WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, January 6, 2016

BABA KAMA ULIVYOTUFUNDISHA KUSALI



January 6

Tafakari ya leo hebu tusali pamoja tukimshukuru Mungu kwa wema na ukuu wake kwetu;

Eh Baba kama ulivyotufundisha  kusali katika sala kuu  ya Bwana ambako tunautukuza ukuu wako na pili tunaomba msamaa wa makosa yetu na hatiamye tunaomba Baraka ya mahitaji yetu na kuutukuza ukuu wako;

Tunatakiwa kuhesabu furaha tupu tunapopatwa na majaribu mbalimbali, kwa sababu tunajua ya kuwa kujaribiwa ndani ya imani yetu huleta saburi.  Saburi na iweze kufanya kazi yake inatakiwa kuwa timilifu, ili tupate kuwa wakamilifu,  na hivyo tutakamilishwa, bila kupungukiwa na kitu cho  chote. 

Tunafahamu kuwa mara nyingi miongoni mwetu  tunapungukiwa na hekima na ndio maana tunazidi kukuomba wewe Mfalme wa wafalme , wewe uliye Alfa na Omega uzidi kuayasikiliza maombi yetu na utujalie kuupata msaada tuuombao, tunafahamu kuwa wewe ni  mwenye ukarimu na wala huna kinyongo,.

Lakini  umetufundisha kuwa tuombapo inatupasa kuwa na imani na  kuamini na  kutokuwa na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama  wimbi la bahari, lililochukuliwa  na upepo na kutupwa huku na huku.  Mtu kama huyo  tusidhani ya kuwa atapata kitu cho chote kutoka  Kwako. Yeye ni mtu mwenye nia mbili,  mwenye kusitasita katika njia zake zote.

Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri,  ili tupewe rehema na kupata neema ya  kutusaidia wakati wa mahitaji na Maombi yetu, sisi sio wale wenye haki  tunatamani kuwa miongoni mwao kwani tunafahamu kuwa maombi ya wenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.  Tunamkumbuka Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi.  Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. Kisha akaomba  tena, mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake.  


Tunajongea mbele ya kiti chako kwa unyenyekevu tukiomba wingi wa huruma yako na utusikilize katika shida zetu, na utupe majibu ya maombi yetu. Amen

Tuesday, January 5, 2016

JE UNAWEZA FUKUZA SUNGURA WAWILI KWA WAKATI MMOJA?



January 5

Je umeshafikiria jinsi gani ni rahisi kupoteza muda wako katika kufanya au kufikiria vitu ambavyo sio vya maana katika maisha yako ya kila siku?

Tunahitaji kutafakari kwa khali ya juu jinsi ya kutumia muda wetu vizuri, na kitu kikubwa amabcho kinaweza kutusaidia katika kufikia tafakari ambayo ni nzuri, ni kuangalia muongozo ambao lazima tujiwekee katika maisha yetu ya kila siku. Bibilia inatuongoza kuwa kama tutaweza kuyangalia maisha katika kuruzi halisi tunaweza kujiepusha na matatizo mengi sana ambayo yako mbele yetu leo.

Tatizo kubwa tumejikita katika mambo ambayo hayana faida yeyote kwetu. Tukumbuke mwenyezi mungu baada ya kuumba mbingu na dunia na kumkabidhi Adamu utawala wa dunia hii pamoja na Hawa. Aliwaambia wafuate sheria na utaratibu ambao aliwawekea ambao ulikuwa raisi sana; ilikuwa jukumu tu la wao kufuata maelekezo. Lakini kwa vile hawakuzingatia mambo muhimu Nyoka aliwasaliti kwa kuwadanganya na walidanganyika. Matokeo yake walikosa kabisa maisha mazuri ambayo waliandaliwa na Mwenyezi Mungu. Mafano huu ni sawa na msemo usemao huwezi kufukuza sungura wawili kwa wakati mmoja kwani wote wawili watotoroka na hutaweza wakamata.

Ili tuweze kufanikiwa inatakiwa tuzingatie zaidi upande mmoja. Kama Bibilia inavyotukumbusha kuwa hatuwezi  kumtumikia Mungu na Mali au anasa za dunia hii; Ni jukumu letu kuchagua tumtumikie au Mungu au Mali kwa upande mwingine. Hatuwezi kumtumika mungu na Mali kwa wakati mmoja. Tukisoma kitabu cha Waefeso 5.17 kwa sababu hiyo msiwe wajinga bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya bwana.

