Kuna wimbo mmoja wa zamani ambao una maneno
haya namjua anayeishikilia kesho na anayeshikilia mikono yangu. Tunatakiwa
tujiulize swali moja kama hatuna mamlaka na kesho kwanini bado tunaendelea
kupanga kuhusu maisha yetu ya kesho? Mungu ndiye anayeendesha maisha yetu na
hatima yetu ya kesho na anajua kesho yetu itakuwaje la msingi sifa na utukufu
uwe juu yake
Hata viongozi wa siasa pamoja na jitiada zao
za kuongoza nchi bado hawana mamlaka na nguvu ya kuiona au kuishi kesho;
mipango yetu yote inaishia leo, hivyo kesho yetu ni kwa kudra ya Mwenyezi
Mungu. Hivyo hakuna kiongozi yeyote zaidi ya Mungu ambaye ndiye anayeijua hatima
yetu ya kesho.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa sisi ni
wanadamu tunaoishi leo huo ndio ukweli mtupu tupende kuamini au kuwa na kiburi
cha kutoamini hivyo.
Mwenyezi mungu anajetoa ahadi kwetu kuhusu
kesho; kama mwenjili Mathayo 6:34 anavyosema basi msisumbukie kesho kwa kuwa
kesho itaisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Au tukisoma kitabu cha
Yakobo 4: 13-16 haya basi ninyi msemao leo au kesho tutaingia katika mji Fulani
na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida: walakini hamjui
yatayo kuwa kesho. Uzima wenu ni ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa
kitambo kasha kutoweka. Baada ya kusema Bwana akipenda tutakuwa hai na kufanya
hivi na hivi. Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisisfu kotekwa
namna hii ni kubaya.
Tafakari ya
leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kumtamamini mungu zaidi katika kila jambo
tulifanyalo kwani katika mikono yake ndipo neema yote ya maisha yetu imo. Hivyo
ni Mungu tu ambaye anajua na anamiliki kesho yetu; ndio maana hatujui hata
mbingu inafanana vipi, kwani kesho yetu imejaa utukufu wa ajabu na amani ya
kweli sio kama leo yetu ambayo tunaishi iliyojaa kila aina ya tabu na uozo.
Lakini kesho yetu
ili iweze kuwa katika mikono yetu lazima tujijengea tabia ya kuwa na imani
dhabiti. Kwani kwa imani tunakuwa na hakika ya mambo ambayo hayaonekani lakini
yanatarajiwa nasi. Na kuwa na imani ni kinyume cha kuwa na woga. Je tunawoga
kuhusu kesho? Tujikumbushe kuwa kuwa ukiwa mwoga katika maamuzi yako na katika
maisha yako ni wazi kuwa huna imani na Mungu hutegemea sana dunia hii.
Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa kama hujui kesho yako wewe mwamini Mungu yeye ndio mwenye haki miliki ya kesho. Tuondoe wasiwasi na kujihakijishia kuwa Mungu atandenda yote kwa ajili yetu; ni muhimi kwetu kutekeleza majukumu yetu nay eye atafany sehemu yake;
Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa kama hujui kesho yako wewe mwamini Mungu yeye ndio mwenye haki miliki ya kesho. Tuondoe wasiwasi na kujihakijishia kuwa Mungu atandenda yote kwa ajili yetu; ni muhimi kwetu kutekeleza majukumu yetu nay eye atafany sehemu yake;
Tukumbuke kuwa tunatakiwa
kumwamini na kufuata maelekezo ya Mungu ili tuweze fanikiwa ili kuweza kuifikia
kesho , na njia pekee ni kwa maombi sala ni salaha pekee ambayo itatufungulia
njia ili tuweze ifikia kesho yetu. Tukisoma 1 Wathesalonike 5: 17-18 ombeni
bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu
katika kristo yesu.
Tafakari yetu ya
leo inatukumbusha maneno yaliyoandikwa na Mwenjili Mathayo 6: 33 -34 Basi
utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi
msisumbuke kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Hivyo wapendwa
hatuna sababu ya kuhofu kuhusu kesho kama tumejikabidhi wenyewe katika mikono
ya Mungu. Hatuna sababu ya kuhofu kwani tunajua kuwa Mungu ndio tegemeo letu na
yeye peke yake ndio mwenye hati miliki ya kesho yetu. Amen
No comments:
Post a Comment