January 8
Tafakari ya leo
tunaangalia huluka ya binadamu; binadamu tunapenda kupokea zaidi kuliko kutoa.
Na pale tunapokuwa tayari kutoa tunajitahidi kutoa kile cha ziada ambacho
hatukihitaji kwa wakati husika. Tunajua kuwa utoaji ni kielelzo cha juu kabisa
cha neema ya kimungu ndani ya maisha yetu.
Bibilia inatufundisha kuwa
kutoka mwanzo kuwa Mungu ndio mmiliki wa kila kitu na maisha yetu yote na vyote
ambavyo tunavyo. Sisi ni watumishi tu, hivyo kama yeye alivyomtoaji nasi
tunapaswa kufanya hivyo.
Je sisi ni watumishi ambao
tunafurahia kupokea tu na sio kutoa?
Je mtumishi bora ni yupi
Yule ambaye hutoa kwa moyo wake wote kwa wahitaji au Yule ambaye anatamani tu
kupokea?
Kutoa ni moyo wa ushujaa
sana kwani ni tendo njema la kuwasaidia wahitaji ambao hawana kimbilio na
kimbilio liko kwako kwani Mungu alivyotumba sisi alituumba kwa mfano wake;
hivyo nasi tunatakiwa tuwe kama Baba yetu ambaye anatuagiza leo tuwe watu wa
kutoa sio wa kupokea zaidi.
Katika Jamii yetu tunao
watu ambao ni wahitaji msaada katika Afya zao, katika Elimu zao, na kadhalika
na tunapo fikiria mtu ambaye anaweza kusaidia katika hili hapa ndipo wazo la
kutoa linapotimia. Mtoaji huleta furaha ndani ya jamii kwani humsaidia yule
ambaye ni mwitaji; ukiwa mtoaji ni ukweli kuwa unamweka mwenye shida mbele na
unakuwa tayari umefanya kazi ya Utumishi wa Mungu wa kuleta furaha ndani ya
jamii ya wenye shida. Ni vyema kama tutaweza kujijengea tabia ya kutoa zaidi
kuliko kupokea, Badala ya kuthamani kujiwekea utajiri.
Katika tafakari ya leo Bibilia kupitia kitabu
cha 2 Wakorintho 9:6-7; inatumbusha kuwa apandaye haba atavuna haba; apanda ye
kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivokusudia moyoni
mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa
moyo wa ukunjufu. Pia tumetiwa moyo tuwe watunzaji wema wa kile ambacho Mungu
ametupa.
Lakini pamoja umuhimu wa
kutoa lakini lazima tuzingatie maelekezo ya Yesu kupitia Luka 16:11 Basi kama
ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa iliyo yenu
wenyewe. Pia tumewajibika kuwatafutia risiki wale wa nyumba yetu ndio dhana ya
utoaji inapoanzia;
Kitabu cha 1 Timotheo 5:8
atukumbusha: “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa
nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.ni
kweli kuwa; ni mapenzi ya Mungu tupate vitu vyote vitakavyotufanya tufurahie maisha yetu duniani. kimaisha,
tunapata thawabu kubwa kwa Mungu. Kumsaidia mhitaji kitu, ni kujikopesha mbele
ya Mungu . tukumbuke kuwa Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho ndicho mtakachopimiwa. Kwani Mungu wako atakubariki kama
alivyokuahidi.
Kama akiwapo mtu maskini
pamoja nawe usifanye moyo wako kuwa
mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini”. Mathayo 25:35, 40, 34 Kwa
maana nalikuwa na njaa mkanipa chakula, nalikuwa na kiu mkaninywesha, nalikuwa
mgeni mkanikaribisha, nalikuwa uchi mkanivika, nalikuwa mgonjwa mkaja
kunitazama, nalikuwa kifungoni mkanijia. Yesu akawaambia; Amini nawaambia,
kadri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu wahitaji, mlinitendea mimi.
Hivyo, njooni mliobarikiwa
na baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu. Mdo
20:35 tunapohitimisha tafakari yetu ya leo tukumbuke kuwa ni kheri kutoa kuliko
kupokea. Kwa maana Mungu atakupa kwa wingi Baraka katika maisha yako na uzao
wako hapa duniani na atakupa uzima wa milele mbinguni kama tutaendelea kutimiza
wajibu wetu wa kutoa zaidi kuliko kupokea.
Amen
No comments:
Post a Comment