Tafakari yetu ya juma hili tunaangalia dhana ya
woga katika maisha yetu; woga ni kielelezo kuwa kuna kitu kimesimama katika
njia mbayo tunastahili kupita; lakini pengine kwa mantiti ya ukweli kabisa
hakuna kitu cha namna hii; woga huleta wasiwasi na kutufanya kushindwa
kufanikiwa malengo yetu; woga hutupotezea kabisa uwezo wetu wa kufikiri na
kufanya maamuzi sahihi wa kufikia malengo ambayo ndio lengo la mafanikio yetu;
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa vizuizi
kama woga visiwe kikwazo katika maisha yetu hasa ya kiroho tunakumbushwa hata
tukijikwaa kwenye ukuta ni lazima
tukubali kuwa kujikwaa sio mwisho wa safari. Woga ambao husabibisha akili zetu
kudumaa lazima upate ufumbuzi ndani ya akili zetu. Akili zetu lazima zijue kuwa
kushindwa kunakutokana na woga hatupaswi kutoa nafasi kwani bibilia inatukumbusha kuwa neema
yake inatosha katika shida zetu. Woga utupe sisi ujasili wa kupata ushindi;
kushindwa kunakosababishwa na woga kuwe sehemu ya ushindi; Yesu alipokuwa
akitembea juu ya maji wafuasi wake walishituka na kujawa na woga wakifikiri
kuwa wameona ni jini; walipomtambua kuwa alilikuwa Yesu Petro akamwambia Yesu
bwana nami naomba nitembee juu ya maji Yesu alimwita akamwambia njoo, alianza
vizuri lakini kwa vile alileta silaha ya woga akaanza kuzama.
Je woga wetu hutoka wapi? Woga katika maisha
yetu huletwa na watu wengine, pengine tunatamani kumpendezesha kila mtu, au
kuishi kwa matarajio ya maisha ya watu wengine na kwa macho yao hivyo kwa kuishi katika maisha ya namna hiyo
huweza kutupa sisi wakati mgumu sana; lazima kutakuwa na vizingiti vingi sana
lakini bado hatutakiwa kukubali kuwa vikwazo vituzuea katika maisha yetu.
Tunatakiwa kuwa tayari kuruka vihunzi, na daima macho yetu yawe yanangalia
mpira ili tuweze kushinda na sio kuwa watu ambao tumejaa woga. Tukiwa na mawazo
ya kushindwa sio sehemu ya ushindi; kushindwa ambako kunatokana na woga ni
ishara ya kutuambia sisi kuwa hatuko sawa;
Najua kabisa hatuwezi kuepuka woga lakini woga
usitawale maisha yetu, hata Yesu alitawaliwa na woga alipokuwa katika bustani
kabla ya safari ya mateso yake lakini kwa ujasiri mkubwa aliushinda woga na
kuweza kubeba kikombe cha mateso kwa ujasiri mkubwa hatimaye kuleta ukombozi
kwetu sote kwa damu yake pale msalabani.
Tukiendekeza woga basi tumeshajiwekea sisi
wenyewe dalili kubwa ya kushindwa;woga unatakiwa utufundishe sisi na kutuletea
mageuzi na kutufanya kuwa watu bora zaidi. Tunaposoma kuhusu maisha ya jehanamu
tunajawa na woga; basi Woga huu unatakiwa utusaidie sisi tuyafuate maelekezo ya
mungu katika kuishi maisha bora ambayo yanampendeza Mungu wetu. Hivyo woga utujengee
sisi ushindi kama Yesu alivyofanya na leo tumekombolewa kupitia damu yake
takatifu sisi sana kwa ukombozi huu jukumu letu ni kufanya matendo mema ambayo yanampendeza
Mungu.
Ni jambo nzuri ambalo sisi binadamu
tumewekewa Mwenyezi Mungu alijua uzaifu wetu kuwa kwa kushindwa kwetu ambako
kunatokana na woga awetu tumewekewa namna ya kuweza kuomba msamaha. Ndio
maana ya kipindi hiki cha toba, kipindi
hiki ni alama tu ambayo tunatakiwa kuishi kwa namna hii katika maisha yetu
yote. Natukiweza kuishi katika namna hii tutakuwa tumefanikiwa sana sana.
Kristo ametuonyesha mfano kuwa yeye aliweza kusimama kidete katika kutuonyesha
mfano maisha yale ambayo Mwenyezi Mungu anataka sisi tuishi; tumepewa nafasi ya
pili ya kujirekebisha na kuishi bila kutanguliza woga mbele bali kutanguliza
ushujaa wa kumpigania Yesu; tunatakiwa tutambue udhaifu wetu na kupata nguvu za
kuukabili udhaifu huo; tubadilishe tabia zetu;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa pamoja na kukabiliwa maisha wakati mwingine yanakuwa magumu sana; kupitia kipindi hiki cha mfungo na kumrudia Mungu
tumepata nafasi nyingine nzuri sana na ya ajabu sana; Mungu anaendelea
kutujalia sisi siri kubwa ya ushindi wa maisha yetu na mbinu za kumshinda
shetani; lazima tukubali kuendelea kujifunza na kuwa tayari kubadilika; maisha
ya ushindi ni magumu na kuwa mwoga haitasaidia kushinda vikwazo ambavyo
vinachelewesha ukamilifu wa safari yetu hapa duniani bali lazima tusimame imara
na kuamini kuwa bila nguvu za kristo ndani yetu sisi wenyewe hatuwezi kuipigana
vita hii kwa ushindi mkubwa; woga wetu utaendelea kuwako bali tukimpokea Kristo
woga hauna na nafasi hata kidogo. Maisha yatendelea kuwa mazuri kwa wale
wanaomwamini kristo na wako tayari kufa pamoja naye. Woga wako ukimtegemea
kristo hauna nafasi kabisa na utakuwa huru; tufunge na Kristo na tufe naye
msalabani kwa kuishi maisha yale ambayo kristo aliishi na kuwa alama ya
ukombozi wetu ;
Huu ndio ujumbe wetu wa wiki hii ya kwaresma.
Amina Amina Amina
Emmanuel Turuka
2017
No comments:
Post a Comment