WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, March 16, 2016

MUNGU NI MSIKILIZAJI MZURI SANA!



March 16

Yohana 15: 14-15

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi kuongea na Mungu, kwani Mungu ni msikilizaji mzuri sana na hutupa majibu ya maombi yetu. Tunavyoongea na Mungu ni sawa kama tunavyotumia simu katika mawasiliano yetu ya kawaida. Tunavyoongea kwenye simu hatumwoni mtu mwingine kutoka upande wa pili ili tunasikia tu sauti hivyo jukumu letu katika mawasiliano ni kuongea na kusikiliza. Hivyo uhusiano wetu na Mungu ni sawa hivyo hivyo. Tunaongea na Mungu kupitia sala  na tunamsikiliza Mungu kupitia mafundisho ya bibilia kwenye jumuia zetu, nyumba za ibada na katika masifu mbalimbali. Yakobo 5:16 uangameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

Yohana 15: 14:-15 ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Yesu ametoonyesha hapa kuwa yey ni rafiki bora kwani amekuwa msikilizaji mzuri katika maongezi yake na Mungu, kisha ameweza kutuletea sisi ujumbe wa neema kwetu. Asingekuwa msikilizaji mzuri asingeweza kutufahamisha sisi habari njema toka kwa Mungu. Hivyo Mungu ni msikilizaji mzuri sana tunapoongea naye. Mungu anapenda nasi tuweze kuwasiliana naye katika shida zetu na katika mafanikio yetu yote. Hata pale tunaposhindwa katika mahangaiko yetu Mungu anapenda sisi tuongee naye na tumpe taarifa. Na jambo nyingine Mungu anapenda sana sisi tumtarifu mipango yetu kabla hata hatujeanza kufanya. Pale tunapotaka kununua chochote tumshirikishe Mungu kwani  yeye yuko kutuongoza; pale tunapokuwa na mipango ya kusafiri tuongee naye kwani yeye atatembea nasi na atatuongoza. Hata katika maamuzi yetu magumu tuongee na Mungu yeye atatuonyesha njia ya kufikia utekelezaji wa maamuzi yetu.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa Mwenyezi  Mungu ametuagiza tunapongea naye na kumweleza shida zetu, mafanikio yetu au pale tunapoomba msaada hataki sisi tuwe wanafiki hata kidogo; Mathayo 6: 5-7 ; tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin nawaambia wamekwisha kupata thawabu. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliyesirini; na baba yako aonaye sirini atakujazia. Nanyi mkiwa katika kusali msipayuke payuke, kama watuwa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu yamaneno yao kuwa mengi.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunapoongea na Mungu tunatakiwa tufanye mazungumzo yetu kupitia sala kwa ufasaha kama tunavyongea na rafiki yako mpendwa na unayemweshimu; kwani unapongea na mtu unayemweshimu huwezi tumia menono ya kihuni ya kimtaa mtaa; au kwa sauti ya juu ambapo hata hamwezi kusikilizana; kwa misamiati migumu ambayo hata mwenyewe unapata tabu kuikumbuka;  hutaki kumhdaririsha hata kidogo hata watu wengine wakikusikia ukiongea wafurahie mazungumzo yenu. Ni wazi kuwa kwa kuongea kwa namna hii mwenyezi Mungu atakujibu maombi yako mara moja bila kuchelewa.

Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa tunatakiwa sana tuisome bibilia na kuielewa ili hata tunapoongea, kumsifu au kuomba msaada kwa Mungu tuwe tunajua mwongozo wa namna ya kuongea naye. 1 Petro 3: 15 Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Na tutaweza tu kuwa tayari kama tutaweza kulielewa na kulishika neno la Mungu; na hata tutakapo kuwa tunaongea naye tutakuwa katika nafasi nzuri. Na ili tuendeleze mahusiano mazuri na Mungu tunatakiwa tutumie muda wetu wa kutosha nay eye, inaweza kuwa kwa kusali pamoja na familia, kusali pamoja na wanajumuia wengine au kwa kusali pekeyako na kwa kufunga Mathayo 6:16-18 tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao,ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin nawaambia, wameshakwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu  kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazia. Yesu hapa anatufundisha kuwa  mfungo hutufanya sisi kuwa karibu zaidi na  mungu lakini kama tutaufanya katika unyenyekevu Mkubwa

