NINAYO FURAHA YA KWELI LEO
January 25
Leo Tafakari yetu inaangalia mafundisho ya Biblia kuwa Walio na
furaha ya kweli , ni hao walio masikini rohoni , yaani tegemeo lao
haliko katika mambo ya kidunia ila wanamtegemea Mungu kwa kila
kitu. Walio na huzuni au wanateseka kwa sababu yake Mungu, nao
watafarijiwa .
Bibilia inatufundisha kuwa ili kuitwa wana wa Mungu yatupasa
kuleta amani na upatanisho miongoni
mwa watu na kati ya watu
wa miongoni mwetu.
Biblia inatoa mfano wa kuwa Chumvi huwa nzuri iwapo tu na ladha,
ikipoteza ladha yake, basi haifai kitu ila kutupwa. Rafiki, wewe ni
chumvi na ili kuhifadhi ladha, unastahili kudumisha amani wakati
wote.
Je daima tunamshukuru Mungu kwa neema ya
ya uzima ambayo tumejaliwa kwa wiki hii nzima iliyokwisha?
Je tunamshukuru Mungu kwa neema ya uzuri
tunaoringia miongoni mwetu?
Wakati unafanya tafakari ya jumapili ya leo wewe uko kwenye kundi gani, kati ya makundi haya matatu hapo chini?
· Watu wema wataendelea kudumu katika
uaminifu na uokovu wa maisha yao .
· Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa
waliyofanya na wanapojirekebisha huwa thabiti katika msimamo wao, watu
walio katika kundi hili Mungu atazidi kuwabariki.
· Watu
wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii ilivyo, ikiwa jamii iko katika
tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo, na ikiwa jamii
haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile hufuatanamna ya utamaduni wao
ulivyo. Mungu hutukumbusha kuwa daiama tunatakiwa kuwa na msimamo na imani
katika maisha na matendo yetu na sio kuishi bila msimamo kama mawimbi ya bahari
ambayo yanasukumwa na upepo kwa mwelekeo wowote ule. Hii ndio tafakari yetu ya leo
No comments:
Post a Comment