January 29:
Tafakari ya leo hebu
tuangalia dhana ya uvumilivu tukisoma Luka 9;52-56, akatuma wajumbe kutangulia
mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha wasamaria, ili
kumtengenezea mahali; lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyoulekeza
uso wake kwenda Yerusalemu. Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo
walisema Bwana wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni uwaangamize: kama
Eliya naye alivyofanya?
Yesu akawageukia
akawakanya Akasemahamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo; kwa maana mwana wa
Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa.
Ni ukweli ulio wazi
kuwa kiongozi anatakiwa kuwa, mtulivu, mvumilivu na anayetumia zaidi
hekima kuliko mabavu kama Yesu alivyowaambia wnafunzi wake.
kiongozi
anatakiwa Kuwa na msimamo wa uvumilivu ni moja ya kazi ngumu zaidi
miongoni mwa viongozi dhidi ya wananchi katika jamii. Ni ukweli ambao
haufichiki kuwa viongozi hawakuzaliwa wakiwa wavumilivu, lakini lazima
tujifunze kuwa wavumilivu. Na hii ni kweli hata kwa jamii inatupasa kuvumiliana
na kumaliza tofauti zetu kwa busara ya majadiliano.
Katika siasa uvumilivu wa
kisiasa unakuza utamaduni wa utawala bora na ukomavu wa demokrasia; na
Kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, wananchi lazima kuwa tayari kuvumilia na
kuvumiliana.
Dhana ya uvumilivu ni ya
msingi sana kwa maendeleo kwani inaruhusu mawazo mapya ndani ya jamii; kupitia
dhana hii ya uvumilivu, kiongozi anakuwa tayari kukubali na
kuheshimu maoni na mawazo ya watu wengine na haki zao kwa uwazi na uhuru.
Katika hali hii,uvumilivu huruhusu kuwepo kwa vyombo huru vya habari
kutumika kama chombo muhimu kuwahabarisha wananchi na kuwasilisha madai yao kwa
viongozi wao.
Tafakari ya leo unatujenga
katika upana wa kuelewa dhan ya demokrasia inahitaji vyombo vya habari ambavyo
hugeuka kuwa daraja la mawazo kati ya viongozi na waongozwa. Vyombo huru vya
habari husaidia wananchi kuelewa taratibu ambazo zinaimarisha
demokrasia. Bibilia inatumbusha kuwa kuptia Uvumilivu wa viongozi kufuata mambo
ya amani na mambo yafaayokwa kuengana; hali hii itasaidia kueneza uwajibikaji
kwani wananchi wataweza kukosoa serikali na ujumbe kufikishwa serikalini bila
kuogopa kwa kuelewa dhan ya uvumilivu.
Yesu alikuwa mwanaFalsafa Mkuu wa Uvumilivu
anawa na kuwakumbusha viongozi na wananchi wanatakiwa kuishi kulingana na
fikira njema. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hayuko tayari kuamsha fikra
mbaya za uvunjajiwa amani bali daima atajitaidi kuziepusha kwa kuendeleza
uamuzi wa uwazi na kwa kutumia njia ya utulivu wa hekima kupitia
uzoefu makini wa kimantiki: Kiongozi mwenye uvumilivu daima hutafakari, na
kuziweka fikira mahali pamoja kabla ya kufanya uamauzi.
Ni ukweli ambao haufichiki
kuwa sisi kama wananchi tukiweza
kuvumiliana katika maisha yetu ya kawaida, na kuweza kukosoana bila kugombana mara
moja hurudisha imani ya wananchi, upendo na matumaini kati wananchi wao
kwa wao au dhidi ya serikali yao; Tukumbukwe kuwa Ingawa watu wengi kufikiria
uvumilivu ni upole na kuto wajibika la hasha uvumilivu ni uwajibikaji
ulio jaa busara na subira; Hii ni tafakari yetu ya leo. Amina
No comments:
Post a Comment