July 21
Luka
17:20-21
Tafakari ya leo inatukumbusha
kuwa ufalme wa Mungu uko ndani yako; mafarisaya walimuuliza Yesu je ufalme wa
Mungu utakuja lini? Yesu aliwajibu kuwa ufalme wa Mungu hauji kwa kuangalia
vitu na matukio yanayoonekana isopokuwa ufalme wa Mungu uko ndani yenu; hata
pale Philipo alipomwuliza yesu awaonyeshe baba nasi tutaridhika; Yesu alimjibu
kuwa nimekuwa nanyi muda huu wote na bado hamjemjua baba? Yeyote aliyeniona
mimi amemwona Baba; mimi niko ndani ya baba na baba ndani yangu; na yeyote
anayeamini katika neno langu ameamini kwa baba aliyenituma;
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuwa jukumu letu inatakiwa tujiangalie zaidi undani wa matendo
yetu na sio matendo yetu au mwonekano
wetu wan je katika maisha ya kumtumikia Mungu; Mwonekano wetu wa nje unalinganishwa
na jinsi tunavyojiangalia katika kioo na kujiona kitaswira tuko vipi na daima
tunachukua muda wa kujirekebisha ili tuweze kuonekana watanashati. Ni jambo
nzuri hivyo kama tukiweza kuchukua juhudi hizo katika taathimini ya ndani
itakuwa jambo nzuri sana; ni wazi kuwa katika mazingira ya maisha yetu leo hii;
maisha yetu yametawaliwa na utitili wa mambo; maisha yetu yamekabiliwa na
majukumu yetu ya kila siku, kazi ambazo lazima tuzimalize kwa wakati, mahitaji
ambayo tunayaona ya lazima; na tama zetu za kila siku mabazo tunatamani
kuzikamilisha; ni wazi kabisa na rahisi kabisa kama binadamu kupoteza mwelekeo
katika utitili huu wa maisha; Luka 15:17
ni kama mtu ambaye ameshituka kutoka katika ndoto mbaya na
kutisha pamoja na kutokwa na jasho lakini itamchukua muda ili akili yake iweze
kurudi tena;
Tafakari yetu leo
inatukumbusha kuwa katika khali ya
kupotea inapelekea mambo mawili ulinzi
wa uwongo ambao unakudhoofisha wewe mwenyewe; hatimaye unajipoteza mwenyewe
kuna mambo mawili yatajitokeza mosi ni kujijua aina ya mtu uliyezoea kuwa na
pili na unajipoteza kabisa katika uhalisia wako. Je unakumbuka hadithi ya mwana mpotevu alifika mahali akajitambua yeye mwenyewe kuwa
amepotea; tabu zote ambazo alizipata ni matokeo ya tama ambazo alifikiri kuwa
atapata maendeleo makubwa katika maisha yake matokeo yake kuwa aliishia kupotea
na kurudi nyuma kimaendeleo na kimaisha. Utambuzi wa kwanza ambao humjia mtu
mabaye amepotea anapojitambua kuwa alikuwa amepotea ni khali ya kujijutia kwa
namna gani alianguka na kushinda kufika pale alipokuwa amekusudia kufika,
ananza kujenga woga kwa nini amefanya
hivyo alivofanya. Je unakumbuka Samsoni alipoamka na kujikuta mikononi mwa
maadui na sio mikononi mwa Mungu? Au unamkumbuka Yona alivyotapikwa na samaki
ukingoni mwa pwani; ndio maana lazima tukubali kuwa kitu kikubwa hapa duniani
sio wapi tunaposimama bali ni katika mwelekeo gani tunakwenda: na tutafurahi
zaidi pale tukapofika mwisho wa safari yetu katika utukufu wa Mbinguni;
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa kitu kikubwa na cha msingi
sana katika maisha yetu ni kuwa na
furaha ambayo inatupa sisi nafasi ya kutenda; furaha ambayo inatupa sisi kitu
cha kutumaini na ikumbukwe kuwa mtu yeyyote anaweza kupata furaha hasa pale
ambap anapata kamba ya wokovu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumvusha. Tukumbuke
jinsi Samsoni pamoja na kuwa kipofu baada ya kutekwa na maadui kwa sababu ya
Delila lakini kwa kumtumaini na kujuta makosa yake Mungu alimrejeshea nguvu
zake kwa dhumuni hasa la kuwaangamiza wafipipi ambao walikuwa wamemeteka na
kumtesa. Yona pamoja kuwa alikuwa gizani kwenye tumbo la samaki kwa vile
aligundua kosa lake wokovu wa Mungu na mwanga wa wokovu ulimrudia kwa mara ya
pili na kuanza kuhubiri.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mtu lazima aishi kwa malengo na
madhumuni na kama lengo au dhumuni likipotea basi maisha yake yanakuwa hayaeleweki ndipo
tunapohitaji msaada wa Mungu katika kufanikisha dhumuni la maisha yetu. Pale ambapo
tunashindwa kujitambua unakuwa umepotea kiroho, macho yako yanakuwa yamefungwa
masikio yako yanakuwa yamezibwa, na ni Mungu pekee yake ambaye anaweza kuleta
muujiza katika wakati kama huu. Ni wkati ambapo neema ya Mungu inahitajika.
Tumkumbuke Daudi alipopotelea katika dhambi lakini ujio wa Mungu Katika maisha
yake uliweza kumrudishia furaha na amani. Amani ya kweli upendo wa kweli na
maisha ya neema ya kweli hayawezekani bila uwepo wa Mungu. Mungu ni kila kitu
kwetu na katika maisha yetu ya kweli.
Ni ujumbe mzito ambao unahitaji utambuzi wa kweli. Hii ndio
tafakari yetu ya leo. Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment