July 14
Tafakari ya leo tunaangalia tatizo la kumwogopa mtu mwingine
katika maisha yetu kama wakristo; kama wewe ni mfuasi wa Yesu basi hutakiwi
kumwogopa mtu mwingine yeyote ambaye hawezi kuua roho; kama katika maisha yako
utakuwa unafanya maamuzi yako kwa kumwogopa mtu au watu wengine basi wewe
unatatizo kubwa sana la kiimani. Kama tabia hiyo ikikutokea basi unatakiwa
kucha kuwaangalia watu wengine katika kutimiza mahitaji yako; bali tunatakiwa
tumtazame Mungu ndiye pekee mtoaji wa mahitaji yetu; kwa kufanya hivyo utajisikia
vizuri mwenyewe bila kufuata maoni ya wengine.
Tafakari yetu leo inatukumbusha ili kujiridhisha katika maamuzi
yako jambo la kwanza unatakiwa ujiulize kuwa wewe ni nani? Na ukumbuke kuwa
wewe umepewa na mwenyezi Mungu neema ya kupendwa na yeye; tulivyoumbwa
tuliumbwa watupu na Mungu kwa mapendo yake ametujaza na Baraka ya upendo. Kama
wewe umejazwa na upendo wa Mungu kwa nini sasa unakubali kutawaliwa na watu
wengine katika mawazo yako? Binadamu mwingine yeyote yule hana nguvu ya
kutawala akili yako isipokuwa Mungu tu. Ndio maana Yesu alivyosema kuwa
unapojiona kuwa unatabia ya aina hiyo yeye ana njia ya kutokea; basi tunatakiwa
kumruhusu Yesu kujaza sisi na upendo wake ambao hauna mipaka lakini kama
tutakuwa tayari kutekeleza mipango ya Mungu na sio mipango ya binadamu
tunatakiwa kuwa tayari katika kutimiza utukufu wa mungu na sio matamanio yetu.
Ili tuweze kujihakikishia kuwa tuko imara na hatumwogopi mtu yeyote lazima
maisha yetu tuyaweke chini ya msingi wa uangalizi wa Yesu hapo hatutakuwa na
sababu ya kumwogopa mtu yeyote na tutajihakikishia furaha ya kweli;
Tafakari yetu inatuonya kuwa hatutakiwi kabisa kutawaliwa na
mawazo, woga ; mwonekano dhidi ya watu wengine kuwa watasemaje ; najua mara
nyingi tatizo linakuwa pale wanapotaka kunufaika na kile ambacho wao wanancho
na pengine mimi au wewe huna au sina na unatamani upate huko ukifikiri kuwa
Mwenyezi Mungu hawezi kukupa wewe hiyo Baraka. Tunapo mwamini na kumtumaini
mungu yeye Baraka zake anazitoa kwa namna ya ajabu na pekee kabisa. Hivyo hata
pale tunaposoma bibilia katika msingi huu ndipo tunapoona jinsi gani
tunavyowaogopa binadamu wengine. Tuangalie mifano kutoka Mwanzo 12:10-20 au
Mwanzo 20: I-2 AU Hesabu 14:11 DEUt 1:17 Zaburi 56:3-4 Matahayo 10:28 1 petro
3:14
Lazima tutambue kuwa woga wa kweli wa kumwogopa Mungu ni kupitia
maungamo; Mathayo 22:16 kwa kuungama dhambi zetu Mungu kupitia bwana wetu Yesu
Krsito anaondoa woga kabisa; tunatakuwa kujitathimini wenyewe kwa kujiridhisha
kuwa mungu ni wa ajabu katika maisha yetu na hatuna sababu ya kumwogopa
yeyote isipokuwa yeye; woga kwa Mungu ni chanzo cha maarifa. Mungu lazima
aogopwe kwa sababu yeye ni chanzo cha haki;
chanzo cha upendo; na mafanikio yetu. Zaburi ya 77: 13
Ili tuweze fanikiwa lazima tuishi katika mafundisho ya
Mungu; tujiepushe kwa kikombe
cha ubinafsi na baada yake tunatakiwa tujazwe na kikombe cha roho wake
ili kitupe ujasiri wa kuweza kushinda woga na kuwa tayari kuungama dhambi zetu
ili kujipatanisha na Mungu. Bibilia inatufundisha kuwa watu wamegawanyika
katika makundi makubwa matatu; maadui, majirani na wafuasi wa kristo. Jambo
kubwa katika makundi hayo yanayoleta tofauti ni upendo upendo huleta kila kitu;
tunawahitaji watu ili tuweze kuwauliza maswali; je tunawahitaji watu ili
kukamilisha haja zetu? Wafilipi 2:3 auwarumi 13:8. Tukumbuke kuwa woga ni
tatizo la jumla kwa binadamu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment