January 4
Tafakari yetu leo inaelekwezwa katika agizo la Yesu kwa wafuanzi
wake na wananfunzi wake pale alipofundisha kuhusu amri ya Upendo kwa jirani
kama tunavyojipenda wenyewe. Yesu angeweza tu kusema mpende jirani yako na
kuishia hapo; lakini kwanini aliamua kuhitimisha kwa maneno haya “ Kama
unavyojipenda Mwenyewe”?
Binadamu tuna huluka na silika ya kujipenda zaidi sisi wenyewe
kuliko kumpenda mtu mwingine. Ni tabia ambayo tunayo na imekuwa vi vigumu
kuondokana nayo; tafakari ya leo inatukumbusha kuwa agizo la Yesu ni la muhimu
ili tuweze kuuridhi uzima wa milele lazima na jirani zetu tuwapende katika
mizani ile ile tunayojipenda sisi wenyewe. Katika biblia kuna amri kuu mbili za
upendo wa kumpenda Kwanza Mungu kwa moyo wetu wote, na ya pili
inafanana na hii ya kwanza ya kumpenda jirani: “Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe.” (Mathayo 22:39)
Hapa tuna jifunza kuwa kumpenda jirani, kama
vile kumpenda Mungu, si hisia tu; ni jambo linalotakiwa lionyeshwe kwa matendo.
Kuwapenda wengine kama tunavyojipenda wenyewe kunamaanisha kwamba tunawaona
wengine kama tunavyotaka watuone na kuwatendea kama tunavyotaka watutendee.
Golden Rule; ambayo msingi wake kiimani kuwa Mtu
wa MUNGU ni yule aliyekaa katika pendo. Je wewe leo unajitambua
kuwa umekaa katika upendo?
Tukisoma kitabu cha Walawi 19:17 kinatukumbusha kuwa : Usimchukie
ndugu yako moyoni mwako; na pale ambapo jirani yako hajefanya sawasawa ni
lazima kumkemea jirani yako, hatuna sababu ya kuumia kimoyomoyo na
kutenda dhambi ya masengenyo dhidi yake; pale inatotupasa kumsahihisha jirani
kwa upendo na tatufnji hivyo tunaishia kutenda dhambi mbele ya mungu
kwa malalamishi yetu juu ya jirani. Tunaweza kuirekebisha dhambi hii kwa
kukwemea.
Mfano mwingine mzuri kuhusu upendo wa jirani hadithi ya Yesu inayopatika katika kitabu cha
Lk. 10:30 mtu aliyeshuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko na kuangukia katika
mikono ya wanyanganyi ambao
walimpiga , kumvua nguo, walimwumiza na kumwacha karibu kufa; Tunaona Kuhani
ambaye ni mtu anayejua sheria za dini na wajibu wake kwa jamii alikuwa akipita
alimwona na kupita kando bila kutoa msaada wowote; Mlawi naye alifanya hivyo
hivyo; lakini msamaria mwema yeye alifika mahali hapo na kwa matendo alionyesha
upendo wa khali ya juu kwa kumfunga majeraha yake na kumpa huduma zote kama
alivyoweza na kasha kuondoka naye na kumpeleka katika sehemu nyingine ambyo
aliweza kupata matibabu zaidi kwa gharama zake. Msamaria mwema hapa ameonyesha
upendo wa khali ya juu na hivyo yeye amekuwa jirani kwa mtu hutu aliyekuwa akihitaji msaada.
Ni vigumu sana kutekeleza agizo hili la Yesu
kama hatuna upendo wa kweli; tukumbuke kuwa tunda la Roho ni upendo, ambao
utaleta furaha, amani,
uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, na upole; kwa
kutekeleza upendo huleta ujirani mwema na utekelezaji wa amri hii kubwa ya
kupendana kwani huta mwia mwenzako na kitu chochote, isipokuwa kupendana; kwa
maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue,
Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inakamilishwa katika neno
hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani
neon baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria”.
Tunaishia kuvunja amri hizi zote kwa sababu
hatuna upendo ndani yetu; tukiwa tumetawaliwa na upendo, hatutaweza kuiba kwani
kwa kuiba unamwibia jirani yako; kwa kusema uwongo unamkosea jirani yako ili
kumletea matatizo ambayo hastahili kuyabebe. Ukizini unatenda kosa la kumsaliti
jirani yako ambye ni mUme wako au Mke wako; kwa ufupi tukitimiza amri ya upendo
inavyotatimwa hatuwezi kufanya dhambi yeyote, bali tutaweza kuishi maisha ya
amani na upendo mkubwa sana kwa kujali na kusaidiana kama biblia inavyotaka
sisi leo tuishi.
Basi siku ya leo tuendelee kutafakari nafasi
yako au yangu katika kutekeleza amri hii kubwa ya upendo kwa matendo amen.
No comments:
Post a Comment