Tukumbuke kuwa  mahusiano mazuri yanjengwa katika msingi wa uaminifu;  najua hakuna Ndoa yeyote itadumu au kuwa na mafanikio bila wanandoa kuaminiana; mahusiano ya maisha yetu yanajengwa katika kuaminiana na sio katika sheria. Tunajifunza kwa walimu wa kanisa na wanasheria wakati wa yesu kila kitu chao kilikuwa kimejengwa katika sheria, sheria, sheria. Yesu alituonyesha sisi muhimu wa kuwa waaminifu katika kutekeleza majukumu yetu mbele ya Mungu. Mungu anaitaji Kuwa na Imani na kuwa waaminifu katika kutekeleza maelekezo yake; kwa Imani na Kuamini tutamweka Mungu Mbele katika majukumu yetu. Waebrania 11:1 basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya  mambo yasiyoonekana. Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yey yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Kuamini ni sawa na Barabara mbili. Ni lazima tumwamini Mungu na Mungu Mungu lazima atuamini sisi, tukizingatia kuwa Mungu ni Yule Yule Jana, leo na Kesho. Mungu ni mwaminifu na wala hatabadilika hata kidogo.

Yesu alituonyesha kupitia agano jipya maisha yake na mawasiliano yake na Mungu hakuwa unazingatia sana sheria Fulani,hata wafuasi wake daima walikuwa wakimwangalia na walikuwa wakishangaa jinsi alivyokuwa akiongea na Mungu kwa utulivu na kwa amani kubwa.

Tukumbuke kuwa mara nyingi tunavyoongea na Mungu tumekuwa watu ambao tunamwogopa tukifikiri kuwa Mungu hutisha, anahasira na sio rahisi kumridhisha; Lakini Yesu ametufundisha kuwa Mungu ni Rafiki yetu wa ajabu na ndio kimbilio letu la kudumu na Mungu anapenda sana kutumia muda wake mwingi nasi kupitia sala zetu na masifu katika ibada zetu;

Tafakari  Ya leo inatushauri kuwa tuondoe vikwazo tulivyojiwekea tunavyoongea na Mungu ili tuendelee kuona uzuri na wema wa Mungu wetu; tunatakiwa tuimarishe mahusiano yetu na Mungu kwa kufuata mafundisho na maagizo yake kama tulivyoelekezwa na Bwana wetu yesu kristo.

Tafakari ya leo inatufundisha kuwa Katika maisha yake Hapa duniani Yesu alikuwa rafiki wa kila mtu alikunywa na wenye dhambi, wakasema , mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Yesu aliwapenda watoto; aliwajali Malaya alipokuwa akiwafundisha kuhusu wokovu ili waachane na dhambi zao na wamrudie mungu; watoza ushuru, wenye dhambi, mwana mpotevu, mwanamke msamalia; na mwanamke ambaye alifumaniwa akizini na ambaye alitakiwa apigwe na mawe mpaka kufa lakini aliyaokoa maisha yake; yesu alimpenda kila mtu hata walimu wa sheria ambao wao walikuwa adui wakuu wa  Yesu. Jambo la msingi tunatakiwa tuimarishe mawasiliano yetu na Mungu Kupitia sala.

Hii ndio Tafakari yetu ya Leo Amina


Emmanuel Turuka

Tuesday, March 15, 2016

MTAZAMO WAKO DHIDI YA MUNGU UKOJE!



March 15

Wafilipi 2:5

Kwa ujumla Mtazamo/tabia ni zao la ndani ya kila mmoja wetu tunapolinganisha na mazingira yanayomzunguka kama watu na vitu; Tabia inatumika sana wakati unapofanya kitu chochote nje yako mwenyewe yaani kitu ambacho akikuhusu wewe mwenyewe. Neno la Mungu linatukumbusha katika hili kuwa kwa kuwa kwetu wakristo tunatakiwa kuimarisha tabia na kuwa kama Yesu; Tukisoma Wafilipi 2:5 Iweni na nia iyo ndani yenuambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu: Tukisoma Waefeso 4:22 mvue kwa habari ya Mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya;

Wengi wetu kwa urahisi tunaweza kutambua mitazamo mibaya kuonekana katika mazingira tofauti kutoka na vitendo vyetu kama uasi, dharau, kukosekana kwa uvumilivu, kukosekana kwa ushirikiano, kutojali, kuvunjika moyo, kokosekana uhuru, dhulma, kiburi, ubinafsi, Hii ni mifano ya msimamo mbaya ambayo Wakristo wanapaswa kukataa.

Mithali  23:7 hata mshale umchome maini; kama ndege aendaye haraka mtegoni; wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Tukumbuke kuwa mtazamo au tabia ni zao la mtu la ndani, limejificha ndani ya mtu ambalo ndilo msingi wa matendo yetu tuyafanyayo. Hakuna mtu yeyote ambaye ajuaye wewe unafikiria nini; ndio maana unaweza ukamchekea mtu na kumwonyesha kuwa wewe ni mtu safi sana kwake bali mtazamo wako uko tofauti sana; kumbe wewe ni adui, mkubwa; Lakini usijisahau kuwa Mungu anajua nini unawaza na nini unataka kumfanyia mwenzako. Hivyo Mtazamo au tabia ni kitu ambacho Mungu tu ndiye anayefahamu na yeye pekee anaweza kukusaidia kukurekebisha kwani mabadiliko hayo lazima yaanzie ndani yako na kwa Masada wake.

Mifano ya tabia mbaya iko mingi hasa kwa sisi wakristo kuna wale ambao wanakwenda kanisani na kushiriki vitu vingi hata uimbaji wa kwaya, utoaji wa michango mikubwa, wenye furaha wakati wote kwa sababu kila kitu kipo sawa kwa upande wao; Kwa bahati mbaya mambo ya kigeuka hasa upande wa uchumi yakianza kwenda vibaya kila kitu uanza kugeuka mahudhurio kanisani yanapungua; watu wanaanza kujijengea chuki na watu wengine na hatimaye chuki hiyo hujengwa dhidi ya Mungu wakiamini kuwa kwao Mungu ni sababu ya anguko lao; hivyo uasi unaanza hapo.

Lakini tukumbuke kuwa mtazamo ulio bora wakati wa shida inatakiwa kwa tuwe karibu zaidi na Mungu - kuangukia miguuni pa Yesu. Biblia inaeleza wazi kwamba Mungu hufanya mambo yote katika wakati wote kwa upendo ule ule bila kubadilika katika mafanikio yetu na katika shida zetu; tukumbuke kuwa shida kamwe haitamshinda mtu mwenye mtazamo sahihi na mwenye kumtegemea Mungu.

Wagalatia 5:19-21 Matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi; husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawatauridhi ufalme wa Mungu.

Tutambue kuwa mtu yeyote ambaye ana tabia mbayo inakwenda kinyume na mamlaka ya dunia pia ana matatizo mbele ya Mungu.Wagalatia 5: 22-23 lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu, wema, fadhili. uaminifu;  upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Mtazamo sahihi mbele ya Mungu:  Zaburi ya 111:10 kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, wote wafanyao hayo wana akili njema, sifa zake zakaa milele. Tukisoma Marko 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwan nguvu zako zote. Yohana 14:15 mkinipenda, mtazanishika amri zangu. Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpigeni Shetani, naye atawakimbia.  Mtazamo wetu lazima heshima, utii, upendo, uaminifu, unyenyekevu, utii, worshipful, na sala.

Mtazamo wetu kuhusu watoto wa Mungu Yohana 13: 34-35 Amri mpya nawapa, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Warumi 12:10 kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu. Wakolosai 3: 16 Neno la kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana  kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Waebrania 3:13 lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe  mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

Mtazamo wetu kuhusu watawala wa dunia unatakiwa wa kuheshimu mamlaka, kushirikiana na mamlaka, kuwajibika ipasavyo, kuwa wenyeneyekevu, kutoa msaada unaotakiwa, kuhimizana na kushirikiana. Waebrania 13:17 watiini wenye kuwaongoza na kuwanyenyekea; maana  wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi. 1 Peter 2:13-15 Tiini kila kiamriwacho na watu,kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipizia kisasiwatenda mabaya na kuwasifu watenda mema. Kwa sababundiyo mapenzi ya Mungu Kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu.

