February 19
Tafakari ya leo
tuangalie agizo la Mungu kwa wana wa Israeli wakati wa uongozi wa Nabii Joshua:
Mungu alimwagiza Joshua kwa kuwaambia kuwa Joshua 1:8 kitabu hiki
cha Torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,
upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Huu ni ujumbe mzuri
katika tafakari yetu ya leo; kwani maagizo haya yanatufundisha kuwa jukumu letu
ni kutekeleza maelekezo ya Mungu na kwa kufanya hivyo Mwenyezi Mungu wetu atakuwa yuko juu ya maisha yetu. Tukitafakari na kufuata mwongozo kupitia nukuu hii ni wazi
kuwa tutapatiwa chochote tunachohitaji, iwe utajiri, mafanikio katika maisha
yetu, ndani ya familia zetu, sehemu zetu za kazi na ndani ya jumuia zetu.
Lakini tunakazi
kubwa ya kufanya ili kufikia mafanikio haya ukumu letu kubwa ni kusoma kuelewa
na kutafakari neno mungu na kisha kuishi kulingana na neno hilo siku zote za
maisha yetu; sio jambo la mara moja. Tafakari ya leo inataka sisi tujenge
mazoea ya kulitafakari neno na sheria za mungu siku zote za maisha yetu.
Ni ukweli amabo pengine
hatuuelewi kuwa Mungu hajetuahidi sisi kuwa atatupa busara, lakini anajua kama
tutasoma na kuelewa yaliyoandikwa na kuagizwa katika kitabu cha torati tutaweza
kuishi na kufanya mambo yetu au maamuzi yetu kwa busara kubwa sana.
Tujue kuwa neno
lisiondoke kinywani mwetu linatufanya sisi kuwa karibu sana na Yesu. Na agizo
hili litakuwa ni chachu ya sisi kujua kuhusu ukweli wa Mungu na miujiza yake
kwetu, na ukweli ambao hatuwezi kuujua kuhusu yeye kama hatutakuwa tayari kusoma
na kuelewa na kutafakari kitabu hiki.
Je sisi wafuasi wa Kristo tunatimiza wajibu
wetu kulingana na kitabu cha Torati? Tu wakweli kwa kiasi gani? Wawajibikaji kwa
kiasi gani, tunazingatia sheria za Mungu na za nchi kwa kiasi gani? Je
tunakumbuka ahadi ya Mungu kuwa tukitimiza ahadi zake tutapata neema ndani ya
maisha yetu; siri kuwa ya mafanikio kulingana na kitabu hiki cha Torati ni
UTII: Tukumbuke kuwa utii huleta amani, utii ni ufunguo pekee ambao Mwenyezi Mungu Kupitia Bwana wetu Yesu Kristo ametufungua milango yote ya baraka kwetu. Je tunatumia funguo hii ipasanyo?
Tafakari ya leo inatuonyesha kuwa tunashindwa
sana kutimiza maelekezo ya Mungu kuhusu utii na kutufanya tukose baraka nyingi
sana. Je wewe na mimi utii wetu kwa Mungu uko kwa kiwango gani? Maagizo ambayo
Mungu alimpa Joshua yanatusaidiaje sisi leo?
Je tunatafakari neno la Mungu Mchana
na Usiku? Au maisha yetu ya kila siku yamechukua nafasi ya kwanza ndani ya maisha hivyo hatuna muda kabisa wa muda wa kutafakari Torati ya Mungu kwa dhati kabisa?
Kama tunafanya hivyo bado tunaendekeza kiburi chetu ndani ya mioyo yetu
jambo ambalo Mwenyezi Mungu alipendi sisi tufanye. Ondoa kiburi chako na tuanze kutafakari neno
la Mungu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo; Amina
No comments:
Post a Comment