February 1
Katika Tafakari yetu YA LEO tuanze Kwanza kwa kumshukuru Mungu kwa
Kutojalia kumaliza Mwezi wa January kwa usalama na kheri; Pili tuwaombee wale
wote kwa namna moja au nyingine ambao wako katika khali ngumu au wametangulia
mbele ya haki;
Je umeuanza mwezi February
kwa maswali kwa nini mimi? Kwa nini hiki kinatokea kwangu? Kwa nini
maisha ni magumu? Kwa nini naandamwa na ambo haya? Magojwa, kukosa pesa,
kutokuwa na maelewano mazuri ya kindoa; na kadhalika.
Tukisoma 2 Corinthians 1:1-11 mtume Paulo anatukumbusha
kuwa daima maisha yetu yamejaa masononeko, malalamiko, malinganisho; anasema
lakini nachelea; kama Yule nyoka alinyomdanganya hawa kwa hila yake, asije
kuwaharibu fikra zenu, mkauaacha unyofu na usafi wa kristo. Mtume Paulo
anatusahauri kuwa katika khali kama hii bado tumtumaini Kristo kuwa ndiye pekee
anaweza wajibu maswali haya yote magumu.
Ni kweli katika wakati kama
huu tunajiuliza maswali mengi yuko wapi Mungu wangu na kwa nini ananipa mimi
wakati mgumu kiasi hiki? Kama wafuasi wa Kristo imara hatutakiwi kuwa na
mashaka tunalotakiwa kulifanya ni kuendelea kuomba neema ya Mungu ambayo iko
juu ya kila kitu na ambayo ndio pekee katika ushindi wetu wa ugumu wa maisha
yetu;
Na tukumbuke kuwa
ugumu ambao tunaouona katika kila jambo ndani ya maisha yetu sio kwa sababu ya
ugumu bali ni jinsi sisi tunavyo ukabiri ugumu huo. Je tunapokabiriwa na ugumu
wa maisha kama magonjwa, khali ngumu ya kiuchumi, magomvi miongoni mwetu;
Je hatua yetu ya kwanza
katika kutatua tatizo hilo inakuwaje? Namna ambayo tutakayo ichukua katika kutatua
tatizo hilo ndio itakuwa suluhisho sahihi. Mara nyingi tunakimbilia kujihukumu
kwa nini hii imetokea kwangu? Lakini njia sahihi ilitakiwa tujiulize hapa ninajifunza
nini? Ni wapi nimekosea mpaka nimefikia hapa nilipofikia? Je uchaguzi wa njia
ya kutatua tatizo hili kwa mara ya kwanza ulikuwa sahihi? Je niliomba mwongozo
wa Mungu kabla ya kufanya uamuzi huu? Tunajua Mungu anaruhusu ugumu wowote kutokea
katika maisha yetu ikiwa ni njia ya kujifunza na vile vile ili uwe ni fundisho
kwa siku zijazo; au matayarisho ya jambo
kubwa zaidi mbele ya maisha yetu;
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa tujitambue kuwa sisi katika ugumu wowote ule sio waathirika
(victim); na hivyo Mungu anatuadhibu la hasha daima Mungu yuko nasi na wakati mwingine anaruhusu vile vile ugumu
katika maisha yetu ili kutusaidia sisi kutembea
katika njia sahii kufikia mahitaji yetu;
Mtume Paulo kwa Warumi 8:28 anatukumbusha kuwa
nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale
wampendao katika kumpatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Hivyo hata
katika ugumu wa maisha yetu lazima tuendelee kuamini kuwa Mungu yuko kazini kwa
faida yetu;
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa daima tumpe sifa Mungu kwani ni yeye pekee ambaye ni
kitulizo katika shida zetu; ni yeye pekee hututuliza katika magonjwa yetu
tukiwa wagonjwa au pale mpendwa etu anapokabiliwa na tatizo kama hili;
Tukumbuke kuwa zaburi ya 23 inavyosema;
bwana ndiye mchungaji wangu na sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani
mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu;
na kuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam nijapopita kati
ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja name,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Hivyo tukumbuke kuwa
matatizo yetu au ugumu wa maisha unaotukabili unaweza kuwa ni Baraka kutoka kwa
Mungu sio tu kwako na kwa wengine ambao wanaweza kujifunza kwa faida kubwa
mbeleni.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa katika ugumu wa maisha yetu kuna mwingine ambaye
anatuangalia na kutubariki na sio mwingine bali na Mungu Kupitia Bwana wetu
Yesu Kristo.
Hivyo tunavyokuwa
katika wakati mgumu tunatakiwa tujifunze kuwa tumwamini Mungu; tuangalie
matendo makubwa ya yesu Kristo kama alivyowafufu wafu; Je atashhindwa kutatua
ugumu ulio nao katika maisha yako? Upeo wetu wa kutatua ugumu wa maisha yetu
unakikomo lakini kwa Mungu na Mkombozi wetu Yesu hakuna kikomo; utendaji wao ni
wa milele yote;
Tumeagizwa jambo moja
katika kutatua shida za ugumu wowote unaotukabili ni kwa kusali bila kukoma au
kuchoka; tunatakiwa kuwa na imani tuombapo; nah ii ni tafakari yetu ya leo.
Amina
No comments:
Post a Comment