AUGUST 4
Isaya 55:7-9
August 17
Tafakari yetu ya leo
inatukumbusha umuhimu wa zawadi na adhabu; katika maisha yetu ya kila siku
tumekuwa watu wa kupenda sana kupokea au kupewa kile ambacho ni kizuri hata
kama hatustahili zawadi hiyo; ustahili wa kupokea zawadi stahilivu ni pale
matendo yetu yanaonekana wazi kabisa tunatenda haki bila shuruti; tukumbuke
kuwa daima Mungu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo yeye ndio mwenye usukani nay
eye ndiye yeye; Mungu hapendi kutuadhibu sisi anapenda daiama kutupa sisi kile
kilicho kizuri na bora kwa ustawi wa maisha yetu hapa duniani na baadae
mbinguni; Zaburi 89:14 inatukumbusha kuwa Haki na
hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
Daima hukumu ya Mungu imejaa haki tupu;
Tukisoma kitabu cha
Isaya 55:7-9 kinatukumbusha kuwa Mtu mbaya
na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye
atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu
si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko
nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko
mawazo yenu. Kwa kuzingatia haki
ya kweli ya Mungu siku ya hukumu
kutakuwa mgawanyiko wa makundi kulingana na matendo yao lile kundi la
wenye haki wataungana na Mwenyezi Mungu katika utukufu wake na lile kundi la
watenda maovu watatupwa kwenye moto wa milele jahanamu na watapata adhamu ya
milele; kwa huruma na ukuu wa Mungu bado sisi leo hii tunanafasi nzuri ya
kuungama dhambi zetu ili tusipate hiyo adhabu ya milele;
Tafakari yetu inatuuliza
kama Bwana wetu Yesu kristo alivyowauliza makutano nani ni mtumishi mwaminifu?
Yule ambaye katika fikra zake hana kusitasita katika matendo yake mema na yuko
taayri kumtumikia Mungu kwa Moyo wake wote; au kundi ambalo haliko tayari
kumtumikia Mungu wakijua kuwa bado wana muda wa kutosha hivyo ngoja waendelee
kufurahia maisha ya hapa duniani na Mungu watamtumikia baadae wakisha tosheka
na maisha ya Duniani? Tukumbuke kuwa Mungu ndio kila kitu utukufu na utawala
wote uko juu yake na yeyey ndiye mtawala wa kila kitu. Yeye hutupa zawadi na
kutupa sisi adhabu. Je tunakumbuka hadithi ya Mwanan mpotevu; tukisoma 2 Petro
3:9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama
wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote
apotee, bali wote wafikilie toba. Jambo
la msingi nikuomba ili kuweza kufanya toba ya kweli.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kazi zetu tu
hazitusaidii sisi kupata sifa ya kuridhi mzima wa Mungu, bali kazi zetu na
utiii ni ishara tosha ya kumwonyesha Mungu kuwa tumepokee neema yake; lakini
kama tukiendeleza kiburi na kuto kutii hivyo hiyo ni ishara tosha kuwa hatuko
tayari kupokea neema zake; jukumu letu sisi leo tunatakiwa kufanya kila kitu
katika uwezo wetu kumpenda na kumtumikia Mungu na kutimiza amri zake kwa msingi
kwamba tukitekeleza hili hatutakosa zawadi ya kushiriki utukufu wake mbinguni.
Hii ndio
tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel
Turuka
No comments:
Post a Comment