JANUARY 1
Leo tunapoanza mwaka mpya 2016 tuna
kila sababu ya kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa upendo wake kwetu na
kwa familia zetu. Tuendelea kujiuliza tumpe Mwenyezi
Mungu kwa upendeleo huu mkuu wa kuweza kuiona siku hii mpya katika
mwaka huu mpya? Je mimi/wewe tunaupekee gani tofauti na wale wote ambao
wameitwa katika pumziko la milele? Kwa baraka na neema hii kubwa sisi sasa tunatakiwa tumrudishie nini mungu wetu? Je mwaka huu mpya kwetu una maana
gani?
Je nini tunatakiwa kutafakari katika
mwaka huu 2016?
Niliyoyafanya mwaka 2015 yote
yalimpendeza Mungu au yalikuwa yananipendeza mimi mwenyewe?
Mwaka huu mpya tuiwekee nadhiri ya
kuyaacha yote ambayo yalikuwa hayampendezi Mungu na kutuletea
utengano naye; tukisoma kitabu cha waefeso sura ya 5:14-18 mtume
Paulo anatukumbusha kuwa kwa matemdo yetu mabaya anatuasa tuamke na
kubadilisha tabia kwani hakuna mtu mwingine yeyote atakaye ibadilisha
tabia yangu/yako isipokuwa mimi/wewe mwenyewe. Njia pekee ni kumkaribisha kristo
Yesu ambaye ni mwanga katika mabadiliko ya maisha yetu.
Mwaka wa 2016 uwe ni mwaka wa matendo yanaendana na kutumia muda wetu vizuri kwa utukufu wa mungu,
kutisoma kitabu cha waefeso sura ya 6 Mwenyezi Mungu ametupa uwezo wa
kutumia kila kitu, kwa kupambanua uthamani wake mbele ya mungu na
utukufu wake. Inatakiwa tukumbuke kuwa yesu ni sadaka yetu pekee
kupitia damu yake takatifu iliyomwagika msalabani kwa ajili ya
msamaha wa dhambi zetu, na hatuhitaji hata kidogo msamaha mwingine wa
dhami zetu, kama kitabu cha John 3:16 kinavyotukumbusha, sisi
tunachotakiwa kuwa hekalu la Mungu ambaye ataishi ndani yetu. Sasa
kama ukimkarisha mungu ndani yako unahitaji nini tena?
Zaburi ya 46:10 inatuonya kuwa
sisi binadamu daima tunafanya vitu kwa uwezo wetu baada ya kutegemea
nguvu za Mungu, na tunajivuna sana kama tukiona kuwa tumefanikiwa na
kudharau nguvu ya Mungu. Lakini tunajisahau kuwa maisha yetu sio
chochote na hatuwezi kuyamuda hata kidogo. Tukumbuke kuwa katika
mazingira yeyoye yale, mungu peke yake ndiye anayeongoza na kutawala
maisha yetu.
Katika mahangaiko, hofu, mashaka na
mafanikio ya maisha yote naamini kuwa mungu peke yake ndio daraa
pekee la mafanikio yangu/yako na familia yangu/yako. Mimi binafsi naamini kuwa kwa namana yeyote ile
mafanikio yangu ni baraka pekee kutoka kwa Mungu juu yangu.
Ninatembea katika ushindi mwaka huu wa bwana kwa sababu kubwa moja
kuwa mimi daima natembea na bwana. Kama mwenjili Luka 1.28 anavyosema
kuwa Mungu yu pamoja nami; kinachohitajika ni uwezo wa kusikia sauti
ya kimungu ndani yetu hiyo ndio msingi wetu wa mafanikio na imani
yetu ya ushindi wa mafanikio yetu.
Mwenjili matayo katika sura ya 7:8
anatukumbusha kuwa kwa yeyote ambaye anaomba hupokea, na yule
atafutaye huona na yuke abishae hufunguliwa. Kwa hiyo tunatakiwa
kuwa na imani na uthabiti na unyenyekevu ili tuweze kuuridhi utukufu
na neema ya kimungu juu ya maisha yetu. Hatutakiwi kukata tamaa hata
kidogo. Isipokuwa tunatakiwa tuendelee kumshukuru Mungu kwa uaminifu
wake kwetu kwa kuendelea kusali kila siku na kila wakati bila
kuchoka. Hatutakiwi kukata tamaa kwa kuchelewa kupata matokeo ya
maombi yetu. Daima mwenyezi Mungu anafanya kazi katika utukufu wa
maficho yake kwa faida yetu sisi. Na tusifahau kuwa majira ya mungu
kwetu ni ya uhakika sana sana lakini kama tunaenenda katika imani.
Nakutakia safari njema ya Tafakari katika mwaka huu 2016 tembea nami kila siku katika kusifu na kumshukuru mungu kwa mema ambayo ameendelea kutenda juu yetu .Amina
No comments:
Post a Comment