January 7
Tafakari ya leo inahusu swala nzima la umuhimu wa
uwajibikaji na maagizo ya bibilia yanavyosisitiza umuhimu kwa viongozi wote wa
dini na siasa na serikali kuwajibika kwa Taifa husika. Tunajua kuwa viongozi wa dini wanao wajibu wa kuhakikisha kuwa wanawa hudumia
waumini wao ipasanyo katika kutimiza kazi ya mungu kwa umakini, upole na
unyenyekevu, na lazima matendo yao yawe na mfano wa uwajibikaji wenye Tija kwa
taifa.
Ni ukweli kuwa uwajibikaji unahusu uadilifu,
uaminifu, unyenyekevu, kutenda haki, kujali wananchi wanyonge ambao hawana
kimbilio isipokuwa kwa kiongozi mwabijikaji na awezaye kusimamia haki kwa wote; Tufahamu kuwa leo hii wananchi
wanawahitaji viongozi ambao ni wawajibikaji, waadilifu, wakweli, na
wanao mwogopa Mungu katika matendo yao. Ndio maana sikuhizi wananchi wanao uwezo
mkubwa wa kuwawajibisha viongozi wao ambao utendaji wao sio mzuri; wanaojali zaidi masilahi binafsi, na sio ya
Taifa; ili kuwapa wananchi wao maendeleo wanayoyatamani kwa naona waweze
kujiona kama ni sehemu ya jamii ambayo inafurahia matunda ya taifa lao.
Bibilia inatukumbusha kuwa viongozi lazima wawe
waadilifu na wanajali uwajibikaji wa taifa uadilifu huleta upendo kwa taifa na
mshikamano kama tunavyosoma kutoka katika
kitabu cha 1 wakorinto 13. Wazo kubwa hapa ni upendo ambao unasaidia kufanya
kazi kwa uadilifu; upendo ni kila kitu haufurahii udhalimu bali hufurahia dhana
ya pamoja.
Tukizingatia kuwa wananchi wanawachagua viongozi
kwa vile wamewaamini na kuwapa dhamana na sio bure wanawataka sasa waweze
kuwajibika; kiongozi ambaye hawajibiki hujenga chuki, hasari, visasi kati yake na wananchi ambao wameamua kuwachagua.
Matayo 6; 22 anatukumbusha kuwa uwajibikaji ni taa ya ni jicho; basi jicho lako
likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru, hii ndio dhana ya uwajibikaji.
Marko anafafanua vizuri sana 10:45 kwa maana mwana wa Adamu naye hakuja
kutumikiwa bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe faida ya wengi.
Kiongozi mzuri atafurahi pamoja na wananchi wake na
atalia pamoja na wananchi wake; kwani ukitaka kuwa kiongozi lazima uwe mtumishi
wa wote. Tunawaombea viongozi wetu wawe na moyo safi wa kuwajibika na
kuwafundisha wakubali kukosolewa na wale ambao wanashindwa kuwajibika tuweke
mfumo wa kuwawajibisha. Tukumbuke kuwa hakuna kiongozi ambaye anasifiwa akiwa
ni mtu wa kuendekeza ubinafsi, bali ukiwa mwajibikaji mtoaji kwa wananchi
katika maendeleo yao huwa unasifiwa sana na unapata baraka za kimungu.
Kiongozi mwajibikaji huwa anaangalia kwanza
masilahi ya watu wake; Yesu katika kitabu cha Matayo 11.28- 30 alielezea nini
maana ya uwajibikaji kuwa unakuwa ni kimbilio la wanyonge aliposema njoni
kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawawapumzisha.
Viongozi ambao sio wawajibikaji hutumia nguvu zaidi
katika kuhakikisha kuwa jamii inapoteza haki zao za msingi nguvu zao za kipesa
pamoja na wafuasi wao wachahce na hivyo kuwatesa
wanyonge kwa kuwanyima haki zao za msingi kama, matibabu, haki ya kupata huduma
bora za usafiri na maji salama, haki ya elimu bora na malazi salama.
Kiongozi mwajibikaji na mwogopa mungu ataweza
yasimamia vyema shida za jamii yake na analinganishwa na maneno haya mimi ni mpole
na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapata raha nafsini mwenu nitawatua mizigo yenu. Tunahitaji viongozi wa kama Yesu katika jamii zetu watakuwa wapole hawana kiburi na wanamwogopa mungu.
Kitabu cha Wafilipi 2.3 –4 kinatukumbusha kuwa tusitende
neno lolote kwa kushindana wala majivuno bali kwa unyenyekeve, kila mtu na
amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake
mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Hii ndio dhana ya uwajibikaji ambayo bibilia
inataka sisi tutekeleze kama viongozi. Tunatakiwa tutimize kusudi la mungu
ambalo ni njema mbele ya watu tunaowaongoza. Tukumbuke kuwa pale tunapowatendea
haki waja wa Mwenyezi Mungu Yeye aliyeanziasha hii kazi nzuri Moyoni mwetu
hatatuacha peke yetu atakuwa nasi na ataendelea kutupa nguvu ya ajabu katika
kutimiza wajibu wetu kwa Taifa lake.
Hii ni tafakari ya leo ambayo
tukiitekeleza ipasavyo itatatufunulia nuru ya kweli katikautendaji na uwajibikaji wetu -
amina
No comments:
Post a Comment