Hatutakiwe tuwe wapumbafu na maisha yetu, tukumbuke kuwa tumepewa zawadi ya maisha kuishi mara moja tu hata kama tutakuwa na pesa nyingi au nguvu vyote ni vya msimu tu, bado tunatakiwa kuwa makini katika maamuzi yetu na mali zetu na nguvu zetu tunazitumiaje. Mwenyezi mungu anataka sisi wenyewe tujipangie nini tunataka na tutatumiaje?

Uzuri ni kuwa Mwenyezi Mungu anampango mzuri na kila mmoja wetu, lakini tatizo letu hatusikilizi sauti yake, tunaleta kiburi na kukataa kufanya kazi ya Mungu mfano wa Yona 1:2  alipoambiwa aondoke na kwenda ninawi, akapige kelele juu ya Mungu, lakini Yona akaondoka na kwenda Tarshishi, ili aweze kujiepusha na uso wa mungu lakini tunajua nini kilimtokea Yona. Mungu alituma dhoruba na Yona akatupwa baharini na kumwezwa na samaki mkubwa na kukaa ndani ya samaki huyo kwa siku tatu;

Tafakari hii ya leo inatufundisha kuwa lazima tuwe makini katika malengo yetu na vipau mbele vya uchaguzi wetu juu ya nini tunataka kufanya na kuwa; tunatakiwa kuwa makini katika kukisikiliza sauti ya Mungu, sio kukumbatia zaidi yale ambayo sisi tunayataka ambayo hayana faida kwetu ya kudumu kwani mwisho wa siku tumalizapo maisha ya hapa dunia tunajikuta tuko njia panda.

Tunatakiwa tukumbuke kuwa Mungu yuko kila mahali  na tunalijua hilo ila mara nyingi tunaendelea kumjaribu na huku tukifikiri kuwa Mwenyezi Mungu hatuoni na uovu wetu. Popote pale ambapo tutakuwa au tutakwenda yeye yuko, tujifunze toka kwa Yona pamoja na kubadilisha mwelekeo Mkono wa Mungu ulikuwa juu yake.  

Tunapokataa sauti na maelekezo ya Mungu ni  na maamuzi na ishara ya kiburi na ubinafsi. Ndio maana mwisho wa siku ni sisi tunakuwa tumefanya kazi ambayo haina malengo na mafanikio kwetu wenyewe. Tukisoma zaburi 139:7 inauliza je naweza kwenda  sehemu nyingine yeyote kuogopa roho wa bwana?

Lakini tukumbuke kuwa Mungu ambaye daima anaanzisha kazi nzuri ndani yetu yeye ndiye atakaye ikamilkisha ndani yetu kitabu cha Wafilipi 1:6; kinatueleza kuwa Mungu daima anafanya kazi ndani ya maisha yetu tunachotakiwa ni kuelekeza akili na nguvu zetu kwake na kuacha tabia ya kufukuza sungura wawili kwa wakati mmoja kwani tutapoteza malengo muhimu. Mungu anajua
nini kitu muhimu unachohitaji au unachotakiwa kufanya au kuwa, kinachotakiwa tu kwetu ni kumsikiliza na kutimiza wajibu wetu kama binadamu.

La msingi tunapopatwa na matatizo tunatakiwa kujiuliza nimefikaje hapa, uwe ni kiongozi wa serikali au raia wa kawaida au mtumishi wa Mungu.

Je unatenda haki kwa wananchi wako, wanatendewa vile mungu alivyokuagiza uwafanyie? Haki zao wanapata? Je kwa wananchi wa kawaida nasi tunatimiza wajibu wetu kwa serikali kama inavyotakiwa?

Je viongozi wa dini wanaisadiaje serikali na wananchi wake katika kusikia sauti ya Mungu?

La msingi katika tafakari ya leo sote tunafanya makosa  la msingi tunatakiwa kwanza tuweze kukiri dhambi zetu na kuwa tayari kuziacha, hii itatusaidi tuweze kupata nguvu mpya ya kuanza upya na hatutakiwi kurudia tena kosa la kufukuza sungura wawili kwa wakati mmoja . lazima tuchague kumfukuza mmoja ambaye atakuwa na faida endelevu kwako. Na kitabu cha 2 cha wakorinto kinatumbusha kuwa tunakuwa wapya na tunaweza kuanza malengo yetu mapya ambayo yatatupa dhawabu kubwa mbele ya Mungu.


