AUGUST 15
Luka
11:27-36
Tafakari
yetu ya leo tunaangalia fundisho la yesu katika uwezo wetu wa kuona na kutambua
maono; Yesu daima alikuwa akizungumzia mafundisho ya aina yake, hasa pale
alipotaka sisi tutambue maono ya kiroho juu ya uwezo wa macho; Yesu alikuwa
hazungumzii macho yetu haya ya kibinadamu au upofu wa kibinadamu bali alikuwa
akizungumzia macho ya kiroho; tunatambua kuwa tukiwa na macho mazuri
tunafurahia uzuri wa juu na mwanga tunaweza kuona vitu vingi vizuri na kufanya
uchaguzi; na kama tutakuwa na macho mabovu hatuwezi kufaidi vitu hivi vyote;
neno kubwa hapa mwanga ni kiashiria cha ukuu wa mungu katikqa maisha yetu
kupitia Yesu mwenyewe; yeye alishawahi tufundisha kuwa yeye ni mwanga; Yohana
1:4-5; Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno
alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye
hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima
ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. ni
ukweli ambao haufichiki kuwa mwanga ni asili ya kila kitu; mwanga ni zao la
maarifa, neema na ukweli yeye aliuwasha mwanga kwa wokovu wetu na kwa ushiriki
wa roho mtakatifu;
Tafakari
yetu inatukumbusha kuwa ni jukumu letukupitia mwanga wa kweli kuwa wapole,
wanyenyekevu, kuwa na Imani na kuendlea kutumia vipaji vyetu vizuri; 2 Petro
1:5-9 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno,
za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu,
mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa
upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi
chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika
upendano wa ndugu, upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele,
yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana
wetu Yesu Kristo. Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi
kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.
Tafakari
yetu inatutaka kujiepusha tusije angukia kwenye giza la kiroho hivyo upofu
hautakiwi uwe sehemu ya maisha yetu ya kiroho; tunatatikwa kutumia mwanga wa
ndani na wan je kama faida ya maisha yetu ya baadae; Yohana 1:9 mwanga wa
kiroho kurunzi lake kubwa ni bibilia; tujikumbushe kuwa mwanga wa mwili ni
macho ambaya yanauwezo wa kuona na kuhakiki: tukumbuke kuwa mtu bila jicho ni
sawa na mtu bila mwanga; mwanga wa mwili ni jicho; zaburi ya 14:1 Mpumbavu
amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,
Hakuna atendaye mema.
Tafakari
yetu yatupasa pia kujua thamani ya macho ya kiroho ni mwanga ambao unaletwa na
Yesu kristo kupitia mafundisho yake kuwa yeye ni mwanga na uzima hakuna ambaye
anaweza kwenda kwa baba bila yeye; kwa mwanga wa kiroho tunabarikiwa
kuona kila kitu katika utukufu wa Mungu. Tukisoma waefeso 1:18 macho ya
mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa
utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
Tafakari
nyingine ni jicho la maelewano jicho hili kazi yake iko kwenye akili mawasiliano
ndio kielelezo cha juu kabisa katika kuutafakari mwanga na kuuishi; lakini Yesu
anatuagiza kuwa tunatumia macho yetu katika maono ya kiroho,tunatakiwa kutambua
kuwa yatupasa kuwa wakweli,waaminifu, ambao akili zetu haziharibika; angalia
mfano wa mpanzi: jinsi inavyokuwa rahisi kwetu kuangamia au kurudi katika giza;
na moja ya sababu tunapenda sana vitu vya kidunia; Mathayo 13:15 Maana mioyo ya
watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao
wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa
kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Tafakari
yetu inatukumbusha kuwa mara nyingi tuko tayari kuona kile ambacho
tunataka kuona; na kile ambacho hatutaki kukiona hata kama ni kizuri na
hatutakiona; kile mtu ambacho hataki kukisoma hatakisoma hata kama titakuwa
rahisi namna gani; ndipo hapo tunapobadilisha macho yetu na katika mwenekano wa
ajabu kabisa; mwanga unafunikwa macho yakuwa na ugonjwa roho zetu hujazwa na maumivu
ya kujikataa; ni wakati ambao ukweli hukataliwa; uwongo utawala maisha , dhambi
pia utawala maisha; kiburi huwa ndio mwanga wao; 1 Yohana 1:6-7 Tukisema
ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala
hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika
nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha
dhambi yote.
Hii
ndio tafakari yetu ya leo: Amina
Emmanuel
Turuka
No comments:
Post a Comment