Katika
Tafakari ya leo tunaendelea kuungana na Mtumishi wa Mungu Dr. Aba Mpesha Ambaye
anatukumbusha umuhimu wa kudumisha amani katika maisha yetu ya kila siku;
Tafakari
ya Heri wenye Upole inanikumbusha
maneno ya Bwana Yesu kuhusu AMANI. Yesu alisema: “Heri wenye kuleta amani, maana
wataitwa watoto wa Mungu (Matayo
5:9).
Ukitafakari
kwa kina, wito wa Yesu kwa wafuasi wake ni kueneza Amani. Wote walioitwa
na Yesu, walikutana na Amani – Yesu ambaye ni mfalme wa Amani. Kwa hiyo, Yesu ndiyo Amani yao.
Kusema
kweli, wafuasi wa Yesu hawakuiitwa kuwa na Amani tu, pia walipaswa kuleta
Amani. Wangeitwa kuwa na Amani bila kupata agizo la kuleta Amani, wangekuwa
watu wa ubinafsi. Kwa sababu hawakuitwa wawe na ubinafsi, waliagizwa kukana
vurugu na malumbano. Vurugu na malumbano havisaidii kutimiza lengo ya Yesu la
kuleta Amani. Ufalme wa Yesu ni wa Amani tele. Ndiyo maana wote walio kwenye
jumuiya ya Yesu Kristo husalimiana na busu la Amani.
Wanafunzi
wa Yesu malisisitiza kudumisha Amani kwa kuchagua kuteseka badala ya kufanya
wangine wateseke. Hata Petro alijifunza hilo kutoka kwa Yesu usiku ule Yesu
alivyokamatwa, Petro katika kumtetea Yesu, alimkata sikio mtumishi wa kuhani
mkuu. Ebu sikiliza Yesu alisemaje. “Rudisha upanga wako mahali pake, maana
wote waushikao upanga, wataangamizwa kwa upanga.” (Matayo26:52).
Ni
kweli wafuasi wa Yesu wanapaswa kuhifadhi jamii, wakati dunia inavunja jamii.
Wanapaswa kukana kujitutumua binafsi na kukaa kimya wakikumbana na chuki na
dhuluma.
Ni
kwa njia hii wafuasi wa Yesu ushinda uovu na wema.
Ebu jiulize, jamii yetu ambayo imelea utamaduni wa
vurugu na malumbano, ingekuwaje kama watu wote wangekana vurugu na malumbano,
na badala yake wakatekeleza utamaduni wa Amani. Ni kweli tutaitwa watoto wa
Mungu na kuirithi nchi tuliyopewa na Mungu, kwa sababu Amani itatawala.
NAAMINI HII
NI DUNIA TUNAYOILILIA.
BASI
TUMWOMBE MUNGU ATUPATIE SHAUKU YA KUTAKA KULETA AMANI HAPA DUNIANI, NDIPO
TUTAITWA WATOTO WA MUNGU. Hii ni tafakari ya leo toka kwa mtumishi Aba
Mpesha.
No comments:
Post a Comment