Kwani yeye daima ana mipango mizuri juu yetu daima. Kama alivyo mpa Yona nafasi ya pili na alitimiza kazi ya kuhubiri na kuwakoa wale walikuwa wapotea. Tukumbukekuwa mungu yuko kila mahali, Mungu wetu ni wa msamaha daima hivyo hatujechelewa kupokea baraka za Mungu kwa mara ya pili. Amen  

Monday, January 4, 2016

JIRANI NI NANI




January 4

Tafakari yetu leo inaelekwezwa katika agizo la Yesu kwa wafuanzi wake na wananfunzi wake pale alipofundisha kuhusu amri ya Upendo kwa jirani kama tunavyojipenda wenyewe. Yesu angeweza tu kusema mpende jirani yako na kuishia hapo; lakini kwanini aliamua kuhitimisha kwa maneno haya “ Kama unavyojipenda Mwenyewe”?
Binadamu tuna huluka na silika ya kujipenda zaidi sisi wenyewe kuliko kumpenda mtu mwingine. Ni tabia ambayo tunayo na imekuwa vi vigumu kuondokana nayo; tafakari ya leo inatukumbusha kuwa agizo la Yesu ni la muhimu ili tuweze kuuridhi uzima wa milele lazima na jirani zetu tuwapende katika mizani ile ile tunayojipenda sisi wenyewe. Katika biblia kuna amri kuu mbili za upendo wa kumpenda Kwanza Mungu  kwa moyo wetu wote, na ya pili inafanana na hii  ya kwanza ya kumpenda jirani: “Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe.” (Mathayo 22:39) 

Hapa tuna jifunza kuwa kumpenda jirani, kama vile kumpenda Mungu, si hisia tu; ni jambo linalotakiwa lionyeshwe kwa matendo. Kuwapenda wengine kama tunavyojipenda wenyewe kunamaanisha kwamba tunawaona wengine kama tunavyotaka watuone na kuwatendea kama tunavyotaka watutendee. Golden Rule; ambayo msingi wake kiimani kuwa Mtu wa MUNGU ni yule aliyekaa katika pendo. Je wewe leo unajitambua kuwa umekaa katika upendo?

Tukisoma kitabu cha Walawi 19:17  kinatukumbusha kuwa : Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; na pale ambapo jirani yako hajefanya sawasawa ni lazima kumkemea jirani yako, hatuna sababu ya kuumia kimoyomoyo  na kutenda dhambi ya masengenyo dhidi yake; pale inatotupasa kumsahihisha jirani kwa upendo na tatufnji hivyo tunaishia kutenda dhambi  mbele ya mungu kwa malalamishi yetu juu ya jirani. Tunaweza kuirekebisha dhambi hii kwa kukwemea.

Mfano mwingine mzuri kuhusu upendo wa jirani  hadithi ya Yesu inayopatika katika kitabu cha Lk. 10:30 mtu aliyeshuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko na kuangukia katika mikono ya wanyanganyi  ambao walimpiga , kumvua nguo, walimwumiza na kumwacha karibu kufa; Tunaona Kuhani ambaye ni mtu anayejua sheria za dini na wajibu wake kwa jamii alikuwa akipita alimwona na kupita kando bila kutoa msaada wowote; Mlawi naye alifanya hivyo hivyo; lakini msamaria mwema yeye alifika mahali hapo na kwa matendo alionyesha upendo wa khali ya juu kwa kumfunga majeraha yake na kumpa huduma zote kama alivyoweza na kasha kuondoka naye na kumpeleka katika sehemu nyingine ambyo aliweza kupata matibabu zaidi kwa gharama zake. Msamaria mwema hapa ameonyesha upendo wa khali ya juu na hivyo yeye amekuwa jirani kwa  mtu hutu aliyekuwa akihitaji msaada.

Ni vigumu sana kutekeleza agizo hili la Yesu kama hatuna upendo wa kweli; tukumbuke kuwa tunda la Roho ni upendo, ambao utaleta  furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, na upole; kwa kutekeleza upendo huleta ujirani mwema na utekelezaji wa amri hii kubwa ya kupendana kwani huta mwia mwenzako na kitu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inakamilishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neon baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria”.

