February 12
Tafakari ya
leo tufungue mioyo yetu na tusikie "Sauti ya mtu imesikika jangwani:
`Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake. Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima
vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa. Na, watu wote watauona wokovu
utokao kwa Mungu."`
"Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani
aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja? Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu”.
Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi? Akawajibu, Aliye na nguo
mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo. Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, Mwalimu,
tufanye nini? Naye
akawaambia, Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa.
Nao askari wakamwuliza, "Na sisi tufanye
nini? Naye akawajibu, Msichukue vitu vya
mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara
yenu."
Tafakari ya leo
natamani kulizungumzia neno hili Toshekeni na mishahara yenu:
Neno hili ni zito japo lilizungumzwa kipindi
kirefu nyuma lakini tunaendelea kulishuhudia leo tunapowaangalia watendaji wetu
katika serikali zetu; Neno hili linatufundisha uadilifu, uwajibikaji kulingana
na maadali na kanuni za kazi ambazo
zinatulazimu sisi kama watendaji wa Taifa kuweka mbele matakwa ya Taifa na sio
masihahi binafsi;
Najiuliza
tena Neno hili linamaana gani kwa taifa
letu?
Kama nchi na
wananchi wake tunahitajii uhuru wa kiuchumi ambao unatokana na viongozi wetu waridhike
na mishahara yao; kinyume chake kama hawataridhika na mishahara yoa na kuweka
mbele masilahi yao vitendo vya rushwa na
ufisadi ambao unarudisha maendeleo ya Taifa nyuma sana vitadhidi kuendelea.
Tafakari itukumbushe
sisi Kama Taifa na kama Raia na
watendaji ambao tumekula kiapo cha utii na maadili bora ya uwajibikaji kwa Taifa
letu kuwapa wananchi wanyonge zawadi kubwa ya
uhuru wa kiuchumi ni ili kila mmoja wetu aweze kuyafurahia zawadi pekee rasilimali ambayo Mungu amelijalia Taifa hakuna
atayepingana name kuwa nchi yetu
imefurikakwa asali na maziwa tazo ni
wachache tu ambao wanafaidi kwa kutoridhika na mishahara yao.
kwa kipindi kirefu tumeona kuwa nchi yetu Tanzania iliyokuwa ikifurika neema ya rasilimali sasa imegeuka; kwa wengine imekuwa ni nchi inayofurika machungu; matendo yaleyale ya kifisadi, ya ukandamizaji, ya unyanyasaji ambao Farao aliwatendea wana wa Israeli huko misri miaka hiyo; lakini kwa kuangalia falsafa hiyo ya matendo ya Farao ndio tunaona Namna watendaji wetu walikokabidhiwa dhamana ndani ya Taifa letu ambao sio waadilifu wananyatenda sasa yanaenda kinyume na uhuru tuliopewa kama zawadi kuto kwa Mungu ambao kila mmoja anastahili kufurahia na kufaidi asali na maziwa yanayofurika katika nchi hii. Na sio kwa kikundi kidogo cha watu.
Yohane Mbatizaji a usitadhi kabisa anayafafanua makundi yaliyokusanyika uwiano sahihi wa toba. Kulingana na Yohane matajiri wanaotakiwa kuangalia haki ya maskini, "Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo."(Lk 3,11), kwa watoza ushuru waepuke rushwa na matendo ya kifisadi "Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa."(Lk 3,13) na kwa maaskari wazingatie haki "Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu."(Lk 3,14).
Leo hii ndani ya Taifa vitendo hivi vimeshamiri tena kwa kiasi kikubwa katika jamii yetu, na pengine kila mmoja ameshiriki kwa namna moja au nyingine katika uovu huu, moja kwa moja au kwa kutokuwajibika ipasavyo katika eneo lake la kazi na hivyo kusababisha mianya katika kukua kwa matendo haya maovu. Tafakari ya leo inatuasa sisi kama Taifa inatupasa tubadilike na kuhakikisha haki na upendo vinashamiri katika jamii yetu.
Kama tutafanikiwa kuishi kwa ujumbe huu wa Yohani Mbatizaji kuwa tutosheke ni mishahara yetu mimi naamini kuwa tukiweka mbele maslahi ya nchi, nchi itasonga mbele. TUKUMBUKE KAULI YA YOHANA MBATIZAJI KWA WALE ASKARI kuhusu dhuluma: TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU, watu wana madaraka makubwa mishahara mikubwa na masurufu manono lakini bado wanaiibia nchi.

Je watendaji wetu wako tayari kutoa hesabu za utendaji wao siku
watakapotakiwa na Mwenyezi Mungu tukiamini kuwa kazi zote hutoka kwa Mungu “Sisi
tunajielewa kuwa ni watenda kazi wa saa ya kumi-na-moja katika shamba la Bwana
la siku za mwisho, na kwamba ingawa mishahara yetu haijulikani mapema,
lakini hatuna mashaka kwa sababu Bwana wetu ni mkarimu”.
Tafakari hii inatufundisha kitu kingine kipya kuwa tunatakiwa kujihadhari na tabia ya kupenda fedha, na yatupasa toshekeni na vipato tulivyo navyo kwa sababu Mungu
mwenyewe alisema,
Tukisoma Ebr 13:5,6 Kwa vyovyote sitakupungukia kabisa, wala sitakutelekeza na
kukuacha bila msaada. Kamwe, kamwe, sitakuacha hata kwa kiwango kidogo,
kukuacha bila msaada, au kukuacha, au kukuangusha, au kulegeza mkono wangu
kwako. Hakika sitafanya hivyo! Kwahiyo tunafarijika na kutiwa moyo, na kwa
uhakika na ujasiri twathubutu kusema, ‘Bwana ndiye anisaidiaye.
Kwa kutosheka na mishahara yetu na kwa kuamini kuwa sisi ni
wachache ambao tumechaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa saidia wengine ili waweze
kupata ridhiki zao; au kufurahia asali na maziwa kwa vipaji vyetu kwa kutimiza wajibu wetu tutakuwa tunatekeleza ujumbe huu wa Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu
na haki yake na hivi vitu vingine vyote mtapewa kwa maelefu.
Tukitenda kila kitu kwa haki kamwe hatutakosa chochote
tunachohitaji unachohitaji ambacho kitakuwa ziada. Mwenyezi Mungu atakupa namna
yauta kila uchokihitaji zaidi.
Imani yangu ni kama ile ya Paulo kama tutatosheka na mishahara
yetu,na kuwajali wanyonge katika Kupata Riziki
zao, Na Mungu wangu atawajazeni na kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu. Hivyo tunawaomba watendaji wetu kutosheka na mishahra yao na hivyo kutawapa muda wa kulisaidia Taifa na kuacha kuhangaika na shughuli binafsi ambazo ziko nje ya maadili ya utumishi wao kwa msingi bora wa kimungu.

"Mungu hatakosa kuwajaza wale wote wanaoifanya kazi yake
sawasawa na mapenzi yake" hii ndio tafakari yetu ya leo -amina
No comments:
Post a Comment