February 22
Leo tuungane na Mtumishi wa Mungu Dr. Aba Mpesha ambaye
anatuletea tafakari ya leo tukiwa tunatimiza sikuya 12 ya Kwaresma: Heri wenye Upole maana hao
watairithi nchi (Matayo 5:5)
Nilipofikiria mstari huu, swali lililonijia ni hili: Nani
anaweza kukana haki zake zote kwa ajili ya Yesu Kristo? Nilipochunguza na
kutafakari vizuri zaidi, niligundua upole aliouzungumza Yesu katika
mstari huu alimaanisha yafuatayo:
1. Mtu
akidharauliwa ananyamaza.
2. Mtu
akifanyiwa fujo, anastahimili.
3. Mtu
akikataliwa anakubali.
4. Mtu
ambaye hatashtaki ili apate haki yake.
5. Mtu
asiyepiga kelele akinyimwa haki yake.
Ni yule asiyetaka haki kwa ajili yake mwenyewe, bali anataka
haki kwa ajili ya wengine – mara nyingi anataka haki kwa ajili ya wanyonge,
walala hoi, wajane, maskini, wasiojiweza, watoto, viwete, na watu kama hao.
Katika tafakari hii nimejiuliza swali hili:
Je watu ninaokutana nao na wakasikia maneno au kuona matando
yangu, wanamwone Yesu?
Nilisita kutoa jibu kwa sababu upande wangu lilkuwa ni la!
Ndipo nikamlilia Yesu na nikamwomba, Bwana Yesu niumbie
UPOLE ili niweze kuirithi nchi.
Hii ndio tafakari yetu ya
leo, Amina
No comments:
Post a Comment