Tunaishia kuvunja amri hizi zote kwa sababu hatuna upendo ndani yetu; tukiwa tumetawaliwa na upendo, hatutaweza kuiba kwani kwa kuiba unamwibia jirani yako; kwa kusema uwongo unamkosea jirani yako ili kumletea matatizo ambayo hastahili kuyabebe. Ukizini unatenda kosa la kumsaliti jirani yako ambye ni mUme wako au Mke wako; kwa ufupi tukitimiza amri ya upendo inavyotatimwa hatuwezi kufanya dhambi yeyote, bali tutaweza kuishi maisha ya amani na upendo mkubwa sana kwa kujali na kusaidiana kama biblia inavyotaka sisi leo tuishi.

Basi siku ya leo tuendelee kutafakari nafasi yako au yangu katika kutekeleza amri hii kubwa ya upendo kwa matendo amen.



Sunday, January 3, 2016

Bwana Tufundishe jinsi ya kusali:

JANUARY 3



Hili lilikuwa ombi la wafuasi wa yesu, pamoja kuwa na yesu siku zote wafuasi wa Yesu walijifunza na walimwona yesu akitumia muda mwingi akiwa akiongea na Mwenyezi Mungu kwa sala. Na alikuwa akitumia muda huo akiwa katika faraga na sehemu ya utulivu; hali hii ilikuwa ni ngeni kwa wanafunzi ndipo nao walitamani kufanana na Yesu hivyo waliomba nao wafundishwe jinsi ya kusali.

Tunafahamu kuwa sala ni njia pekee ambayo inafungua njia ya mawasiliano na Mungu. Sala ni njia pekee ambayo inatuunganisha na mungu. Sala ni njia pekee ambayo inaonyesha ukuu wa mungu katika maisha yetu; sala ni nia pekee ambayo inaonyesha shukrani yetu, unyenyekevu wetu, na kuomba msamaha kwa mungu;

lakini tukumbuke kuwa maombi pia yanaunganisha mioyo yetu na akili zetu ambazo zinaleta utulivu kwani mwili wako ndio hakelu la bwana, hili ni kanisa ndani yako; tukisoma kitabu cha James 4: sala hutupatanisha na Mungu; sala huleta upatanishi miongoni mwetu, huwezi kuwa mpatanishi kama hujui jinsi ya kuomba; upatanishi msingi wake mkubwa ni unyenyekevu na unyenyekevu hutoka na uwezo wetu wa kuongea na Mungu; ndio maana wapatanishi wanaitwa wana wa Mungu; tukisoma Matayo 5:9 anafafanua zaidi.

yesu alipokuwa akihubiri kuhusu upatanishi alikuwa akiliongelea hili katika maana pana sana. Hakuwa anaongelea tu kuwa kuna mtu mmoja ambaye anawajibu wa kuleta upatanishi pale ambapo tunafikiri kuwa kuna khali ya kutokuwa na amani; Yesu alikuwa anatuagiza sisi sote kuwa jukumu la luleta upatanishi ni letu sote.lakini upatanishi wa kweli utapatikana kama tunajua jinsi ya kusali; jinsi ya kuongea na Mungu kama Yesu alivyokuwa.

je tunajua kuwa amani huleta haki na furaha ya maisha? Na amani ya kwelihupatikana kwa sala ambayo hutufanya sisi kuwa wanyenyekevu.

Kwa hiyo tukiendelea na tafakari yetu katika mwaka huu tukumbuke kuwa sisi nasi leo tunatakiwa kuendelea kuomba kufundishwa jinsi ya kusali kama wafuasi wa Yesu walivyo omba kufundisha na Yesu aliwafundisha.

Saturday, January 2, 2016

YESU ANASEMA NJONI KWANGU NIPO KWA AJILI YENU.



