July 22
Warumi 3:10
Tafakari ya leo Kwa hakika mwanandamu anahitaji upeo mkubwa wa
nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia zote za
kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa
moyo mpana na kujenga daraja la msamaha. Kusamehe mtu ambaye amekukosea,
kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu
kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau,
kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu
ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii.
Tafakari yetu inatukumbusha umuhimu wa kumsamehe
yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile
vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe
tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini pasipo imani
haiwezekani (Waebrania 11:6).
Inatufundisha kuwa mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini
kwamba yeye yuko,
na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na
Mungu katika Imani.
Kama ilivyoandikwa
hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha
imeelezwa katika Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari
kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi
tumaini lake la msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa
na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na
Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala
Baba yenu hatawasamehe makosa yenu." Wale wamesamehewa husamehe.
imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye
huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe
ninyi."
Tafakari inasisitiza neno kusamehe kwa
kweli hakuhesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero
akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe?
hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara
sabini." Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa
dhambi. Wakolosai 2:13-14 inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa
sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja
naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena
akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami
nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia
furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi
zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho
iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu
usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya
wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa
dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye
rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu
mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu
likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi
yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana
naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati
unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."
Tafakari yetu inaonyesha umuhimu wa
kuwa mnyonge wa moyo wako mbele ya Mungu na wala kutambua hatia yangu,
haijafika hali ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina
zote za tabia zetu mbaya pamoja na misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya
mambo fulani mabaya: kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane
watu, tamaa mbaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika
dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba
asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi
kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya
wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa
ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo
uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole,
uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia
ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha
mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Ni jambo la muhimu sana kujua kuwa hakuna
dhambi ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba
kila mmoja wetu hatimayeawe na uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na
kumsababishia majeraha ambayo yamejenga chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu
anataka tupokea msamaha na utakaso wa Mungu ni; katika imani jambo ni rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia
kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu
wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli
pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule
aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu
na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu
katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na
kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na
ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili
kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo hebu
jitafakari kwa nini umekuwa na kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani
yako, ndugu yako ambao wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali
amekukosea mara ngapi angalia je wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule na
mara ngapi?- amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment