January 18
Tafakari
ya leo tuangalie jinsi bibilia ilivyohubiri amani; swali la msingi ambalo mimi
najiuliza nani anatawala dunia yetu leo? Jibu ni rahisi tu amani ya bwana ndio
inayotawala dunia yetu hii kwa wale ambao wanaamini; yesu aliwaambia mitume
wake amani yangu nawaachia, sio tu amani bali ni amani yake YESU; kama utaweza
kupokea amani ya bwana utaweza kuishi maisha mazuri sana yenye utulivu wa
kihoro na kimwili; na hiyo amani itakuwwezesha wewe kuishi kwa nguvu ya
Kimungu.
Amani iletwayo na Yesu ni ajabu kwani imejaa neema
na matumaini; kwani mwenye Matumaini huongozwa na Mungu ambaye analindwa na
hila za adui; nakumbuka nilipokuwa mdogo giza lilipokuwa likiingia na
nilipokuwa natumwa kwenda kuchukua kuti chochote nilikuwa naogopa nilikuwa sina
amani na daima niliomba ulinzi wa kunisindikizwa. Na nilipoulizwa nilijibu kuwa
giza ni nene hivyo nahitaji mssada. Hivyo nilikuwa sina amani wala matumaini;
Lakini Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tukiwa na amani ya Bwana hatutaogopa
chochote kwani tayari tupo ndani ya ulinzi wa Mungu.
Tukisoma warumi 14.19 paulo basi kama ni hivyo na mfuate mambo
ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. Ni jukumu letu kuitafuta amani na
kuitetea kwa faida ya wote, lakini inakuwa ni rahisi kama amani yako itakuwa ni
za la kristo Yesu;
Zaburi ya 119:165, 167 inasema wana wa amani nyingi waipenda sheria
yako, wala hawana la kuwakwaza; ndipo tutakaposifu na kusema nafasi yangu
imezishikashuhuda zako name nazipenda mno. Hivyo yatupasa kukumbuka kuwa mungu
yu daima juu yetu na uwepo wake ndio chanzo cha amani yetu. Tunatimiza uwepo wa
Mungu pale tunapo yaelekeza mawazo yetu mazuri juu yake na amri zake katika
utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku. Lakini tuka kuumbwa kwa dunia Mungu
ametupa uhuru wa kuchagua kumtegemea yeye katika yetu au kuendelea kuhangaika
na matatizo yetu. Tukumbuke kuwa nani ameshikilia suluhu la matatizo yetu?
Hata pale ambapo matatizo ambayo yako mbele yetu hayaeleweki bado
tunatakiwa tumtumaini Mungu ambaye yey ndio asili ya amani ya fikra zetu;
tukumbuke kitabu cha Methali 3:5 -6 mtumaini bwana kwa moyo wako wote wala
usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye naye
atayanyosha mapito yako. Ndio katika maisha yetu ya kila siku mambo mengi yako
nje ya uwezo wetu na ndio asili ya kuvunjika kwa amani. La msingi tusijaribu
kuhangaika kupata suluhu ya mambo pasipo Mungu. Tukumbuke kuwa bila uwepo na
nguvu yake mungu tunapoteza nguvu nyingi katika kutafuta amani ya kweli ndani
ya maisha yetu. Tumesahau kuwa tunatakiwa tukae kwa furaha tukijua kuwa Mungu
tayari anatembea nasi siku zote kama tukizikaribisha sheria zake na
kuzitekeleza kwa maelekezo yake.
Mtume Paulo kwa Wafilipi 4:6-7 msijisumbue ka neon lolote; bali katika
kila neon kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na
Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia
zenu katika Kristo yesu.
Je ni kitu gani tunatamani kumwuliza Mungu sasa hivi? Je unatamani
yeye aje ndani ya maisha yako ili uweze kufurahia amani yake: ili ikusaidie wewe
uweze kufurahia amani iel ya milele yote?
Nini
kinaharibu amani yetu leo? Ni dhana ya kujisikia mkosaji na kama hii ndio kweli
umemkosea nani? Amani ya kweli inaletwa na upendo wa kweli miongoni mwetu; Tumefundishwa
kuwa tuwapende wenzetu kama tunavyojipenda kwani kipimo kile kile ambacho
tunamtendea mmoja wetu ndicho kitakuwa kipimo chetu. Tutafakari Pamoja siku hii
ya leo kuwa je wewe ni kwa namna gani unahubiri amani?
No comments:
Post a Comment