JANUARY 2

Tukisoma kutoka katika kitabu cha 2 cha Wakorito 4:7; matatizo na majaribu ambayo tunakumbana nayo katika maisha yetu ya kila siku bililia inatueleza ni ya muda tu kama tunaamini ukuu wa Mungu. Jukumu letu ni kuamini katika ukuu wa kazi ya Mungu. Tunatakiwa kuendelea kuamini kuwa tukiweza kufungua mioyo yetu na kuukaribisha utakatifu wake ndani yetu tutafanikiwa; lakini bila nguvu ya Mungu sisi sio kitu na hatuwezi kitu chochote. Uwezo wa kufikiri, uwezo wa ubunifu, uwezo wa kuongea vizuri na hata mafanikio yote ambayo leo tunajivunia ni zawadi kutoka kwake. Nani aijuaye kesho? Kesho iko mikononi mwa Mungu peke yake;

Kumbusho kubwa hapa ni hili hakuna kitu chochote kinachoshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu; hata kama tunakuwa na shida au maumivu tunakumbushwa kuwa maumivu ni sehemu ya maisha na ukuaji wa maisha ya ukristo ndani yetu. Tunatakiwa kutumia maumivu tunayoyapata katika maisha yetu ni sehemu ya kukua kwetu kiimani.Tunaaswa kuwa ushindani mkubwa amabo daima tunapambana nao ni mapigano ambayo yapo ndani ya miili yetu yetu kati ya nguvu ya mwili na nguvu Roho; Nguvu ya mwili ina jumuisha: matamanio ambayo ndio yanatawala maisha yetu kwa kiasi kikubwa kama, choyo, ubinafsi, kutukuwa na subira; kushindwa kujishusha hii inahitimiswa na dhana ya kuwa sisi ni wafalme wa maisha yetu na hatuhitaji msaada wa Mwenyezi Mungu katika mafanikio yetu hapa duniani.

Nguvu ya roho ni ile khali ya kumtegemea Mungu kuwa yeye ni kila kitu kila jambo nzuri au bay ambalo lio mbele yetu ni kazi ya mikono yake na inatupasa kushukuru; Unyenyekevu ni silaha inayotumika kwa wale wote ambao hutegemea nguvu ya Kiroho; Hapo ndipo yesu anajidhihirisha kwa usemi huu wa Njoni kwangu nami nitawasaidia katika shida zenu;Mungu pekee ambaye yeye hutuongoza katika mapito yake ambayo ni sahihi lakini tunatakiwa tuweze kusikia sauti yake ili uweze kukanyaga kwenye mapito yaliyo sahihi;

Mara nyingi tunaendelea kulalamika kuwa Mungu hasikilizi shida zetu na kwa nini shida zetu zinaendelea kudumu kwa muda Mrefu? Tatizo ni dogo tunashindwa kuwa wanyenyekevu wakusikiliza sauti yake bali sisi tunaendeleza kiburi chetu na tunajifanya hatusikia sauti ya bwana na huo ndio unakuwa mwanzo wa upotevu.

Tunatakiwa kusikiliza neno la mungu ambalo ndilo ngao kwani neno la mungu ni ngao salama kwa ajili ya ukombozi wetu na baraka katika maisha yetu. Ni kweli kabisa unaweza pita katikati ya bonde ka mateso kumbe likawa linakutayarishia na kukujengea daraja la baraka.Tumesahau kuwa kama tunaishi katika imani ya kweli tukumbuke kuwa daima mungu hugeuza kilio kuwa furaha kubwa sana sana.

Jukumu letu la msingi ni kuwa tayari kubadilika na kumwamini Kristo kama ni njia pekee ya utatuzi wa maumivu katika maisha yetu; tukumbuke kuwa maumivu tunayoyakabili kila siku yanaweza tu kukoma kama tutakuwa tayari kumkaribisha Kristo ndani ya maisha yetu. Kwani alitueleza kuwa njoni kwangu wote wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapa faraja tukikumbuka kuwa yeye anapobeba mizigo yetu huondoa kabisa maumivu sisi wenyewe hatuwezi kuyaondoa.

siku ya leo inatupasa kutafakari kuhusu umuhimu wa kujijengea IMANI ya kweli ili tuweze kufanikiwa katika kufanikiwa katika maishayetu. Endeleaa kutembea nami katika tafakari hii muhimu ya maisha yetu na kuutafuta soluhisho la kweli kuhusu mizigo yetu.


Friday, January 1, 2016

TAFAKARI YA KILA SIKU

                                                         JANUARY 1

Leo tunapoanza mwaka mpya 2016 tuna kila sababu ya kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa upendo wake kwetu na kwa familia zetu. Tuendelea kujiuliza tumpe  Mwenyezi Mungu kwa upendeleo huu mkuu wa kuweza kuiona siku hii mpya katika mwaka huu mpya? Je mimi/wewe tunaupekee gani tofauti na wale wote ambao wameitwa katika pumziko la milele? Kwa baraka na neema hii kubwa sisi sasa tunatakiwa tumrudishie nini mungu wetu? Je mwaka huu mpya kwetu una maana gani?
Je nini tunatakiwa kutafakari katika mwaka huu 2016?

Niliyoyafanya mwaka 2015 yote yalimpendeza Mungu au yalikuwa yananipendeza mimi mwenyewe?
Mwaka huu mpya tuiwekee nadhiri ya kuyaacha yote ambayo yalikuwa hayampendezi Mungu na kutuletea utengano naye; tukisoma kitabu cha waefeso sura ya 5:14-18 mtume Paulo anatukumbusha kuwa kwa matemdo yetu mabaya anatuasa tuamke na kubadilisha tabia kwani hakuna mtu mwingine yeyote atakaye ibadilisha tabia yangu/yako isipokuwa mimi/wewe mwenyewe. Njia pekee ni kumkaribisha kristo Yesu ambaye ni mwanga katika mabadiliko ya maisha yetu.

Mwaka wa 2016 uwe ni mwaka wa matendo yanaendana na kutumia muda wetu vizuri kwa utukufu wa mungu, kutisoma kitabu cha waefeso sura ya 6 Mwenyezi Mungu ametupa uwezo wa kutumia kila kitu, kwa kupambanua uthamani wake mbele ya mungu na utukufu wake. Inatakiwa tukumbuke kuwa yesu ni sadaka yetu pekee kupitia damu yake takatifu iliyomwagika msalabani kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu, na hatuhitaji hata kidogo msamaha mwingine wa dhami zetu, kama kitabu cha John 3:16 kinavyotukumbusha, sisi tunachotakiwa kuwa hekalu la Mungu ambaye ataishi ndani yetu. Sasa kama ukimkarisha mungu ndani yako unahitaji nini tena?

Zaburi ya 46:10 inatuonya kuwa sisi binadamu daima tunafanya vitu kwa uwezo wetu baada ya kutegemea nguvu za Mungu, na tunajivuna sana kama tukiona kuwa tumefanikiwa na kudharau nguvu ya Mungu. Lakini tunajisahau kuwa maisha yetu sio chochote na hatuwezi kuyamuda hata kidogo. Tukumbuke kuwa katika mazingira yeyoye yale, mungu peke yake ndiye anayeongoza na kutawala maisha yetu.

Katika mahangaiko, hofu, mashaka na mafanikio ya maisha yote naamini kuwa mungu peke yake ndio daraa pekee la mafanikio yangu/yako na familia yangu/yako. Mimi binafsi naamini kuwa kwa namana yeyote ile mafanikio yangu ni baraka pekee kutoka kwa Mungu juu yangu. Ninatembea katika ushindi mwaka huu wa bwana kwa sababu kubwa moja kuwa mimi daima natembea na bwana. Kama mwenjili Luka 1.28 anavyosema kuwa Mungu yu pamoja nami; kinachohitajika ni uwezo wa kusikia sauti ya kimungu ndani yetu hiyo ndio msingi wetu wa mafanikio na imani yetu ya ushindi wa mafanikio yetu.


Mwenjili matayo katika sura ya 7:8 anatukumbusha kuwa kwa yeyote ambaye anaomba hupokea, na yule atafutaye huona na yuke abishae hufunguliwa. Kwa hiyo tunatakiwa kuwa na imani na uthabiti na unyenyekevu ili tuweze kuuridhi utukufu na neema ya kimungu juu ya maisha yetu. Hatutakiwi kukata tamaa hata kidogo. Isipokuwa tunatakiwa tuendelee kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake kwetu kwa kuendelea kusali kila siku na kila wakati bila kuchoka. Hatutakiwi kukata tamaa kwa kuchelewa kupata matokeo ya maombi yetu. Daima mwenyezi Mungu anafanya kazi katika utukufu wa maficho yake kwa faida yetu sisi. Na tusifahau kuwa majira ya mungu kwetu ni ya uhakika sana sana lakini kama tunaenenda katika imani.

Nakutakia safari njema ya Tafakari katika mwaka huu 2016 tembea nami kila siku katika kusifu na kumshukuru mungu kwa mema ambayo ameendelea kutenda juu yetu .Amina