January 15
Tafakari ya leo hebu
tuangalie ulinzi wa mungu juu ya maisha yetu; Daud katika zaburi ya 23 anasema
hivi:
1 Bwana ndiye
mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha
nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam,
nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe
upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza
mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na
kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema
na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa
Bwana milele
Nimeipenda sana zaburi hii
ukiisoma na kama unaielewa ni mwongozo pekee wa maisha ya kila siku. Na somo jingine
ambalo tunafundishwa katika zaburi hii kuwa Mkristo sio hasa inahusu madhebebu
yetu bali ni zaidi inahusu uhusuiano wako na Yesu ukoje;
Tukumbuke Yesu Mwenyewe
alijiita yeye ni Mchungaji Mwema tukisoma injili ya Yohana 10:11. Maana yake ni
nini? Kuwa yesu kwa kuwa mchungaji Mwema hapungukiwi na kitu chochote
unachohitaji katika malisho bora, Majani mazuri yeye hutoa; ulinzi wa mifugo
yeye husimamia kwa msingi huu kuwa Mungu yeye ni kila kitu tunachohitaji na
hivyo Mungu alimtuma Mwanae aje kutukomboa kutoka katika utumwa wa dhami hivyo kwa
msingi huu tukiwa na Yesu hatupungukiwi na kitu.
Ukiwa mfugaji na ukiwa
kwenye machungio na wakati wa jioni ukifika na mifugo yako iko tayari kupumzika
kuna mambo manne ambayo yatafanya mifugo yako iweze kulala salama:
Kondoo hawatakuwa tayari
kulala kama wanahofu ya usalama wao yaani wamenusa hatari ya adui: Kondoo
hawatakuwa tayari kulala kama kuna kuto elewana miongoni mwao ( friction);
kondoo hawatakuwa tayari kulala kama kuna wadudu kama (mbung’o) katika eneo ambalo wanatakiwa
walale. Na mwisho kondoo hawatakuwa tayari kulala kama hawajeshiba na bado wanataka
kuendelea kutafuta chakula.
Tafakari hii inatufundisha kuwa lazima kuwe na uhuru ambao hujitenga na woga
wa usalama, ugomvi miongoni mwao, wadudu na njaa kabla kondoo kuweza kulala. Je
tunaitafasiri hali hii vipi katika maisha yetu ya kila siku. Jibu la msingi
kama Daudi alivyolezea katika zaburi hii
ya 23 kuwa Mungu anaondoa vikwazo katika maisha yetu, kwa dhumuni la kutupa
sisi ufadhali wa maisha yetu.
Tukiendelea kutafakari siku ya leo tukumbuke kuwa Baraka ambayo yesu anatueleza
sio kuwa tutaishi bila shida au majaribu; katikati ya majaribu ndipo tunapopata
furaha ya kweli ya kimungu na tunaendlea kujaliwa Baraka mara dufu. Tunatakiwa kumuamini
Mungu, kuwa anajali; anasikiliza; na ananipenda na atanilinda na nguvu zote za
shetani; sisi kama kondoo sio viumbe wenye akili kumzidi Mungu, sisi kama
viumbe hatuna nguvu ya kujilinda kama sio kwa nguvu ya Mungu; sisi ni viumbe
ambao tunamtegemea Mungu; lakini kama walivyo kondoo lazima tuishi kwa Imani ya
kumtegemea Muchungaji wetu Bora ambaye ni Yesu Kristo.
Tatizo letu leo hii sisi tulio wengi tunaishi maisha yetu katika
uliwengu wa kulalamika na kukata tama; tukumbuke kuwa Mungu ndio nguvu yetu nay
eye peke yake ataimarisha nguvu zetu. Hii ni tafakari yetu ya leo ; Amina
No comments:
Post a Comment