August 19
2 Timotheo 1:7-8
Tafakari yetu leo inamwita
Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mwokozi wetu aweze kuja kukaa nasi; Maisha
yetu kama binadamu tunapambana na matatizo na mahitaji mengi ambayo mengine
hujisababishia sisi wenyewe na Mengine Husababisha na watu wetu wengine: katika
mazingira ya aina yeyote ile hatutakiwi kupoteza imani; kama Mtume Paulo
anavyotukumbusha kuwa pamoja na mateso ,kufungwa na kujua kuwa maisha yake
yataishia kuuawa bali hakupoteza iamani yake aliendelea kumwamini Mungu kupitia
kwa bwana wetU Yesu Kristo ambaya alikuwa anakaa ndani ya Moyo wake; Hivyo ni
jukumu letu nasi leo kumkaribisha Yesu katika mwili wetu aweze kuisha nasi
katika maisha yetu; tunajua kuwa ugumu wa maisha uko mbele yetu; msongamano wa
mawazo uko mbele yetu; haya yote yanavyotokea lazima tuwe tayari kuyakabili,
lakini unapomkaribisha Yesu ndani ya maisha yetu changamoto hizi ni rahisi
kuzikabili kwani neno lake linatoa faraja kubwa na kufukuza mbali shida zote;
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuwa ushindi mkubwa wa msiaha yetu ni kuwa kwani yeye anafahamu
hata idadi ya nywele Mathayo 10:20 lakini ninyi,
hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Sisi hatuna uwezo wa
kujua idadi yake lakini yeye anajua; hivyo tunataka zawasi gani zaidi katika
maisha yetu kama sio uwepo wake katika maisha yetu? Yesu ni jibu la maswali
yetu yote; je nani angeweza kufanya kama Yesu ambaye aliuacha utukufu wake wote
na kukubali kuja duniani na kupata mateso, kudharauliwa, kupigwa, kutukanwa na kasha
kusulubiwa msalabani kwa ajili yangu mimi? Kwa nini sasa nisimkaribishe Yeye
katika maisha yangu? 2 Timotheo 7-8 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya
nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana
wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami
kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;
Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa;
inatukumbusha mfano wa Yule mama ambaye alikuwa akisumbuliwa na tatizo la
kutoka damu kwa miaka mingi na alikuwa akitafuta tiba kwa kipindi hicho chote;
Lakini aliposikia habari za Yesu na ukuu wake alijisemea moyoni mwake
namkaribisha Yesu katika maisha yangu, lakini kwa uwezo ambao anao pamoja na
kumkaribisha katika maisha yangu nitaligusa tu pindo la vazi lake nami nitapona.
Pamoja na umati mkubwa wa watu alifanya kila jitihada za kujipenyeza, kusukuma
na watu ambo pia walitaka kumwona na kumsikiliza Yesu lakini walikuwa hawaka
tayari kumkaribisha Yesu katika maisha yao ili aweze kuwaponya na matatizo yao;
lakini yeye alifanikiwa kumgusa pindo lake kwa imani moja tu kuwa ugonjwa wangu
utapona kwa tendo langu na ilikuwa hivyo; hivyo tunamwitaji yesu kwa kuwa Yesu
ni jibu katika matatizo yetu:
Hii ndio tafakari yetu ya leo- Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment