Kitabu cha Maombolezo 3;
40 kinatukumbusha kuwa na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, na kumrudia bwana
tena, Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa
Mungu.Warumi :23 Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye,
lakini mwanadamu alikwenda Kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu
badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya Zambi; hi maana yeke ni nini, mtu
anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi. Hapa
ndipo tunapoona umuhimu wa kuanza kusafisha nyoyo zetu
Lazima tujisafishe tukijua
kuwa Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa
mkubwa ambao unaotutenganisha na ufa huu ni dhambi. Mwenyezi Mungu anatutaka
sisi leo tujisafishe ili tuweze kuondoa huu Ufa
na hatimaye kumfikia Mungu na kuishi naye tena katika bustani ya Adeni.
Tukumbuke kuwa mwanzo Mungu alipomuumba Adamu na baadae Hawa waliishi naye bila kuwa na Ufa wowote ule;
Lakini walipotenda dhambi ndipi Mungu alipojenga Ufa na Kuwafukuza kutoka Adeni
kwani walikuwa ni wadhambi;
Tunatakiwa
Kujisafisha kwa matendo mema na sala na kumkaribisha Mwokozi wetu Yesu Kristo
Mioyoni mwetu kwani yeye ni Mpatanishi wetu kama anavyosema ; Tazama, nasimama
mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia
kwake. Yesu anaishi ndani ya nafsi
ambayo inachukia dhambi tumeonywa kuwa dhambi isitawale ndani ya miili yenu. Sisi
kama wafuasi wa Kristo ambao tuko tayari kusafisha nyoyo zetu tukumbuke
kuwa tunaishi chini ya neema ya uokovu
wa mungu tukikubali kubadilika.
Luka 7.21 inatukumbusha
kuwa “ Si kila mtu aniambiaye, Bwana,
Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya
Baba yangu aliye mbinguni”. Mapenzi ya Baba ni kukubali kubadilika ili nasi tuhesabiwa
haki. Yatupasa kutenda yale yatupasayo
kutenda; ili tuendelee kumwita Yesu
Bwana na hatutendialiyofundisha? Kila
mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda. Tunatakiwa tusafishe nyoyo zetu tukizingatia kuwa upendo wa mungu
ni tofauti kabisa na upendo wetu kwa binadamu mwingine; tukumbuke kuwa baba
mzuri anapenda mazuri zaidi kwa watoto wake anajitoa sadaka kwa ajili ya yao na
anawapatia mahitaji yao wanayoyahitaji kwa wakati na pale wanapokosea kwa faida yao anawaadibisha na kuwasamehe.
Tunatambua kuwa wakati
mwingine watoto wetu wanakataa ushauri wa baba ambao ni mzuri na kukimbilia
ushauri wa kuaacha kilicho bora na muhimu; hapa tunaona kiburi na ubinafsi
ukiwa unatawala zaidi. Wanaingia atika maisha ya anasa na mwisho wa siku
wanaishia pabaya. Tujifunze kutoka hadithi ya mtoto mpotevu. Tunashauriwa
kujisafisha kwa kuzingatia kuwa mwenyezi Mungu ametupa uhuru wa kuchagua nakutenda
tutakavyo, yeye alichotusaidia ametuwekea sheria tuzifuate ili tuweze kuwa
miongoni mwa wateule wake; amaetujalia ufahamu na uwezo wa kuamua kati ya mabaya
na mazuri. Mungu aliumba ulimwengu na sheria zinazo ongoza kila kitu ili
tuzitii; tukumuke kuwa sheria ya maadili ya Mungu ni muhimu kwa sababu
inatokanamisingi ya Kimungu.
Hivyo zambi zetu kutoka zile
za mababu zetu zimevunja uhusiano wetu
na Mungu. Tusafishe uasi wetu ambao umetengeneza ukuta wa utengano kati ya
Mungu na sisi. Ni kweli kuwa tumekuwa bize katika maisha yetu ya kila siku ya
kidunia na tumekosa muda hata kidogo tu wa kumshukuru Mungu.
Tafakari ya leo bado
hatujechelewa tunanafasi kubwa tu ya kusafisha nyoyo zetu ni kutambua kwamba Neema
ya Mungu bado iko juu yetu ya kuendelea kumshukuru Yesu kuwa ni bwana na mwokozi
wa maisha yetu na alikufa msalabani ili aweze kuondoa ukuta wa utengano ambao
uko kati yetu na Mwenyezi Mungu kwa Dhambi zetu. Tunatakiwa kubadilisha fikra zetu kuwa tukisafisha Nyoyo zetu tutapata haki za kuwa watoto wa Mungu. Hii ndio tafakari yetu
ya leo.
Amen
No comments:
Post a Comment