Mtazamo wetu kuhusu tukipatwa wakati Mgumu tunatakiwa kuwa wapole, watu wa kushukuru na kuamini kuwa hakuna linaloshindikana mbele ya Mungu. Warumi 8:28  Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Mungu anajua mitazamo yetu ndio maana kila mara anawatuma wajumbe wake ambao ni manabii katika kutuelekeza katika mitazamo iliyo bora: Yeramia 1: 17., 19 Haya Basi wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao; Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda maana; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana ili nikuokoe. Au alivyoongea na Ezekieli 2:7 Nawe utawaambia maneno yangu; kwamba watakusikia au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.

Tafakari ya leo inaendelea kutukumbusha kuwa tunatakiwa twende mbele ya Mungu na Mitazamo yenye, utii, unyenyekevu, adabu; ya kushukuru na yenye kuomba msamaha. Mungu pekee yake ambaye anatujua na tabia na mitazamo yetu ambayo iko mioyoni mwetu ambayo uzaa matendo mema au mabaya. Tunatakiwa kutembea katika njia ya bwana ya kumtii, na kutekeleza yale yote anayotuma kufanya au yale ambayo tayari yamekwisha ainishwa katika vitabu vyake na mafundisho yote ambayo Yesu alitufundisha.

Hii ndio tafakari yetu ya leo. Amina

Emmanuel Turuka




Monday, March 14, 2016

TUNAUTUMIAJE MUDA/WAKATI WETU?





March 14

Zaburi ya 90
Tafakari ya leo tuangalie jinsi ambavyo tunatumia muda wetu. Je tunautumiaje muda wetu na kwa faida ya nani? Tukumbuke kuwa tunatakiwa kutumia muda wetu vizuri hasa tunapofahamu kuwa hapa dunia tuko katika mpito wa maisha yetu; na mbele ya Mungu hakuna dakika wala sekunde ambazo tunaweza kuzirudisha nyuma. Tukumbuke kuwa Mbele ya Mungu kila siku inafungua ukurasa mpya tunapaswa kuwa makini jinsi ambavyo tunatumia muda wetu. Tunaaswa  kuwekeza ili tuweze kupata furaha na mafanikio ya kweli.
Tunaishi kwa kufuata majira kwa kujua kuwa muda ni muhimu katika maisha yetu hivyo hatutakiwi kucheza nao. Katika mahangaiko yetu mara nyingi tunapigana sana na wakati tukikimbizana huku na huku na pengine bila mafanikio yeyote. Lakini tunamwona Bwana wetu yesu Kristo yeye pamoja na kuwa na kazi kubwa ya ukombozi wetu kamwe muda haukuwa tatizo kwake; alikuwa anajua kuwa ana muda mfupi wa kutimiza kazi ambayo alikuwa amepewa na Mwenyezi Mungu, bado alikuwa  na muda wa kuwawekea mikono na kuwabariki watoto; Muda ulikuwa rafiki kwake.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa Mungu anaishi katika wakati wote yeye ndiye aliyeumba muda huu ambao sisi leo hii unatuendesha mbio. Lakini tukisoma bibilia kwa makini tutajua namna ya kuutumia muda ili uwe rafiki na sio adui. Mwenyezi Mungu anatukumbusha kuwa tunatakiwa kuthamini muda na kuufanya kuwa kitu muhimu sana katika misha yetu. Kila siku ipitayo ina maana kubwa sana kwetu.
Je tunajua thamani ya mwaka mzima katika maisha yetu? Kipimo rahisi cha kupima wakati kwa mwaka mmoja, tunaweza kupima kwa kumuuliza mwanafunzi ambaye amefeli katika masomo yake na ameshindwa kuendelea na shule;
je tunajua thamani ya  saa moja tumuulize mfanya biashara ambaye ndege yake ilicheleweshwa na akakosa mkutano wa kibiashara na akaishia kupata hasara kubwa katika biashara zake.
Je dakika moja ina thamani gani tunaweza kujifunza kwa mtu ambaye amepata shida ya Moyo na maisha yake yakaokolewa na wafanyakazia wa dharura;  
na je sekunde ina faida gani muulize mtu ambaye amekoswa koswa kugongana uso kwa uso na gari nyingine. Hawa wote watakusimulia nini maana ya kujali wakati: na wangeweza kupata nafasi mpya wangeutumia wakati vizuri sana.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa  jana ni historia, kesho haiko mikononi mwetu; muda ambao tunao ni sasa ambao ni zawadi; muda upo jinsi ulivyo sisi tunatakiwa tujibadilishe ili kwenda sambamba na muda huo lakini kamwe hautungoji sisi; muda ni kitu ambachohakibadiliki;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa pamoja na mbio zetu zote za maisha bado tuna nafasi nzuri ya kuweza kuratibu Muda wetu; kama nafasi ya kwanza tutampa Mungu na nafasi ya pili kwa ajili ya familia zetu; tukikumbuka kuwa kila dakika ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo tunapasa kuitumia vizuri. Hivyo wajibu wetu sio kuhangaika Kuutawala muda bali tunatakiwa kujitawala wenyewe na kuutumia muda vizuri. Kama waefeso 5:14 -15 Hivyo husema, Amka wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, na Krsito atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima. Tunatakiwa kutembea kama watu wenye hekima sio wapumbafu.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kama hatutaweza kutumia vizuri muda wako hivyo mtu mwingine atakusaidia kuutumia muda wako vizuri. Muda ambao tumepata uko sawa kwa wote hivyo hakuna mtu ambaye amepata muda mwingi zaidi. Bibilia kupitia Luka 12:34 kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapo kuwapo na mioyo yenu.
Tujikumbushe hadithi ya  Mariamu na Martha:  Mariamu aliyeketi miguuni pake yesu, akasililiza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema Bwana huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Mwambie anisaidie. Bwana akamjibu akamwambia Martha, Martha, unasumbuka na Kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi. Lakini kinatakiwa kitu kimoja tu: Mariamu amelichagua fungu lililo jema ambalo hataondolewa.

