February
2
Tafakari
ya leo tunakumbushwa kujitambua na kuona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kujiwekea Mkakati binafsi katika
ukuaji wa kiroho. Ukuaji wa kiroho ni njia pekee ambayo inatunganisha
sisi binadamu na Mungu: pamoja na kupotea kwetu katika safari hii ya Kiroho
bado Mwenyezi Mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo anatumia mambo mawili katika
maisha yetu ya kutusaidia kurudi kwenye njia sahihi; ni kupitia neno lake na
kwa sisi wenyewe kundelea kuomba na kushukuru.
Tafakari
ya leo inatukumbusha kuwa Mungu anazungumza nasi kupitia Neno lake na sisi
kujibu kwa maombi. Tukitekeleza hilo ukuaji wetu wa kiroho huleta maana; Yesu alisema kwamba kama
tunampenda wajibu wetu kushika amri zake. sisi ni wafuasi Kristo moja ya wajibu wetu mkubwa ni kuendelea kumtafuta na kutii maelekezo yake.
Tunaonywa kuwa ili tufanikiwe kukua kiroho
tunatakiwa kuwa msatari wa mbele katika kuonyesha upendo wa Kuwahudumia
wengine na kuondokana na dhana ya ubinafsi ambao ndio hulka kubwa kwetu.
Tunajua kuwa Mwenyezi Mungu ana majukumu katika mchakatowa mabadiliko ya maisha
yetu, lakini anataka yaanzie kwetu. Na tukumbuke kuwa ni wajibu wetu sisi
kushirikiana na Mungu Yeye daima hufanya kazi ndani yetu. Tukisoma kitabu
cha waefeso 2:10 Kwa maana sisi tu viumbe vyake - tuliumbwa katika Kristo Yesu
tutende matendo mema; na tukumbuke Mungu hufanya kazi ndani yetu kupitia sisi
wenyewe.
Neno la Mungu heleta mabadiliko makubwa ya
kiroho ndani yetu; tunapompokea Roho mtakatifu na kuamini katika uwepo wake
ndani ya nafsi zetu ndipo safari ya kiroho inapoanza na kutujengea maisha
bora kabisa ya kiroho. Ukimpokea roho wa kweli huleta mageuzi ndani ya ya
maisha yetu. Tunakuwa tayari katika hatua za kutimiza wajibu wetu wa kumwambia
Mungu tuko tayari kwa maisha mapya ya ukuaji wa kiroho; hivyo Mungu huanza kazi
yake ndani yetu ambayo inaamsha mabadiliko ya maisha yetu.
Tukumbuke kuwa Yesu alipopaa Mbinguni
aliwaambia wanafunzi wake nitawaletea msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu
hutupa sisi; nguvu , hubadilisha mfumo mbaya wa maisha yetu; Roho
wa Bwana hukaa mahali pasafi na penye neema ya Kimungu. Hivyo Roho wa Mungu
husaidia kubadilisha mazingira yetu mabaya yaliyojaa dhami kwani uwepo wa
Mungu ndani yetu hudhiirisha usafi wa mazingira yetu;
Mtume Paulo anatukumsha kuwa wokovu Ni
zawadi ya bure ni neema ya Mungu ambayo lazima ianzie kwetu. Kwa kweli
tunatakiwa kuishi maisha kama Kristo: Yatupasa kusali bila kuchoka, na
kushukuru kwa kila jambo; kwa kufanya hivi ukuaji wa kiroho utaweza kukamilika
ndani yetu;
Tunatakiwa kudumu katika maombi; walipo
wawili au watatu wakisali pamoja nami nitakuwa katikati yao; hivyo inatupasa
kujiepusha na upweke, na tudumu katika ibada, kutoa fungu la kumi,
kuwahudumia wahitaji wagonjwa, wajane na wenye shida mbalimbali na kuwa mtu
mwaminifu. Sisi kama wanafunzi wa Yesu; yeye alitimiza wajibu wake kama mwalimu
kwa kuwasilisha ukweli kuhusu Mungu; wajibu mwanafunzi kuwa tayari na kukubali
kujifunza na kuwajibika ili kupata elimu anayohitaji kwa hiyari yake.
Mtume Paulo, anatukumbusha kuwa katika
mpango wa kukua kiroho tunatakiwa tutazame mambo yaliyo mbele yetu na kukaza
mwendo kufikia yaliyo bora katika kufikia hatua ya mwisho ya wokovu
ambayo ni zawadi ya pekee ambayo Mungu ametutayarishia mbinguni kupitia Mwokozi
wetu Kristo Yesu.
Hii ni tafakari ya leo amina
No comments:
Post a Comment