AUGUST 14
ZAWADI
AMBAYO KILA MTU ANAHITAJI KATIKA MAISHA;
2 Timothy 3:1–5
Tafakari
yetu leo inatukumbusha kuwa kila mtu anahitaji zawadi iliyo bora kabisa katika
maisha yake; ni kila mtu anahitaji zawadi kubwa ya maisha ambayo ni upendo;
ukiwa na upendo kwa kweli familia zetu au jumuia zetu zitakuwaje? Je myumba
zetu zitakuwaje? Je ofisi zetu zitakuwaje? Je shule zetu zitakuwaje? Natumaini
kama tutakuwa katika maisha ya upendo hakika tutakuwa katika ni kisima cha
ajabu chenye upendo mkubwa Galatians 6:10 . Kwa hiyo
kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio
Itakuwa ni rahisi kujiuliza swali hili je leo nani atakuwa mbarikiwa
kwani daima akili yetu itakuwa ikiangalia upande mzuri wa maisha yetu na sio
upande mbaya: 2 Timothy 3:1–5 Lakini ufahamu neno
hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye
kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi
wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu,
wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa
kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake;
hao nao ujiepushe nao.
Tafakari
yetu inatuonya kuwa Kunyume cha upendo ni uangamizi kwani kila mtu atakuwa
kweney harakati; na akiyatizama maisha yake pekee yake watakuwa wakijisifu
katika mafanikio ambayo hayajali maisha ya watu wengine. Daima tunajisahau na
kujiona kuwa wafalme katika mafanikio yetu; na kwa msingi huo tunakuwa hatuna
muda wa kuonyesha upendo kwa wengine; lakini tukumbuke kuwa kamwe hatujeumbwa
kuishi kwa ukabaila na uchoyo; ni wajibu wetu kufanya jambo lolote amablo
litaonekana tofauti kwa wengine. Siri ya Mungu kwetu ni hii kamwe hatutakuwa
tumeishi maisha ya kumpendeza Mungu kama hutafanya jambo njema kwa wenzetu bila
kujihatijika wao kurudisha fadhila. Je umeshaona jinsi marafiki wanavyoishi kwa
kuumizana? Ukiwa bizi sana huwezi kuliona hili mpaka pale utakapo tuo
ushirikiano na kujifunza kwa watu wengine kwa kuona shida zao; Mathayo 25:40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia,
kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea
mimi. Methali 19:17 Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa
tendo lake jema.
Tafakaria
yetu ina tuuliza kuwa; Je wewe umefanya tofauti gani leo? Kwa mjane? Kwa mototo
yatima; kwa mzee au masikini ambaye anahitaji huruma ya Mungu kupitia kwako?
Tunapofanya wema kwa wenzetu tunawajengea taswira ya ajabu katika mioyo yao na
wanamwona Mungu katika maisha yao kupitia kwetu: je uko tayari kuwa sehemu ya
utukufu wa Mungu kwa kuwasaidia wahitaji wa kweli leo? Kama mtoto mmoja
alivyomuuliza Mama mmoja ambaye alimnunulia pea tatu za viatu ambavyo alikuwa
akivitamani sana kuwa je wewe ni Mke wa Mungu? Katika taswira yake anajua wema
unatoka kwa Mung tu? Je wewe uko tayari kufanya wema ili utukufu wa Mungu ungae
katika maisha yako? Kutoa kwa moyo ni hadhina pekee unayojijegea mbele ya
Mungu. Yatupasa kujifunza kuwa watu wa kutoa na kuwa mwema katika maisha ya
watu wengine; Yatupasa kuonyesha maisha yetu mema kila wakati na kila mahali
tunapokwenda;
Tafkari
yetu leo inaendelea kusisitiza kuwa Upendo lazima uonekane katika maisha yetu
kwa vitendo; kupitia muda wako, uwezo wako wa kifedha hata kwa maneno
mazuri ya kuhamasisha kwa kufanaya hivyo tunamkaribisha Mungu katika maisha
yetu ya kila siku; wakati mwingine tunakatishwa tamaa pale ambapo unatoa msaada
wa wenzetu lakini wahusika wakisha pata msaada yaani wanakuwa hawana muda wa
kusema asante, la msingi uelewe kuwa mungu daima anaweka kumbukumbu katika kila
jambo njema ambalo tunalifanya hivyo hatunasababu ya kusubiri asante ya
kibinadamu waajibu wetu yatupas kushukuru kwani Mungu yeye ndiye atakaye
kurudishia wewe mara elfu elfu kwa wema wako. Jicho la mungu ni la ajabu
linaona kila kitu tufanyacho. Mbegu iliyo bora hupandwa kwenye udongo mzuri na
udongo mzuri hutoka kwa mungu. Sikila shida za watu nawe uwe utabarikiwa kwa
msaada wako kwao kwani wao hawana uwezo mwenyezi Mungu atakubariki kwa
upendo wako;
Tafakari
yetu leo inatukumbusha kuwa pendo la kweli lazima lionyeshwe kwa matendo yetu,
tukumbuka kuwa watu wanatuangalia sisi, tukumbuke kuwa kadiri tunavyowasaidia
wengine ndivyo hivyo Mungu atakavyo turudishia na kutusaidia kwa kadiri ya
mahitaji yetu; Mungu atakuzidisha mara elfu elfu lakini lazima utambulike
kwa matunda ambayo umeyapanda na
yameleta furaha na amani kwa wengine; Mathayo 7:16–20. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika
miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri;
na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti
mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa
motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
Tafakari yetu inasisitiza
kuwa ili kuweza kutekeleza utumishi ulio
tukuka lazima atimize wajibu wake wa kujijenmgea msingi ulio bora Mathayo 7: 24-27
Basi kila asikiaye hayo maneno
yangu, na uyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake
juu ya mwamba; mvua ikanyesha,
mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana
misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
Na kila asikiaye hayo maneno
yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya
mchanga; mvua ikanyesha,
mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko
lake likawa kubwa.
Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment