August 31
Luka 10:41-42
Tafakari yetu leo
tunaangalia umuhimu wa kutembea na Yesu katika kila hatua ya maisha yetu; dhana
ya kutembea ni kitu cha kawaida katika maisha yetu; na tunapotembea katika
maisha yetu ya kila siku mara nyingi watu wanaotuzunguka wanatuangalia jinsi
tunavyotembea; na hata wakti mwingine wanakuwa na maoni tofauti kuhusiana na
matembezi au kutembea kwetu; hii ni tofauti unapomkaribisha Yesu aje kutembea
nawe; tukiwa tunatembea na Yesu tofauti yake kubwa ni kuwa uwe unaangaliwa na
watu; au matembezi yako yana furaha au ugumu; hiyo haijarishi la msingi
tunatakiwa kukumbuka kuwa kutembea na Yesu kunahitaji hatua tofauti kabisa na
umakini mkubwa: tukisoma Waefeso 2:8-10 Kwa
maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi
zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu
awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa
katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu
aliyatengeneza ili tuenende nayo. inatukumbusha
kuwa kutembea na Yesu kunahitaji neema ya Mungu;
Tafakari yetu tukiangalia na kusoma Waefeso 4:1-3 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana,
mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa
unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na
kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. tunatambua kuwa Mtume Paulo anaainisha jinsi
tunavyotakiwa kutembea na Yesu kwa kuzingatia vipau mbele hivi; uvumilivu;
unyenyekevu; ubinadamu; upole; kuvumiliana;kupendana;kuimarisha umoja wa
waamini kwa kufanya kazi kwa bidii; tukiweza kuzingatia haya kutembea kwetu na
Yesu ni rahisi sana na tutakufurahia sana; kama tutaweza kutembea katika msingi
huu kinachotokea hapa ni kuwa watu wengine watapata nafasi ya kwanza katika
kila kitu unachofanya;watathaminiwa zaidi , watapendwa, wata saidiwa hivyo ndivyo Yesu anavyotamani iwe;
Tafakari yetu msisitizo yatupasa kufanya nini ili tuweze kufurahia
kutembea kwetu na Yesu; Waefeso 3:20-21 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote
tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam,
atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na
milele Amina. Ili kuweza kutimiza ndoto hii
lazima tuweze kujitambua na kukua kiroho; Kukua kiroho kunaendana na kutimiza
vipau mbele vyote ambavyo Paulo ameviainisha;
Tafakri yetu inatukumbusha somo nzuri kutoka kwa injili ya Luka 10:38-40 Ikawa katika
kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha
akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake
aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini
Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana,
huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie
anisaidie. Tunachojifunza hapa kuwa kati ya hawa ndugu wawili mmoja aliamua
kutembea na Yesu katika matendo yake na Mwingine alikuwa bado anahangaika na
maisha ya dunia; sio kwamba mambo aliyokuwa anayafanya yalikuwa hayafai lakini
sio katika kipau mbele cha maisha ya kiroho; kama anavyofundisha Luka 10:41-42 Bwana
akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu
vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo
jema, ambalo hataondolewa;
Tafakari yetu basi inatufundisha kuwa kwa habari hii
njema wewe leo hii ni nani kati ya Mariamu au Martha; Je uko karibu na Yesu kwa
kiasi gani? Je unaweza kujihesabu kuwa unatembea na Yesu katika kila hatua ya
Miasha yako? Hili ni swali la msingi katika tafakari yetu ya leo, hatujechelewa
kumkaribisha Yesu katika maisha yetu; Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment