Hili lilikuwa ombi la wafuasi wa yesu, pamoja kuwa na yesu siku
zote wafuasi wa Yesu walijifunza na walimwona yesu akitumia muda mwingi akiwa
akiongea na Mwenyezi Mungu kwa sala. Na alikuwa akitumia muda huo akiwa katika
faraga na sehemu ya utulivu; hali hii ilikuwa ni ngeni kwa wanafunzi ndipo nao
walitamani kufanana na Yesu hivyo waliomba nao wafundishwe jinsi ya kusali.
Tunafahamu kuwa sala ni njia pekee ambayo inafungua njia ya
mawasiliano na Mungu. Sala ni njia pekee ambayo inatuunganisha na mungu. Sala
ni njia pekee ambayo inaonyesha ukuu wa mungu katika maisha yetu; sala ni nia
pekee ambayo inaonyesha shukrani yetu, unyenyekevu wetu, na kuomba msamaha kwa
mungu;
lakini tukumbuke kuwa maombi pia yanaunganisha mioyo yetu na
akili zetu ambazo zinaleta utulivu kwani mwili wako ndio hakelu la bwana, hili
ni kanisa ndani yako; tukisoma kitabu cha James 4: sala hutupatanisha na Mungu;
sala huleta upatanishi miongoni mwetu, huwezi kuwa mpatanishi kama hujui jinsi
ya kuomba; upatanishi msingi wake mkubwa ni unyenyekevu na unyenyekevu hutoka
na uwezo wetu wa kuongea na Mungu; ndio maana wapatanishi wanaitwa wana wa
Mungu; tukisoma Matayo 5:9 anafafanua zaidi.
yesu alipokuwa akihubiri kuhusu
upatanishi alikuwa akiliongelea hili katika maana pana sana. Hakuwa anaongelea
tu kuwa kuna mtu mmoja ambaye anawajibu wa kuleta upatanishi pale ambapo
tunafikiri kuwa kuna khali ya kutokuwa na amani; Yesu alikuwa anatuagiza sisi
sote kuwa jukumu la luleta upatanishi ni letu sote.lakini upatanishi wa kweli
utapatikana kama tunajua jinsi ya kusali; jinsi ya kuongea na Mungu kama Yesu
alivyokuwa.
je tunajua kuwa amani huleta haki na furaha ya maisha? Na
amani ya kwelihupatikana kwa sala ambayo hutufanya sisi kuwa wanyenyekevu.
Kwa hiyo tukiendelea na
tafakari yetu katika mwaka huu tukumbuke kuwa sisi nasi leo tunatakiwa
kuendelea kuomba kufundishwa jinsi ya kusali kama wafuasi wa Yesu walivyo omba
kufundisha na Yesu aliwafundisha.
No comments:
Post a Comment