zaidi wengine mahitaji ya wenzetu jirani zetu, ndugu zetu
tunapowaombea kuhusu shida zao na mahitaji yao.
Tukisoma bibilia
inatukumbusha kuwa kuwaombea wenzetu ni wajibu wetu kama wakristo; kwani kwa
kufanya hivyo tunapata faida nyingi na kama kuwaimarisha kiimani, kwani nikijua
wewe unaniombea inanipa mimi ushindi na uimara.
Pili tunapoombeana
inatujengea ukaribu undugu wa kiroho na
hivyo kila mmoja wetu anabarikiwa. Na hata inaweza kutusaidia kuondoa tofauti
zetu tukijua kuwa sisi sote ni ndugu mmoja kwani tunajua maombi ya mwenye haki
yanaleta matokeo tukumbuke Jinsi Eliya alivyoomba kuhusu Mvua na mafanikio
ambayo yalikuja kulingana na maombi yake.
Kwa hivi sisi tunatakiwa
kufurahi pamoja na wafurahio na kulia pamoja na nao waliao; na htutakiwi
mumlipa mtu ovu kwa uovu tuangalie yaliyo mema machoni pa watu wote. Tuache
kuangalia bali tuushinde ubaya kwa wema. Zaidi ya yote tuwe na juhudi katika
kupendana kwa sababu upendano husitiri
wingi wa dhambi. Tafakari ya leo tunatakiwa kutumia karama zetu katika
kuhudumiana kama mawakili wema wa Yesu katika kufurahia na kushukuru neema
mbalimbali za Mungu. Amina
No comments:
Post a Comment