January 5
Je umeshafikiria jinsi gani ni rahisi
kupoteza muda wako katika kufanya au kufikiria vitu ambavyo sio vya maana
katika maisha yako ya kila siku?
Tunahitaji kutafakari kwa khali ya juu
jinsi ya kutumia muda wetu vizuri, na kitu kikubwa amabcho kinaweza kutusaidia
katika kufikia tafakari ambayo ni nzuri, ni kuangalia muongozo ambao lazima tujiwekee
katika maisha yetu ya kila siku. Bibilia inatuongoza kuwa kama tutaweza
kuyangalia maisha katika kuruzi halisi tunaweza kujiepusha na matatizo mengi
sana ambayo yako mbele yetu leo.
Tatizo kubwa tumejikita katika mambo
ambayo hayana faida yeyote kwetu. Tukumbuke mwenyezi mungu baada ya kuumba mbingu
na dunia na kumkabidhi Adamu utawala wa dunia hii pamoja na Hawa. Aliwaambia wafuate
sheria na utaratibu ambao aliwawekea ambao ulikuwa raisi sana; ilikuwa jukumu
tu la wao kufuata maelekezo. Lakini kwa vile hawakuzingatia mambo muhimu Nyoka
aliwasaliti kwa kuwadanganya na walidanganyika. Matokeo yake walikosa
kabisa maisha mazuri ambayo waliandaliwa na Mwenyezi Mungu. Mafano huu ni sawa
na msemo usemao huwezi kufukuza sungura wawili kwa wakati mmoja kwani wote wawili
watotoroka na hutaweza wakamata.
Ili tuweze kufanikiwa inatakiwa tuzingatie
zaidi upande mmoja. Kama Bibilia inavyotukumbusha kuwa
hatuwezi kumtumikia Mungu na Mali au
anasa za dunia hii; Ni jukumu letu kuchagua tumtumikie au Mungu au Mali kwa upande
mwingine. Hatuwezi kumtumika mungu na Mali kwa wakati mmoja. Tukisoma kitabu
cha Waefeso 5.17 kwa sababu hiyo msiwe wajinga bali mfahamu ni nini yaliyo
mapenzi ya bwana.
Hatutakiwe tuwe wapumbafu na maisha
yetu, tukumbuke kuwa tumepewa zawadi ya maisha kuishi mara moja tu hata kama
tutakuwa na pesa nyingi au nguvu vyote ni vya msimu tu, bado tunatakiwa kuwa
makini katika maamuzi yetu na mali zetu na nguvu zetu tunazitumiaje. Mwenyezi mungu
anataka sisi wenyewe tujipangie nini tunataka na tutatumiaje?
Uzuri ni kuwa Mwenyezi Mungu anampango
mzuri na kila mmoja wetu, lakini tatizo letu hatusikilizi sauti yake, tunaleta
kiburi na kukataa kufanya kazi ya Mungu mfano wa Yona 1:2 alipoambiwa aondoke na kwenda ninawi, akapige
kelele juu ya Mungu, lakini Yona akaondoka na kwenda Tarshishi, ili aweze kujiepusha
na uso wa mungu lakini tunajua nini kilimtokea Yona. Mungu alituma dhoruba na
Yona akatupwa baharini na kumwezwa na samaki mkubwa na kukaa ndani ya samaki
huyo kwa siku tatu;
Tafakari hii ya leo inatufundisha kuwa lazima
tuwe makini katika malengo yetu na vipau mbele vya uchaguzi wetu juu ya nini
tunataka kufanya na kuwa; tunatakiwa kuwa makini katika kukisikiliza sauti ya
Mungu, sio kukumbatia zaidi yale ambayo sisi tunayataka ambayo hayana faida kwetu
ya kudumu kwani mwisho wa siku tumalizapo maisha ya hapa dunia tunajikuta tuko
njia panda.
Tunatakiwa tukumbuke kuwa Mungu yuko
kila mahali na tunalijua hilo ila mara
nyingi tunaendelea kumjaribu na huku tukifikiri kuwa Mwenyezi Mungu hatuoni na
uovu wetu. Popote pale ambapo tutakuwa au tutakwenda yeye yuko, tujifunze toka
kwa Yona pamoja na kubadilisha mwelekeo Mkono wa Mungu ulikuwa juu yake.
Tunapokataa sauti na maelekezo ya Mungu
ni na maamuzi na ishara ya kiburi na
ubinafsi. Ndio maana mwisho wa siku ni sisi tunakuwa tumefanya kazi ambayo haina
malengo na mafanikio kwetu wenyewe. Tukisoma zaburi 139:7 inauliza je naweza
kwenda sehemu nyingine yeyote kuogopa
roho wa bwana?
Lakini tukumbuke kuwa Mungu ambaye
daima anaanzisha kazi nzuri ndani yetu yeye ndiye atakaye ikamilkisha ndani
yetu kitabu cha Wafilipi 1:6; kinatueleza kuwa Mungu daima anafanya kazi ndani ya
maisha yetu tunachotakiwa ni kuelekeza akili na nguvu zetu kwake na kuacha tabia
ya kufukuza sungura wawili kwa wakati mmoja kwani tutapoteza malengo muhimu. Mungu
anajua
nini kitu muhimu
unachohitaji au unachotakiwa kufanya au kuwa, kinachotakiwa tu kwetu ni
kumsikiliza na kutimiza wajibu wetu kama binadamu.
La msingi tunapopatwa na matatizo
tunatakiwa kujiuliza nimefikaje hapa, uwe ni kiongozi wa serikali au raia wa
kawaida au mtumishi wa Mungu.
Je unatenda haki kwa wananchi wako,
wanatendewa vile mungu alivyokuagiza uwafanyie? Haki zao wanapata? Je kwa
wananchi wa kawaida nasi tunatimiza wajibu wetu kwa serikali kama inavyotakiwa?
Je viongozi wa dini wanaisadiaje
serikali na wananchi wake katika kusikia sauti ya Mungu?
La msingi katika tafakari ya leo sote
tunafanya makosa la msingi tunatakiwa
kwanza tuweze kukiri dhambi zetu na kuwa tayari kuziacha, hii itatusaidi tuweze
kupata nguvu mpya ya kuanza upya na hatutakiwi kurudia tena kosa la kufukuza
sungura wawili kwa wakati mmoja . lazima tuchague kumfukuza mmoja ambaye
atakuwa na faida endelevu kwako. Na kitabu cha 2 cha wakorinto kinatumbusha
kuwa tunakuwa wapya na tunaweza kuanza malengo yetu mapya ambayo yatatupa dhawabu
kubwa mbele ya Mungu.
Kwani yeye daima ana mipango mizuri juu
yetu daima. Kama alivyo mpa Yona nafasi ya pili na alitimiza kazi ya kuhubiri
na kuwakoa wale walikuwa wapotea. Tukumbukekuwa mungu yuko kila mahali, Mungu
wetu ni wa msamaha daima hivyo hatujechelewa kupokea baraka za Mungu kwa mara
ya pili. Amen
No comments:
Post a Comment