Yesu anatufundisha hapa kuwa Imani na kazi ni vitu vinavyo tegemeana na vyote ni muhimu kwa ukuaji wetu wa mwili na kiroho. Lakini tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi katika katika kutafuta ufalme wa Mbinguni; ndilo fungu ambalo Mariamu alichagua; hili ni fungu sahihi kwetu sote. Bibilia inatufundisha kuwa matumizi yetu ya muda na maisha yanakwenda sambamba. Tunatakiwa kuwa makini na matumizi ya Wakati ili ulete faida ya kweli mwisho wa maisha haya tunayoishi.

Tafakari ya leo inatukumbusha Wakati huu tulio nao ndio haswa wakati wa kumtumikia Mungu. Kama 2 Wakorinto 6:2 kwa maana anasema, wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndio sasa tazama siku ya wokovu ndiyo sasa. Tukumbuke kuwa Mungu ametupa sisi wakati mzuri wa kumjua Yesu kama mwokozi wetu na kupitia yeye tufurahie maisha ya mbinguni lakini tunatakiwa kutumia wakati wetu vizuri.
Nahitimisha tafakari yetu ya leo kwa kutoa ushauri kuwa wakati ni huu wa kumtumikia Mungu; tukiangalia hivi sasa jinsi migongano mingi inavyoikabili dunia; tukumbuke mafundisho ya ya bibilia kuwa, mwisho wa dunia utakavyokaribia kutakua na vita, tetesi za vita, kusalaitiana; mauaji; majeshi kuasi; tauni na balaa la njaa kila mahali; tunatakiwa kutumia muda wetu vizuri tusije chelewa kama  Mithali 1:28 inavyosema ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; watanitafuta kwa bidii wasinione. Leo ndio siku yetu wa wakovu kwani Mwenyezi Mungu yuko tayari kusikia sauti yetu na kilio chetu. Wakati ni huu wa kumrudia  na kumtumikia Mungu wetu.

Hii ndio  Tafakari  yetu ya leo Amina.

Emmanuel Turuka







Sunday, March 13, 2016

NABURUDIKA NDANI YA YESU

March 13


Tafakari ya jumapili ya leo tuburudike ndani ya Yesu ndio chanzo cha furaha yetu ya milele. Amina

Saturday, March 12, 2016

UTUKUFU UNA YEYE SIKU ZOTE


March 12

Tafakari ya leo tushangilie  ukuu wa utukufu  wake daima. Bado tuko kwenye kipindi cha mfungo kuelekea Sikukuu ya Pasaka tunakila sababu ya kusherekea kazi ya mikono yake Bwana wetu. Amina

Friday, March 11, 2016

JE TUNAZITUMIAJE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI;




March 11

MATHAYO 16:19

Tafakari Ya leo inalenga kuonyesha jinsi ambavyo sisi wana wa Adamu tumekabidhiwa funguo za uzima wa milele. Ni zawadi ya pekee sana kwetu kuaminiwa na kukabidhiwa funguo hizi ambazo ni muhimu sana katika safari yetu ya kuelekea kwenye maisha yetu ya baadae; funguo unakupa uwezo, nguvu ya kuingia sehemu ambayo imefungwa au kufunga ili mtu mwingine mwenye nia mbaya asiweze ingia katika nyumba hiyo. Isaya 22:22 anasema kuwa Na ufunguo wa Nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.

Tafakari ya leo inatuonyesha kuwa funguo ni Nguvu, ni mamlaka, ni upako kwa sisi wakristo inawakilisha ni nguvu au uwezo ambao Mungu anatujalia sisi binadamu, na inapatikana kwa kila mtu aliyeelewa umuhimu na kuwa tayari  kuzitumia funguo hizo kwa maisha ya Mbinguni. Mwenjili Mathayo anaweka wazi tukisoma Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa Mbinguni; na lolote utakalo lifunga duniani; litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Kwa ujumbe huu tumepewa kibali cha kufanya maamuzi.

Yesu alitoa kibali hiki kwa Peter, kibali ambacho Peter  aliwapa mitume na wafuasi wote na hivyo hivyo kibali hicho kimeruhusiwa kwa wakristo wote ambao wako tayari kutumia nguvu na mamlaka ya funguo na ambao wako tayari kuzitumia. Hata tukisoma Injili ya John 20: 21-23 Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi name nawapeleka ninyi. Naye akisha kusema hayo akawavuvia, akawaambia pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaofungia dhambi wamefungiwa. Wow kweli tumepewa nguvu za ajabu lakini hatujui jinsi ya kuzitumia.

Tafakari ya leo tunavyoendelea na mfungo wa siku arobaini kuelekea siku ya ufufuo ambayo ndio siku maalumu ya mwokozi wetu alipounyesha ulimwengu kuwa yeye ni mbarikiwa wa baba tuna kila sababu ya kusifu na kushangilia. Huku tukijitathimini wenyewe jinsi ambavyo tunanashindwa kuzitumia vizuri funguo za uzima ambazo tumepewa. Yesu aliliona tatizo hili tukisoma Luka 11:52 Ole wenu ninyi wanasheria kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.

Yesu anawaonya wanasheria walikuwa wanatumia vibaya neema na maarifa ya funguo kwa kuto wafundisha watu wengine jinsi ya kutumia funguo za mbinguni ili waweze kufurahi neema ya maisha ya baadae hivyo wao wamekalia neema hiyo kwa faida yao pekee. Mathayo 13: 52 Akawambia, kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.

Funguo ambazo tumepewa zina nguvu sana ambazo zinaweza kufungua hazina na kutoa humo vitu vya thamani kubwa katika maisha ya Kiroho; katika imani funguo ambazo tumepewa ni za kufungua nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu juu ya maisha yetu.
Tafakari ya leo inatuonyesha nini faidia ya kuweza kupata elimu ya kutumia funguo za mbinguni? Funguo ambazo tumezipata tunaweza kuzieleza matumizi yake kama ifuatavyo: Unaweza kuziweka pembeni uzizitumie;  unaweza kuzibeba katika mifuko yako hivyo wakati unapotaka kuzitumia unakuwa na kazi ya kuzitafuta; na unaweza zivaa shingoni na ukapata urahisi wa kuzitumia.

Tatizo la kuzivaa funguo hizo shingoni ni ushahidi kuwa kila mtu ataziona na shetani atakuwa anakushawishi uzivue au uweke mahali ambapo hapaonekani mbele ya Macho ya dunia. Kama wakristo tunatakiwa tuone fahari ya kuzivaa na kuzitumia bila woga wowote. Je unaona aibu kusoma bibilia mbele ya yatu? Au kumtangaza Kristo mbele ya watu? Tukumbuke kuwa pale tunapovaa funguo zetu shingoni kunatupa sisi ujasili wa khali ya juu kuwa wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo. Na uko tayari kumpigania wakati wote.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumtoa mwanae yesu kristo ambaye alitufundisha kuhusu funguo za uzima wa milele, na Baraka zitokanazo na funguo hizo na ametusistiza kuwa lazima tuwe watu wa kuomba msamaha na kusamehe ili tuweze kuzitumia vyema funguo hizi .

Hii nitafakari yetu ya leo Amen

Emmanuel Turuka




Thursday, March 10, 2016

NI WAJIBU WETU KUWAHESHIMU NA KUWAPENDA WAZAZI WETU


Kutoka:20:12

March 10

Tafakari ya leo tunaangalia wajibu wetu kama watoto kuwapenda kuwajali wazazi wetu; hili sio ombi ni sheria ambayo Mungu ameiweka katika kitabu chake ambacho ndio mwongozo wetu katika maisha yetu ya kila siku ya ukristo wetu. Kama tunavyo soma katika kitabu cha kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Hata katika 2 Timotheo 1-2 inatukumbusha kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu wakuwa wenye kujipenda wenyewe, na kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukanana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio wasafi;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuwaheshimu wazazi wetu, na sio kuwaheshimu, viongozi wa serikali, au walimu au marafiki, wafanyakazi wenzetu bali wazazi wetu; siri kubwa hapa ni kuwa tukiweza kuwaheshimu wazazi wetu, tukifanya hivyo  mahusiano mengine yote yatakuwa rahisi katika kuyatekeleza. Heshima inaanza nyumbani; kama huwezi kuwaheshimu watu wa nyumba yako utawezaje kuwaheshimu watu wengine wa mbali? Ndio maana shetani anafanya jitihada kubwa ya kuharibu uhusiano mzuri kati ya Wazazi na watoto ili wasitimize adhima yao kutekeleza amei hii ya Mungu bali tuangamie;

Tafakari yetu leo hii inatukumbusha kuwa jinsi tunavyoweza kuwaheshimu na kuwapenda wazazi wetu ndivyo itakavyo kuwa rahisi kwetu kumpenda na kumheshimu Mungu. Huu ni muhimili mkubwa sana katika maisha yetu; wazazi ni kiungo muhimu sana kati yetu na Mungu na wao wanamwakilisha Mungu hapa duniani. Hapa ndipo wazazi wetu wanatakiwa kuwa makini kwa sababu Sisi watoto tunafahamu kwa wao ndio wawakilishi wetu wa kwanza hapa duniani na jinsi taswira ya matendo yao kwetu inakuwa aina ya Mungu ambaye sisi tunamwona kupitia kwao.

Kama wazazi wetu hawawezi kuonyesha mfano mzuri wa maisha yao kwa watoto; sisi tunamjua Mungu wetu na Hulka zake; je sasa mungu tunayemwona kupitia kwao ni Mungu wa upendo, neema, wa msahama, mafanikio? Au Mungu tunayemwona kupitia kwao anageuka kuwa Mungu wa Tamaa za mwili, Uzinzi, hasira, wizi, mkatili, mnyanyasaji na kadhalika?

Tafakari ya leo inatukumbusha  kuwa Baba na Mama wamepewa nafasi kubwa sana katika maisha yetu; na tunatakiwa kuwaheshimu wote katika uzito sawa. Ni wajibu wetu kuwatii na kuwaheshimu kwani Mzazi mwema hatakuwa sababu ya wewe ufanye dhambi yeyote ile. Waefeso 6: 1-3  Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki:  Waheshimuni baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kuonyesha adabu kwa wazazi wetu tunapoongea nao hasa kwenye hadhara ya watu na hasa mbele ya watoto wetu; hata kama hatukubaliani nao yale wanayosema bali tunaowajibu wa kuonyesha adabu na uvumilivu. Tukumbuke kuwa jinsi ambavyo tutakuwa tunawawatendea wazazi wetu ndivyo hata watoto  wetu watakavyo tutendea.

Tafakari ye leo inatukumbusha kuwa Mungu ndio asili ya uhai wetu lakini wazazi wetu ni kiungo muhimu ambacho Mwenyezi Mungu alikichagua katika kutuleta sisi duniani. Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wazazi kwa kweli wao ndio wanakuwa waaribifu wa maisha ya watoto  wao. Lakini bado kama watoto tunatakiwa tuwaombee na wapate msamaha wa Mungu lakini bado tunawajibu wa kuwaheshimu.

Mungu anajua machungu yote ya nyuma lakini anangalia leo yetu na kesho yenye faraja katika maisha yako. Ndio maana anatuambie leteni mizigo yenu kwangu name nitibeba kwa ajili yenu. Tukumbuke kuwa pamoja nay ale yote yaliyotokea katika maisha yetu bado sisi ndio pekee tutayoyajenga maisha yetu. Hivyo itakuwa vyema kama tutaweza kuishi maisha yenye uadilifu, mafanikio na furaha ya kweli na wazazi wetu watutupenda kwa hilo.

Tunafahamu kuwa wakati mwingine inakuwa vigumu kutekeleza amri ya msamaha dhidi ya wazazi wetu kwa makosa yao ya makusudi na kusababisha kukosekana kwa upendo kati ya watoto na wazazi kama tatizo, la utoaji mimba, ubakaji na kadhalika; matendo kama haya hupoteza kabisa upendo wa mzazi kwa motto; hivyo mtoto anakua katika maisha hatarishi na mtoto anajenga hasiri ya kulipiza kisasi cha kutaka kuua na kuwa huru kutoka katika minyororo ya wazazi wa namna hii. Mara nyingi tunawaona wazazi wetu kama vikwazo katika maisha yetu na sio kisima cha busara cha kutusaidia sisi kusonga mbele.

Ndio maana mwenyezi Mungu anatukumbushga leo katika mazingira ya namna yeyote yale bado tunawajibu wa kuwaheshimu wazazi wetu na kuwaombea kwa Mungu. Huku tukiwasamehe dhambi zao. Mungu alipoweka hii amri ya kuwaheshimu wazazi wetu alijua kabisa wazazi ni chanzo cha familia na nyumba ndio msingi mkubwa wa jamii na jumuia zetu; na hakuna jumuia zetu zinataweza kuwa na msingi imara kama hatutakuwa na familia bora ambazo zinajenga jumuia hizo; kinachofanyika nyumbani ndicho kinachofanyika katika jumuia zetu;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tukiyaangalia maisha yetu huko nyuma tunaona kuwa tumekuwa watoto ambao kwa namna moja au nyingine hatukuwapa heshima inayotakiwa kwa wazazi wetu, tume waonyesha kiburi, dharau na hata kuto fuata ushauri wao. Lakini bado ninakila sababu leo kusema asante sana Mungu kwa kunijalia wazazi ambao wamenilea na kunifikisha hapa nilipo leo. Ni ukweli kuwa katika namna moja au nyingine pengine hatukubaliana nao katika baadhi ya mambo; na pengine walitutendea vibaya lakini yoye ya yote tunatakiwa kuwasamehe ili tuweze kutembea katika amri hii ya Mungu tunatakiwa kuwaheshimu wazazi wetu na kuwapenda. Hii ni amri na wala sio ombi na hatuna njia ya kukwepa amri hii. Wazazi wetu wanastahili heshima kwa upendo wote ambao tunastahihi kuwapa.

Hii ndio tafakari yetu ya leo. Ameni

Emmanuel Turuka