February
10,
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa asili ya binadamu ni vumbi , tuliumbwa kwa udongo na
tukapewa neema ya mwili wa utukufu, lakini tukaukana utukufu huo kwa dhambi ya
kutosikiliza maagizo ya Bwana; kutokana na dhambi hii basi kwa udongo tutarudi
mwisho wa maisha yetu hapa dunia. Zaburi ya 49:11 itatueleza kuwa Makaburi ni
nyumba zao hata milele; maskani zao vizazi hata vizazi; hao waliotaja mashamba
yao kwa majina yao wenyewe. Mwanzo 3:19 kinatukumbusha kuwa kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata
utakapoirudia ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi
wewe,nawe mavumbini utarudi.
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuanza kwa kipindi cha mfungo wa siku arobaini katika kipindi
hiki cha Lent;
Lengo kubwa la mfungo huu ni kujitathimini sisi wenyewe wafuasi wa
Kristo na kuona je njia zetu za kila siku katika maisha yetu zinampendeza
Bwana; Kama sivyo basi tunatatkiwa kutubu; hii taathimini inatutaka kuwa
waaminifu na matendo yetu katika maisha yetu, Je matendo yetu ni yale ambayo
yanatakiwa mbele ya Mungu? Na kama sivyo je toba yangu itanisaidia mimi
kuondoka katika njia hizi mbaya?
Hiki ni kipindi ambacho
tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi pekeyetu na Mungu, ni wakati wa kufunga na
kujinyima kwa kweli kwa faida ya uokovu war oho zetu; ni kipindi ambacho
tunatakiwa kitabu cha Mathayo 6:20-21
anapotukumbusha kuwa msijiwekee hazina
duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni
hazina mbinguni kusikoharibika kitu hakuna nondo wala kutu, wala wevi hawavunji
wala hawaibi. Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakuwapo na moyo wako.
Tafakari ya leo inatukumbusha
kuwa tunapojitathimini wenyewe tukumbuke kuwa sisi ni wadhaifu ambao tunahitaji
msaada, na sio watu wenye afya njema ambao hawaitaji matibabu. Tu wadhaifu
hivyo tunaomba huruma ya Yesu katika kipindi hiki cha toba kwani tumekwenda
kinyume na sheria za bwana na Bwana wetu Yesu Kristo yuko tayari kutusikiliza
na kutusaidia. Lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa sisi ni mavumbi na tutarudi
mavumbini, hata kama wakati mwingine kutokana na mafanikio yetu hatuko tayari
kukubali ukweli huu lakini ni ukweli usiopingika kuwa maisha ni zawadi ambayo
tumepewa na Mwenyezi Mungu, hivyo hatutakiwi kuichukulia kama haki yetu. Hivyo tunakila
sababu ya kufunga na kutubu dhambi zetu katika kipindi hiki cha Kwaresima; ni
wakati mzuri wa kujichunguza ni kipindi ambacho tunatakiwa tumpe Mungu mioyo
yetu ili aweze kuichunguza ili kupitia microscope (darubini) yake aweze
kuisafisha na kuondoa wadudu wote wabaya wanaoharibu maisha yetu kwa maagizo
yake kupitia Bibilia.
Tafakari ya leo inatupa
wakati mzuri wa kutafakari kitabu cha Yoshua 1: 8 aliposema Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani
mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia
kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Ni kweli ni wakati
mzuri wa kutafakari maagizo ya Mungu ili kupata kibali cha maisha ya utukufu
ambao tumeandaliwa katika maisha yetu ya baadae.
Tukisoma kitabu cha Mathayo
6:16-18 tunataadhalishwa kuwa tunatakiwa kuwa wanyenyekevu wakti huu wa mfungo;
Basi mfungapo, msiwe kama wanafiki wenyeuso wa kukunjamana; maana
hujiumbuanyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Aminnawaambia,
wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo,jipake mafuta kichwani, unawe
uso; ili usionekane na watu kuwa umefunga, ila na Baba yako aliye sirini, na
Baba yako aonaye sirini atakujazia. Tunatakiwa kuwa makini na kuepuka tabia za
kiunafiki katika kipindi hiki, kiwe kweli ni kipindi cha Toba na kumrudia
Mungu. Mithali 2:1-5 Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba
maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako
upate kufahamu; naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;ukiutafuta
kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu
kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu
Tafakari ya leo inatukumbusha
kuwa tunatakiwa kuuitafuta na kuisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako,
na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na
kuzishika amri zake, Tumshukuru Mungu kwa ushindi amboa uko mbele yetu kupitia
Mkombozi wetu Yesu kristo. Hiki ni kipindi cha kusafisha hekalu letu, tukumbuke
kuwa mwili wetu ndio hekalu la kudumu la Mungu. Hivyo tuna kila sababu ya
kuhakikisha kuwa linakuwa safi muda wote na kufuata maelekezo ya Mungu katika
utimilifu wake. Nawatakieni Jumatano ya Majivu Njema iliyojaa Toba ya kweli
mbele ya Mungu wetu Amina.
No comments:
Post a Comment