February 4
Tafakari ya leo hebu
tuangalia umuhimu wa kutumia mdomo vizuri ili uwe nuru kwa mataifa.
Tunakumbushwa kuwa wakati wa kufungua mdomo na kuanza kufanya mawasiliano
tunashauriwa tuutumie mdomo wetu kwa faida ya wote na kuondoa mashaka ambayo
yanasababishwa na Mdomo. Kitabu cha Zaburi 19:14 kinasema Maneno ya kichwa change,
na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na
mwokozi wangu.
Tafakari ya leo inatuasa mdomo
hufanya mambo kadhaa kutengeneza maneno na mawazo kulingana na mazingira ya
moyo kutafakari maneno hayo kabla ya kufanya hatua ya mwisho ya kuyatoa kwa
kusema kwa mtu mmoja na kikundi cha watu ili kufikisha ujumbe kutoka ndani ya
nafsi yako; hivyo kwa kumsikiliza mwongeaji hivyo unaweza kujua kabisa; kuwa
anaongea kutoka katika mazingira gani;
Leo tunashauriwa kuwa wakati
mwingine ni bora kufunga mdomo wako na kuonekana kama ni mjinga, kuliko kusema
kitu cha kijinga na kisha watu wakajidhihirisaha kuwa kwa kupitia mdomo wako
umeonekana kweli ni mjinga. Au wewe ni katili au wewe sio mtu ambaye unahofu na
Mungu.
Kupitia mdomo wako unaweza
kukufundisha unyenyekevu wa kufikiri na kuongea pale tu panapopaswa kuongea au
kushauri kitu ambacho unakifahamu na unauhakika nacho. Mdomo wenye kheri huwa
na subira, na utafakari kabla ya kusema; na unakufundisha kukubali kwamba hujui
kitu, na kutumia mdomo wako kujifunza
kwa kuuliza maswali na kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Tukisoma 1 Peter 3:10 kwa
maana, atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene
mabaya, Na midomo yake isiseme hila.
Kwa Msingi huu ukiwa na
mdomo wenye unyenyekevu; mdomo wako unakuwa na subira na unakubali kuwa haujui
kila kitu; na kukubali kuwa wakati mwingine unakuwa mjinga mwerevu anayekuwa
tayari kujifunza kupitia mdomo na hatimaye kuwa nuru kwa mataifa;
Je umewaona wale ambao hujifanya kujua kila kitu kupitia midomo yao
na kuwapotosha wengine? Ni bora kujua kidogo na kuwa nuru ya mataifa kuliko
mdomo wako kuwa na ujuwaji mwingi na kuwaangamiza walio wengi.
Marko 7:20-23
anatukumbusha kuwa kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya
mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati. Wivi, uuaji, uzinzi, tama mbaya,
ukorofis, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi upumbavu. Haya yote yaliyo
maovu yatoka ndani ya moyo na kutekelezwa kwa mdomo.
Tafakari ya leo
inatukumbusha ushawishi wa mdomo uwe kwa ajili ya nuru ya mataifa na sio kuwa sababu
ya maangamizo ya mataifa. Mdomo hutengeneza maneno, na maneno haya yawe ni nuru
kwa mataifa. Mdomo wako usitumike katika kuwahukumu wengine. Mdomo wako uwe ni
hakimu wa haki; mdomo wako uwe ni kioo cha haki; mdomo wako utangaze amani,
upendo na sio kuwa daraja la chuki au utengano au mafarakano; Mdomo wako usiwe
daraja la rushwa, wizi au ufisadi; mdomo
wako usiwe ni sababu ya udikteta na ukandamizaji; Je mdomo wako uko katika
ngazi gani?
Tafakari ya leo
inatukumbusha kuwa lazima tujenge hofu ya Mungu kupitia midomo yetu; zaburi ya
50: 19,20 umekiachia kinywa chako kinene mabaya, na ulimi wako watunga hila. Umekaa
na kumsengenya ndugu yako, na mwana wa mama yako umemsingizia. Hili ndilo
tatizo ambalo tunalo na ni kubwa kwa jamii yetu sasa. Tumekuwa sio watu ambao
ni wakweli katika kutimiza wajibu wetu; tunatumia nguvu nyingi kupitia midomo
yetu katika kumtia hatiani mtu mwenye haki ili tu tufurahia starehe fupi katika
ulimwengu huu. 2 wakorinto 13:5.
Tafakari ya leo inamaliza
kwa kusisitiza kuwa mdomo ukitumika vizuri una nguvu ya kuponya, kubariki,
kukwemea maovu, mapepo; kuleta Baraka; kwani kwa neno tu Mungu aliumba
ulimwengu huu, Tukijikumbusha Kitabu cha Mwanzo 1:3 Mungu alisema, Iwe nuru;
ikawa Nuru. Na tunatumia midomo yetu kuomba msamaha kwa Mungu- hivyo MDOMO WAKO UWE NI NURU YA MATAIFA – AMINA.
No comments:
Post a Comment