February 9
1
Wathesalonike 5:18 , Paulo anaandika, " shukuruni kwa kila jambo maana
hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. " Paulo anatuagiza bila
kuchagua maneno kwamba ni lazima tushukuru kwa kila jambo; katikana hili
tumeambiwa hakuna udhuru bali wajibu wetu ni kutoa shukrani . Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tendo la
kushukuru ni la lazima na linatuunganisha na kila jambo katika maisha yetu
ambayo yanatakiwa kujaa shukurani, bila kujali nini kitatokea mbele yetu. Lazima
tutambue kuwa tendo la kushukuru ni
kiini
cha maisha na bora ya Kikristo. Na kuwa wasio na shukrani ni kiini na moyo watu
waovu wasio mwogopa Mungu. Watu wa namna
hiyo hawako tayari kumpa Mungu sifa za utukufu kwa matendo yake makuu kwetu. Tunajua
kuwa Mungu ndiye muumba wa kila kitu, mungu ametupa sisi wanadamu uhai, mungu
ametupendelea sisi wanadamu na ametupa akili ya utambuzi wa jambo jema na baya;
hivyo tuna kila sababu ya kumpa asante kwa zawadi hii kubwa.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tusiwe katika kundi lile wa watu wapumbavu ambao wao wanajua
kuwa kila kitu katika maisha yetu vinatokea kwa bahati na hakuna mkono wa Mungu
juu yake, hivyo kwani wawe ni watu washukurani? Wamshukuru nani wakti vitu
vyote vinatokea kwa bahati? Ni kweli utawezaje kuishukuru Bahati na bahati
haina hata bahati kwa yenyewe? Watu wa aina hiyo ni wanyama hawana kabisa moyo
wa utu na wa ubinadamu ndani yao;
Tafakari ya leo pia
inatumbusha kuwa tujitahidi kujiepusha kundi la watu wanaoamini kuwa hawana
shida ya kushukuru kwa kuwa wao wenyewe tayari wameshafanikiwa kimaisha,
wanamawazo mazuri, wanao ujuzi wa kutosha kuendesha maisha yao, na mafanikio
yote ambayo wanayafurahi ni kazi ya mikono yao bila msaada wa Mungu; sifa za
mafanikio yao ni katika mikono yao na akili zao kwa mipango yao, bidii yao;
ujuzi wao na mbinu za ubunifu ambazo wanazo; sasa kama wao ndio vinara wa
mafanikio yao nafasi ya mungu iko wapi? Na kwa nini wamshukuru? Hivyo wanajipongeza
wenyewe kwa sababu wao wenyewe ndio mafundi na masonara wa maisha yao.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa dunia hii ukiangalia imeundwa na makundi matatu ambayo
hayana shukrani kwa Mungu. Kundi lile linaloamini kuwa wao maisha yao
yamejengwa katika bahati hivto hawana sababu ya kumshukuru Mungu; Kundi la pili
ni lile linalofikiri kuwa hawaamini katika uwepo wa Mungu ila kuna nguvu tu ya
aiana yake katika mafanikio yao sasa hawaoni sababu ya kushukuru. Na kundi la
mwisho linalojiamini kuwa wao ndio sababu ya mafanikio yao na maendeleo yao
sasa kunasababu ya kutoa shukrani? Na kama ndio sasa wamshukuru nani, kwani
wanastahili kujishukuru wao wenyewe.
Tunachojifunza hapa ni kuwa
wajibu wa shukrani uko mikononi mwa watu wote wanaoamini katika ukuu wa mungu
na matendo yake makuu katika maisha yao. Wakristo wanapaswa kumshukuru Mungu
kwa kila jambo; Shukrani ni jambo muhimu sana katika maisha yetu kama wakristo. Ni
ukweli usiofichika kuwa kuna wakristo ambao sio watu wa shukrani. Je wewe
unamshukuru hata jirani yako aliyekutendea jambo njema? Ni rahisi kumwona Mungu
kupitia upendo wa jirani yako; hivyo tunakila sababu ya kusema asante Mungu kwa
wema wa Jirani yangu.
Tukisoma Warumi 8:28 nasi
twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale
wampendaokatika kuwapatia mema yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Mungu anafanya
kila jambo kwa ajili ya mafanikio yetu hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru; na
kama tuanaamini kuwa Mungu yuko kazini katika maisha yetu, na kubadilisha
maisha yetu kuelekea katika maisha bora, tuna kila sababu ya kusema asante.
Hata tunapopatwa na shida bado twatakiwa kushukuru kwani hatujui nini hatiam ya
maumivu yetu. Kwa Mungu baada ya maumivu yetu mwisho wake ni kheri. Hata
unapofanyiwa upasuaji wa tunashuhudia maumivu makali lakini hatima ya maumivu
haya makali ni uponywaji wa kudumu.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tuwe watu wa shukrani kila wakati na katika mazingira yeyote
yale. Amina
No comments:
Post a Comment