January 13
Tafakari ya neno tunaipata kutoka kitabu cha Mwanjili Matayo 8: 5-10. Yesu alipoingia Kapernaumu,
askari mmoja alikuja kumwomba msaada, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza, tena ana maumivu makali. Yesu
akamwambia, Nitakuja kumponya. Lakini yule
askari akamwambia, Bwana, mimi sistahili wewe uingie nyumbani kwangu; lakini
sema neno tu, na mtumi shi wangu atapona. Yesu
aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, Nawaambia
kweli, hata katika Israeli sijaona imani ya namna hii.
Tafakari ya leo inatuonyesha kuwa tunatakiwa
tuwe na imani dhabiti, na kwa kuwa na Imani imara basi kwa neno tu kila kitu
tukiombacho hutimia; kama yesu alipomjibu Yule Askari “Nenda nyumbani, na yale
uliyoamini yatimie kwako. Na yule mtumishi akapona tangu wakati ule ule”.Hapa mwinjili Matayo anatuonyesha zaidi
kuhusu nguvu ya imani:
Binadamu tunaamini zaidi katika nguvu mwili, kuguswa kama unaumwa
ndipo upone; tunaona hata wachungaji wengi hutumia njia hii. Lakini Hapa Yesu
kupitia kwa askari alionyesha kuwa Imani dhabiti huzaa tunda lililo njema
ambalo ni neno.
Kuna maswali mengi ya kujiuliza kulikoni asiingie kwenye Nyumba hiyo
na akamguse ili kumponya mtumishi mgonjwa? Inaonekana kuwa askari alikuwa
amesikia kuhusu nguvu, uwezo na mamlaka ya Kimungu na uponyaji ambayo anayo Yesu alikuwa
navyo. Lakini aliamini kuwa Yesu kwa nguvu ambayo alikuwa nayo haikuwa lazima
kwake kwenda kumwekea mkono ili apone bali kwa NENO lake tu lilikuwa linatosha
kumponya mtumishi wake mgonjwa. Hii ni imani ya Ajabu na kubwa sana.
Katika tafakari ya leo lazima tukubali kuwa katika maisha yetu ya Kila
siku lazima tukuze na kuimarisha imani yetu ili tuweze kufanikiwa katika maombi
yetu. Hata kama tunasali vipi, tunaomba vipi lakini bila Imani ya kweli
hatuwezi kufanikiwa na tutaendlea kulalamika na kusikitika kuwa Mungu asikilizi
kilio na shida zetu;tukumbuke kuwa katika maisha yetu ya Kiroho Imani huza NENO
lenye nguvu ya kukamilishi mahitaji yetu.
Tafakri yetu leo inalenga kuwa hata Yesu alikuwa hajeona mtu mwenye
imani kubwa namna hii na unyenyekevu mkubwa; kwa sababu walio wengi kwanza
walikuwa hawaamini kuwa kweli anaponya kwa nguvu ya kimungu.
Imani ni kila kitu katika maisha yetu, na mwenyezi mungu anapendezwa
na mtu mwenye imani imara, tunapomwamini Mungu na kuamini kuwa yeye ni kila
kitu katika maisha yetu nasi hubarikiwa; imani ambayo askari huyu alionyesha
ilikuwa zawadi kubwa sana mbele ya mungu naye alipokea zawadi kubwa sana. Mungu
ni Imani na Mungu Ni Neno.
Imani ya Asakari huyu ilikuwa kama imani ya baba yetu Abraham ambaye
aliamini kwa neno na bila kuwa na mashaka alitimiza maagizo ya Mungu. Aliamini katika
ahadi za Mungu bila kuzitilia mashaka; na kwa kuamini Abraham alipata zawadi
kubwa sana ya kuwa baba wa Imani.
Je wewe na mimi leo imani yetu iko wapi? Tunaamini katika nguvu na
uwezo wa Neno la uzima ambalo ndilo mwanga katika maisha yetu ya kila siku na
mafanikio yetu hapa duniani na hatimaye mbinguni? Ni wakati mzuri wa kutafakari
wazo hili;
Amina
No comments:
Post a Comment