February 25
Katika tafakari ya leo tunajikumbusha ukuu wa
neno Amina: Neno AMINA linalotumika sana katika maswala ya imani, ni neno lenye maana nzito kwani ni neno ambalo
limetumiwa sana katika bibilia na katika sala na ibada zetu za kila siku.
Neno Amina linaashiria
umoja wetu katika kuamini kile ambacho kimesemwa au
kuombwa kwa Mwenyezi Mungu: Neno Amina linatuunganisha sote katika sala au
maombi na kukubalina katika umoja wetu mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kwa ufupi ni neno linaloashiria “na iwe hivyo”; “tunakubaliana
katika hili tunaloliomba”; “tunaamini
katika uhakika au kuwa na uhakika wa kile tunachokiomba au kukisifu”.
Tunasema neno Amina wakati wote wa ibada zetu
za kila siku, katika sala zetu; Katika mijadala yetu; kwa ujumla Neno Amina
linahitimisha sala na maombi yetu ikiwa ni kielelezo cha makubaliano yetu na MUNGU.
Tukisoma kutoka katika kitabu cha kumbukumbu la
Torati 27:16 inasomeaka hivi na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na
watu wote waseme, Amina. Hii inamaanisha kuwa wote wanakubaliana na laana hii
kwa umoja wao.
Tafakari ya leo inatuonyesha kuwa Amina
inamaanisha kuwa tunakubaliana na Baraka zote, ikiwa ni katika kuzipokea; Zaburi ya 72: 19 inasema kuwa jina lake tukufu na lihimidiwe
milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina, Amina
Tafakari ya leo inatuonyesha jinsi Yesu
alivyosema neno Amina katika mafundisho na mahubiri yake kuliko mwalimu
mwingine yeyote katika Bibilia. Katika John 3:3 Yesu akajibu Amina amina
nakuambia Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Katika majibu
na mafundisho ya Yesu alikuwa anatuonyesha kuwa yale aliyokuwa akiyafundisha na
yawe hivyo. Hapa tunajifunza kuwa neno amina linaonyesha uthibitisho katika kukabiliana Na
yale ambayo yamesemwa au kufundishwa.
Somo muhimu leo ni kuwa "Amina ,"
tunasema , wakati wowote na tunamthibitishia Mungu kuwa toka imara na tuamini kuwa kile tunachokiomba
tunaomba tupate Baraka kutoka kwa Mungu.
Neno Amina tukilisema kwa dhati Mungu atatimiza ahadi ya maombi yetu na kupata neema na baraka tuziombazo tukumbuke kuwa ahadi zote za Mungu tunazipata tukiamini na kushukuru kwa kutumia neno lenye nguvu Amina. Kila kitu ambacho Mungu ameamwahidi mwanadamu, atatimiza. Tukumbuke kuwa Yesu wakati anasulubuwa tukisoma Luka 23: 43 akamwambia Amina nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa neno AMINA lina nguvu sana, kwani
tunalitumia mwishoni mwa sala zetu, tukiwa na maana kubwa ya asante kwa Mungu
kwa kupokea maombi yetu. Hivyo Amina inatufungulia kila ahadi ya baraka, amani
, utoaji , faraja , msamaha, uzima, na utakatifu tukiendelea kutambua kuwa yeye ni mwenye utukufu na nguvu, milele na milele. Amina.
No comments:
Post a Comment