AUGUST 16
Isaya 1:17-18
Tafakari ya leo inatukumbusha
umuhimu wa kuwapenda na kuwahudumia wajane na yatima; tujikumbushe nini maana
ya kuwa yatima na mjane; katika maana ya kawaida kuwa yatima ni hali ya kukosa
wazazi na kuwa mjane ni hali ya kukosa mwenza katika ndoa. Tafsiri
nyingine ya kuwa yatima au mjane tunaiongelea pale tunavpoongelea kuhusu maisha
yetu ya kiroho tukiamini kuwa kila mtu amewahi kuwa yatima au mjane kiroho. Kwa
tafsiri hii sote tulikuwa yatima wa kiroho mpaka pale tulipo chukuliwa na Mungu
waefeso 1:5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya
Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Tukumbuke kuwa Mungu alitupenda sana ndio maana alimua sisi
tuwe miongoni mwa familia yake Wagalatia
4:6-7 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu
alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana;
na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Kwa msingi huu Mungu
aliamua kutupa sisi kila kitu kwa vile sisi ni sehemu ya familia yake;
Tafakari yetu inaendelea
kutufundisha tukisoma katika maandiko ya matakatifu kuwa Mungu anasema kuwa anatutaka
sisi tuwajali mayatima Yakobo 1:27 Dini iliyo
safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na
wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Kuwajali mayatima
ni jukumu letu kuwasaidia na kuwasemea
wale pale ambapo wanakuwa hawana sauti kutokana na mazingira yanayowazunguka au
sauti yao haina nguvu mbele ya jamii yaani haisikiki au inadhararuiwa; kama
vile Mungu anavyowajali mayatima katika njia ya ajabu sana na kwa njia na uwezo
huo huo anataka sisi tuwajali na kuwasaidia. Tukiamini katika Yesu anautembea
katika Imani hii ya Baba ya kuwapenda kwa moyo wetu wote; Matayo 22:37-40 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na
kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende
jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na
manabii.
Tafakari yetu leo
inalenga kuangalia wajibu wetu wa kuwasaidia wajane na yatima; katika uumbaji
mungu aliwaumba wanawake kama kiumbe muhimu cha matunzo. wanawake wameumbwa ili
wapate ulinzi na matunzo mazuri. na Mungu alipowaumba alijua kuwa wanawake ni
viumbe dhaifu hivyo wanahitaji ulinzi mzuri. wanaume kama viumbe vyeje nguvu
ndio mlinzi wa wanawake. ni jukumu la mwanaume kumlinda,malezi, matunzo na
kuwapa mwelekeo ulio bora. tukisoma zaburi ya 68: 5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake
takatifu. Tukiangalia agano la
kale Mungu alikuwa akiwaakiwalinda na kuwapa faraja wajane na aliagiza
kuwa tunatakiwa kuwapa upendo wa khali ya juu sana; Kumbukumbu ya Torati 27:19 Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane
aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. kwamba utalaaniwa wewe ambaye humtendei haki mjane. Isaya 1:17-18 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki;
wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu
zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu
kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa wakati wa Agano tukisoma kitabu cha Kutoka 22:23-24 Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto
yatima. Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao
wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao, na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi
kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima. Mwenyezi Mungu hapa amesema wazi kuwa yeye mwenyewe atasikia
kilio chao na atakuja kutoa msaada; kweli
kuwa wajane wengi walikuwa ni masikini watu ambao hawana hata uwezo wa kujikizi
mahitaji yao wao wenyewe kwa vile walikuwa hawana njia mbadala ya kujisaidia.
na mara nyingi pamoja na ujane wao na umasikini ambao mara nyingi huwazunguka;
mara nyingi ndio wanakuwa watu ambao wanakuwa mstaria wa mbele wa kujitolea na kutoa kila ambacho wananacho
kwa Mungu.tukisoma 2Timoteo 3:1-3 Lakini
ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,
wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu,
wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema; fundisho letu hapa
katika tafakari yetu ni kuwa; wakati
wetu watu hujipenda Zaidi wao wenyewe.
Tafakari yetu
inatukumbusha kuwa mazingira ambayo tunayo ya kiroho yameondoa kabisa upendo
miongoni mwetu na hasa upendo wa kuwasaidia wajane. Watu wamekosa upendo, na hakuna hamasa ya
kuwasaidia watu wengine; watoto yatima nao wamepata kibali cha Mungu kuwa chini
ya ulinzi na uangalizi wa wazazi wao na pale inapotokea kuwa mtoto amepoteza
wazazi wake hivyo kinachotokea mtoto au watoto wanakuwa chini ya ulinzi wa
Mungu kupitia binadamu ambao wanawajali Yatima. Tukiangalia idadi ya wajane na Yatima imeendelea kuwa
kubwa kwa sababu za vita, matatizo yatokanayo na mama uoto ( mother Nature)
kama mafuriko, vimbunga, mafuriko, njaa na kadhalika;Mhubiri 3:19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo
moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi
moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
Tukisoma Ayubu 29:12-13 Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na
yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea
ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha. tukumbuke kuwa tunapowasaidia wajane na mayatima tunawapunuzia
hisia za upweke na kukosa ulinzi: Tunatakiwa kupigania haki zao; tunatakiwa
kuwalisha na kuwavika na tunatakiwa kuwakinga kutoka kwa watu ambao
huwatenda vibaya; tunatakiwa kugawana tulicho nacho; Tunatakiwa tuwe macho kwa
wasioona na tuwe na miguu kwa walemavu; je wewe uko tayari kuwa ni baba wa
masikini? Tafakari yetu inasisitiza kuwa
tunatakiwa kusikiliza Mayatima wanatakiwa kulindwa hasa
pale wanapopoteza ulinzi wao wa kininadamu; Tukumbuke maneno ya Mungu kuwa
ameweka Baraka ya matunzo ya katika ngazi ile ile kama ya kutoa fungu la kumi
tukiweza kuwatunza na kuwapa mayatima tukumbuke kuwa tunatoa moja kwa moja kwa
Mungu naye atatulipa katika uzito ule ule.
Hii ndio tafakri yetu ya
leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment