February 17,
Tafakari ya leo hebu
tuangalie dhana ya mijumuiko wa wakati wa kumwabudu Mungu. Kanisa
linawajumuisha wapendwa katika kutimiza wajibu mmoja mkubwa kwa kumwabudu,
kumsifu na kumshukuru Mungu; hata yale makanisa ya kwanza kabisa katika
mijumuiko yake yalikuwa na lengo moja kubwa kumsifu Mungu, kwa sala na nyimbo
na neno la shukrani.
Tafakari yetu ya leo
inatumbusha kuwa makanisa ua mijumuiko yetu ya imani iwe na lengo la kutenda
haki ya kumsifu Mungu, kumshangilia Mungu na kwa Baraka zake kupitia
mikusanyiko yetu tumepewa uwezo wa kuwaombea wenye shida mbalimbali, za
magonjwa, vipato na maisha mema yenye kibali cha Mungu. Tuanajua katika
makanisa yetu tuna washiriki ambao wanauwezo wa kifedha kuliko uwezo wa kanisa.
Kamwe tusiwageuze hao kuwa miungu watu wetu, kaw kuwasifu wao zaidi kukiko
Mungu kwa vile wao tunawaona.
Tukisoma kitabu cha 2
Wakorinto 4:15 kwa maana mambo yote ni
kwa ajili yenu, ilineema hiyo ikiongezwa sana kwa hao walio wengi shukrani
izidishwe, na Mungu atukuzwe . Kuishi kwa imani. Tukumbuke kuwa Mungu ndiye
atupaye sisi mkate wetu wa kila siku, ni yeye pekee awezaye kutupa sisi
mbegu na mazao yetu yakaongezeka mara
dufu.
Hii inatakiwa kuwa ni
sehemu ya maisha yetu sisi wakristo kwa kuendelea kumpa sifa na mtukufu Mungu
wetu kila siku; kama 2 wakorinto 9: 11 inavyotuambia mkitajirishwa katika vitu
vyote mpate kuwa na ukarimu wote umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Hivyo hili
linatakiwa kuwa ni jukumu letu la kila siku. Tukumbuke kuwa sio tu tunapata
wokovu toka kwake bali tunapata kila kitu toka kwake. Kama sio Mungu unapata
wapi jeuri ya afya njema?
Paulo katika kitabu cha
Waefeso 5:3 anasisitiza kuwa lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala
uchafu wo wotewa kutamani, kama iwastahilivyo wakatakatifu. Wala aibu wala maneno
ya upuuzi wala ubishi; hayo hayampendezi bali afadhali kushukuru. Hivyo Tafakari
ya leo unasisitiza katika kushukuru, kushukuru kushukuru. Tunapofungua midomu
yetu tujiepushe na maneno yote mabaya, machafu ambayo hayampendezi Mungu au
jirani yako. Bali tufunguapo midomo yetu imiminike kwa maneno ya shukrani.
Tuombe kujazwa na Roho wa bwana kwani yeye ndiye kioo cha shukrani atatupa
maneno mazuri ya shukrani.
Sala na kushukuru iwe
ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, tunatakiwa tuanze sana kujijengea utamaduni
wa kushukuru na kutoa shukrani kwa kila kitu na kwa wakati wowote;
tukianza kujenga utamaduni wa aina hii
hata maisha ndani ya Jumuia zetu yatabadilika na tutabarikiwa sana, kwani
katika Kristo unakaa utimilifu wote wa mungu kwa jinsi ya kimwili.
Paulo alipokuwa akiongea na
Wakolosai 3: 15, 17 aliwaambia Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo
mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Na kila mfanyalo
kwa neno au kwa tendo, fanyeniyote katika jina la bwana yesu, mkimshukuru Mungu
Baba kwa yeye.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tuendelea kusali bila kuchoka ikiwa ni sehemu ya muhimu ya
maisha yetu katika kusifu na kushukuru kwa Mungu wetu. Sala ni kitu ambacho
kinatakiwa kuwa cha furaha daiam na unafurahia kufanya hivyo, lakini kama wewe
wakati unapomshukuru Mungu kwa sala
unakuwa huna furaha ujuwe kuwa bado unatawaliwa na kumilikiwa na mambo
ya ulimwengu huu. Hivyo ukijikuta katika wakati huu inatakiwa umwombe roho
Mtakatifu akubadilishe na atakupa furaha ya kweli wakati unasali.
Tafakari ye leo wakati
tunaendelea na kipindi hiki cha toba tunatakiwa kufurahi kila wakati, tusali
kila wakati, na tumtolea Mungu shukrani kila wakati. Mungu anatupenda san asana na anataka sote tushiriki naye katika karamu ya
mwisho tukiimba na kusifu pamoja naye hii ndio tafakari yetu ya leo.
No comments:
Post a Comment