February 11
Tafakari ya leo itukumbushe kuwa kwa hakika mwanandamu anahitaji
upeo mkubwa wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia
zote za kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na
hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la
msamaha. Kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa
ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi
kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau, kukudhalilisha na
kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu ambao wanaielewa
sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii.
Kumsamehe
yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile
vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe
tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini pasipo
imani haiwezekani (Waebrania 11:6). Inatufundisha kuwa mtu amwendeaye Mungu lazima
aamini kwamba yeye
yuko, na kwamba
huwapa thawabu wale wamtafutao,”.
Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na Mungu katika Imani.
Kama ilivyoandikwa hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na
anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeelezwa katika Zaburi 86:5
"Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili
kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi tumaini lake la msamaha?
Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi
cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo
6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni
atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu
hatawasamehe makosa yenu." Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso
4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi
mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."
Kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa.
imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana
ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia
sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu
ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14
inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na
kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe
makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake
iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami
nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia
furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi
zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho
iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu
usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya
wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri
aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia
upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa
kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako
ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi
nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari
maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu
mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia
yeye."
Wale walio wanyonge moyo wako mbele ya
Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika.
Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na
misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile,
kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili,
uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika
dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba
asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi
kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya
wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa
ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo
uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole,
uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia
ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha
mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana
asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na
uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga
chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa
Mungu ni; katika imani jambo ni rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia
kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu
wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli
pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule
aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu
na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu
katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na
kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na
ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili
kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hebu jitafakari kwa nini umekuwa na
kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao
wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je
wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule?
Hii ni Tafakari ya leo Amina
No comments:
Post a Comment