January 21
Tafakari ya leo
tuangalie ni kitu gani sisi huwa tunakipenda zaidi katika maisha yetu: Je
tunaupenda ulimwengu kwa vile tunaufahamu au tunapenda Mbingu kwa vile
tumehaidiwa mazuri mengi? Leo tuangalie kitabu cha 1 Yakobo 2; 15 -17; Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba
hakumo ndani yake.
Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na
Baba bali hutokana na ulimwengu.
Nao ulimwengu unapita, pamoja
na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi
ya Mungu adumu milele;
Starehe za Walimwengu
Kwa walimwengu mtazamo ni kuwa yafurahie maisha katika hali
yeyote ile hata kama maisha yanakufanya ulie kwa ugumu wake lakini wewe
uonyeshe ulimwengu kuwa unasababu elfu moja za kifurahia kwa staili yeyote kama
picha hii hapa juu inavyoonyesha; starehe kwanza halafu mengine baadae; Mungu
tutamkimbilia “ BAADAE” baada ya starehe, bado tuna muda wa kutosha;
Tutafakari yetu tukiulizwa
na Muumba wetu je unapendelea kupita daraja gani kumfikia yeye?
1. Daraja la uzima
ambalo linakwenda moja kwa moja kwake na kwa Muda mfupi kama Waraka wa Yakobo
unavyotufundisha;
2. Daraja la anasa na
malimwengu linavyojieleza ambalo huna uhakika wa kumfikia yeye kwa wakati
muuafaka kabla milango ya mbinguni haijefungwa;
La msingi huu ni
wakati mzuri wa kufanya tafakari kuhusu hatima ya maisha yetu - Amen-
No comments:
Post a Comment