February 3
Mungu alituumba katika
namna ambayo matendo yetu hufuata mawazo yetu; maisha ya mwanadamu yameoanishwa
na asili yake, au tabia ya mtu. Asili ya mwanadamu na maisha ni zao la yale yaliyomo
moyoni wake.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa mazingira tuishio ndio zao letu wanadamu;Mazingira huzalisha
watu wenye tabia zinazoshababiana; swali ambalo nataka tujiulize leo ni kuwa je
ni mazingira gani huzalisha watu wanyenyekevu;
au watu waliojaa tamaa za mali? Au kiburi?, maringo?, majivuno? na uzuri? Je ni
mazingira gani huzalisha watu ambao katika maisha yao huongozwa na Roho wa
Bwana waliojawa na hofu ya Mungu na upendo wa kweli?;
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa akili yetu ni kama shamba la mkulima. Kama mkulima akipanda
mbegu za mahindi atarajie kuvuna mahindi; Kama amepanda ngano atavuna ngano.
Itakuwa ni wazo la kufikirika na la kijinga kwa mkulima kupanda mahindi na
kisha kutarajia kuvuna ngano.
Tupandacho ndicho
tuvunacho; hivyo hata katika akili zetu jinsi tunavyozipanda tutegemee mavuno
sawa; Hivyo katika tafakari ya leo tujiulize je matendo yetu tunayopanda katika
mioyo yetu yatatuletea mazao gani mwishoni?
Kama ni kiongozi na
huwajibiki kulingana na sheria na utaratibu wa kazi yako, na mwisho wa siku
unategemea kuvuna mafanikio hizo zitakuwa ni ndoto. Haiwezekani kwa mtu yeyote
kwenda kupanda kwa maovu na wizi na ukatarajia mwisho wa siku uvune matunda
ambayo yatakupa Baraka za Mungu. Mungu amekupa uwezo wa kudhibiti unachopanda
na hivyo ni busara tuanze kudhibiti kile
ambacho tunachotarajia kuvuna.
Kama Warumi 8: 5-8.
"Kwa wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatayo
roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti bali nia ya roho
ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya mungu, kwa maana
haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili
hawawezikumpendeza mungu.
Tunanahitaji kuangalia na kutumia sheria ya akili yetu kuwa
kile ambacho tumeamrishi akili yetu ifuate ndicho hatimaye kitakuletea matokeo
yake mwisho. Haiwezekani kuweka mambo ya kidunia katika akili yetu na utegemee
matunda ya kiroho; kwani anasa na starehe za dunia hazichangamani na maisha ya
kiroho.
Tafakari ya leo
inatumbusha kuwa sisi binadamu tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kubadilisha
utendaji na mawazo ya akili zetu. Akili yetu iko sahihi kwani hutumwa kufanya
kazi, sisi ndio wenye maamuzi ya kufanya jambo njema au baya; Kama nabii Isaya
anayosema 55: 7, 8 Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo
yake. Na amrudie bwana, naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo
yenu wala njia zenu si njia zangu asema Bwana.
Kama tunaamua
kufuata njia ya kutenda haki haki basi akili yetu itekeleze mawazo ya haki.Ndio
maana njia za Mungu ni tofauti sana kuliko njia yetu ni kwa sababu mawazo yake
ni tofauti kuliko mawazo yetu mawazo yake daima hufikiria haki, upendo na
ukombozi wetu sisi binadamu baada ya kumwasi na kujaza akili zetu matendo
mabaya.
Tafakari ya leo
inatumbusha kuwa yale yanayoendelea katika vichwa vyetu ni hivi sasa ni muhimu
sana kwani yanaelekeza hatima ya maisha yetu. Hivyo ni vyema tudhibiti matendo yetu
kwa kudhibiti mawazo yetu. Ni vyema kuyatafakari na kuyaangalia mawazo yetu na hatimu yetu ya milele.
Tafakari ya leo inalenga
zaidi kutukumbusha kutaathimini mawazoyetu, amabayo mwisho yatakuwa maneno; tutafakari manenoyetu, mwisho
yatageuka kuwa matendo yetu; tuangalia matendo yetu, ambayo mwisho yatageuka kuwa
tabia zetu na tuangalia tabiazetu, ambazo mwisho zitakuwa hatima mwelekeo wa
maisha yetu ya Kiroho; Amina
No comments:
Post a Comment